Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,240
- 9,527
Katika press conference aliyoifanya Mkurugenzi wa makosa ya jinai Tanzania - CP. Robert Boaz, amegusia mambo kadhaa ambayo mimi pamoja na kutokuwa muelewa sana wa sheria naingia wasiwasi kwamba yanaweza kuinfluence mwenendo wa kesi!
1. Anatoa pongeze kwa wote waliohusika kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na upelelezi unakamilika kwa hatua ya kwanza kwa watuhumiwa kuweza kufikishwa mahakamani.
2. Anaongelea kiasi cha madarasa ambayo yangeweza kujengwa au madawati ambayo yangeweza kununuliwa kwa kiasi cha fedha ambacho kingeweza kupatikana kwenye mauzo ya hiyo dhahabu.
3. Anaongelea ugumu wa vita ya kiuchumi na umuhimu wa kumùunga rais mkono kwa kuwa wazalendo ili kuhakikisha taifa linafaidika.
Kwa macho ya kawaida kabisa na moyo mweupe nampongeza sana CP. Robert Boaz kwa hii speech yake ambayo inawaweka wananchi 'up to date' kwa kila kinachoendelea kwenye kesi hii.
Kwanza sijawahi kusikia kashfa yoyote popote inayomhusu Boaz na hivyo sina mashaka na nia yake hiyo njema.
Pili namshukuru kwa kuweka uhalisia wa thamani ya hiyo dhahabu kutoka trillion 3 zilizokuwa zikitajwa na RC Mwanza na wanahabari mpaka billion 27.
Narudi kwa upande wa hakimu atakayehukumu hii case;
1. Kama kuna watu wanapongezwa tena baada tu ya case kuanza kwa kufanya kazi kubwa kuhakikisha hawa wahalifu ,na sio washukiwa wa uhalifu, wanafikishwa mahakamani, hakimu ataweza kweli kwenda tofauti na kazi hii kubwa inayopongezwa na CP kwenye maamuzi yake?
2. Hiki kiasi cha madarasa ambacho kingeweza kujengwa au madawati ambayo yangeweza kununuliwa, kama vile dhahabu hiyo imekwapuliwa hazina, hakiwezi kumfanya mheshimiwa hakimu ajisikie mnyonge kutoa hukumu kama akiona inaweza kutofautiana na uzalendo wa CP?
3. Kama itaonekana hawa washtakiwa wana haki, hakimu si atakuwa anakwamisha vita ya kiuchumi anayopigana rais wetu na atakuwa hamuungi mkono kwenye uzalendo?
Nimejaribu kutafakari haya ila naomba mwangaza zaidi kwa wale wanaoielewa kidogo sheria na kama kuna 'influence' yoyote hapa, isijekuwa tu ni my own ignorance of the law!