'Muendelezo' alioutoa CP. Robert Boaz leo Mwanza hauta influence mwenendo wa kesi?

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,239
9,527
Katika press conference aliyoifanya Mkurugenzi wa makosa ya jinai Tanzania - CP. Robert Boaz, amegusia mambo kadhaa ambayo mimi pamoja na kutokuwa muelewa sana wa sheria naingia wasiwasi kwamba yanaweza kuinfluence mwenendo wa kesi!

1. Anatoa pongeze kwa wote waliohusika kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na upelelezi unakamilika kwa hatua ya kwanza kwa watuhumiwa kuweza kufikishwa mahakamani.

2. Anaongelea kiasi cha madarasa ambayo yangeweza kujengwa au madawati ambayo yangeweza kununuliwa kwa kiasi cha fedha ambacho kingeweza kupatikana kwenye mauzo ya hiyo dhahabu.

3. Anaongelea ugumu wa vita ya kiuchumi na umuhimu wa kumùunga rais mkono kwa kuwa wazalendo ili kuhakikisha taifa linafaidika.

Kwa macho ya kawaida kabisa na moyo mweupe nampongeza sana CP. Robert Boaz kwa hii speech yake ambayo inawaweka wananchi 'up to date' kwa kila kinachoendelea kwenye kesi hii.

Kwanza sijawahi kusikia kashfa yoyote popote inayomhusu Boaz na hivyo sina mashaka na nia yake hiyo njema.

Pili namshukuru kwa kuweka uhalisia wa thamani ya hiyo dhahabu kutoka trillion 3 zilizokuwa zikitajwa na RC Mwanza na wanahabari mpaka billion 27.

Narudi kwa upande wa hakimu atakayehukumu hii case;

1. Kama kuna watu wanapongezwa tena baada tu ya case kuanza kwa kufanya kazi kubwa kuhakikisha hawa wahalifu ,na sio washukiwa wa uhalifu, wanafikishwa mahakamani, hakimu ataweza kweli kwenda tofauti na kazi hii kubwa inayopongezwa na CP kwenye maamuzi yake?

2. Hiki kiasi cha madarasa ambacho kingeweza kujengwa au madawati ambayo yangeweza kununuliwa, kama vile dhahabu hiyo imekwapuliwa hazina, hakiwezi kumfanya mheshimiwa hakimu ajisikie mnyonge kutoa hukumu kama akiona inaweza kutofautiana na uzalendo wa CP?

3. Kama itaonekana hawa washtakiwa wana haki, hakimu si atakuwa anakwamisha vita ya kiuchumi anayopigana rais wetu na atakuwa hamuungi mkono kwenye uzalendo?

Nimejaribu kutafakari haya ila naomba mwangaza zaidi kwa wale wanaoielewa kidogo sheria na kama kuna 'influence' yoyote hapa, isijekuwa tu ni my own ignorance of the law!
 
2.Hiki kiasi cha madarasa ambacho kingeweza kujengwa au madawati ambayo yangeweza kununuliwa, kama vile dhahabu hiyo imekwapuliwa hazina, hakiwezi kumfanya mheshimiwa hakimu ajisikie mnyonge kutoa hukumu kama akiona inaweza kutofautiana na uzalendo wa CP?

Wewe unazidisha hofu tu kwa mambo unayoyahofia wewe kwa vile hujui sheria.

Acha kesi iungurume mahakamani, na kila upande utoe walichonacho mbele ya sheria. Na sheria ndio itakayoamua kutokana na ushahidi uliotolewa.

Tukiendelea kuhofia kila mara yanayosikika mitaani ina maana mahakama basi zisiwepo?

Kazi ni moja tu, acha waliosomea na kubobea katika maswala ya sheria wafanye kazi zao.

In fact, hii ni kesi ambayo hakimu atakayeisimamia akiiendesha sheria ipasavyo atajiongezea sifa. Afanye kazi bila kujali nani anasema nini.

Na hapo hapo, kumbuka kwamba uamzi wa hapo mahakamani sio mwisho wa kesi kwa vyovyote itakavyoamriwa. Kama patakuwepo asiyeridhika na uamzi, si bado atakuwa na nafasi ya kwenda mahakama ya juu zaidi? Na uamzi ukitolewa eti kwa kufikiria madarasa yatakayojengwa bila ya kuangalia ushahidi uliotolewa, si hata wewe usiyekuwa na ufahamu wa sheria utaona jinsi mahakama zetu zisivyokuwa na mamlaka?

Ni mambo kama haya ndio yanayofanya watu wengi wapige kelele kuhusu mamlaka ya mahakama. Wewe tayari umekwishaamua kuwa mahakama haitatenda haki, kwa vile tu maneno yamesemwa nje ya mahakama; lakini bila ya kuwa na ushahidi wowote unaoonyesha kwamba mahakama hazitendi haki!.

Hujaonyesha popote katika taarifa yako kuonyesha kwamba mahakama imeshindwa kufanya kazi zake kwa kuingiliwa mamlaka yake. Kwanini usivute subira hadi uamzi wa kesi utakapotolewa na sote tujiridhishe kuwa haki haikutendeka kwa sababu ya maneno yaliyosemwa nje ya mahakama.
 
Ni mambo kama haya ndio yanayofanya watu wengi wapige kelele kuhusu mamlaka ya mahakama. Wewe tayari umekwishaamua kuwa mahakama haitatenda haki, kwa vile tu maneno yamesemwa nje ya mahakama.

Lakini hujaonyesha popote katika taarifa yako inayoonyesha kwamba mahakama imeshindwa kufanya kazi zake kwa kuingiliwa mamlaka yake. Kwa nini usivute subira hadi uamzi wa kesi utakapotolewa na sote tujiridhishe kuwa haki haikutendeka kwa sababu ya maneno yaliyosemwa nje ya mahakama.
Kiongozi mimi ni mpenzi wa mpira wa miguu. Unajua kawaida ukiona unaanza kuchezewa rafu unanyoosha mikono juu ili refa aone mapema.

Kwenye mpira ukijifanya tafu sana unaweza kuvunjwa na refa asitoe kadi!

Mimi nimeona hii game imeanza na rafu dakika za mwanzo tu!
1. Kwanza RC Mwanza alishaihukumu
2. Kisha mheshimiwa rais akaelezea 'mchezo ulivyokuwa' na kumuelekeza waziri kwamba hiyo dhahabu inaweza kutuongezea fedha za kigeni.
3. Leo CP. Boaz amegongea msumari mwingine kwenye jeneza wakati kesi imeshatajwa.

Nadhani wakili wa hawa watuhumiwa anapaswa kuraise his concerns mapema mahakamani!

Tena kwa vile mheshimiwa Rais alimwambia Jaji Mkuu kwamba 'anampa fedha anayoomba halafu aone serikali ikishindwa kesi mahakamani!' na ukiangalia mwenendo wa issue yenyewe mpaka sasa unapata wasiwasi kuwa kinachoendelea mahakamani ni formality tu!

Game ilishaisha.
 
Tumeingiza siasa mpaka kwenye mambo yanayohitaji ujuzi...

RC sio mkadiriaji wa thamani ya dhahabu ila akakurupuka

CP naye anatoka nje ya mada kwa kutengeneza mwelekeo wa kesi

Lakini je ni nani kathibitisha kama kweli ile ni dhahabu halisi? Kwa kipimo gani? Je ndani yake hamna kanyaboya?
 
NAWAONA KWA MBAAALI WATUHUMIWA WAKIWA HURU.
Naam, labda hilo ndio lengo la Boaz kuwaokoa askari wake kisayansi bila kushtukiwa na Mzee baba au nyie "wazalendo".

Hivi CP Boaz na ujuzi wake wa sheria hajui kuwa kauli kama hizo Kwa kesi iliyo mahakamani na chini ya hakimu mkweli na makini na challenge za wakili mbishi anapoteza?

Anajua hivyo, lakini anajua pia Kwa kauli hizo hawezi kupoteza Kwa Mzee baba.

Huu nao ni uhujumu uchumi Kwa kutumia weledi na kauli
 
Kama kawaida yenu mambo yote ya awamu hii kwenu ni ya is hata ya kushindwa au Yana ishara mbaya, iwe imefanywa Na Rais, iwe ni CRDB, iwe mtu wa idara nyingine yeyote wakati CRDB ilikuwepo awamu iliyopita lakini sikusikia kelele za wachoma mishikaki kwenda kutoa fedha zao.

Kuna watu walipiga au kutengeneza barabara za hovyo hovyo, lakini kelele hazikupigwa , au mahakama ziliachia watu Ktk misingi ya ajabu ajabu lakini kelele hazi kupigwa, sasa kelele zinapigwa Leo , kulikoni.
 
Kuna watu walipiga au kutengeneza barabara za hovyo hovyo, lakini kelele hazikupigwa , au mahakama ziliachia watu Ktk misingi ya ajabu ajabu lakini kelele hazi kupigwa, sasa kelele zinapigwa Leo , kulikoni.
Labda kuna laana!

Unajua uongozi wowote hata wa familia kama kuna damu imemwagika basi ni shida tupu
 
Mimi sina shaka kabisa na matamko ya viongozi iwe ni wa polisi au mikoa au wilaya.
Sina shaka kabisa kabisa!!

Wasiwasi wangu unatokana na Nchi hii na nyinginezo kushindwa kuwa na sheria ya wazi ya Viongozi wa umma kuweka wazi Mali zao ili jamii kabla ya kuhukumu wenzao jamii ione uadilifu wao usio na shaka kabisa.

Wengi tuliona kuwa bila kuwa na sheria ya wazi kabisa chini ya tume ya Maadili ya sio tu viongozi wa umma lakini kwa wafanyakazi ,wafanyabiashara , na kila mtanzania ajulikane anamiliki nini na wapi basi kuna makundi yatapiga kazi kubwa ya kula rushwa kubwa kubwa toka kwa wafanyabiashara wanaowajua kuwa huwa ni wacheza madili.

Hii inajulikana kuwa rushwa ina mtandao mpana unaoshirikisha wale wanaoweza kuvuruga biashara za watu.

Rushwa itapungua au kuisha siku ambapo uwazi kamili wa Mali za viongozi utakapowekwa wazi kwa kila MTU kuhoji na kuzitaja kwa wazi.

Kule Mongolia miaka ya 2000 tulisikia msimamizi wa idara Fulani ya uhujumu uchumi na makosa mbalimbali alikua ni bilionea ,kutokana na kushirikiana na wauza madawa wakubwa, wauza magendo na rushwa toka kwa walioko chini yake na idara na ngazi alizopitia alishiriki vitendo vya rushwa na kuhonga mpaka kupata madaraka makubwa na alipostaafu akakimbilia kwenye siasa na kuwa mwakilishi wa wanachi wa Eneo alilokua anatokea kutokana na umaskini wa watu na yeye kuonekana kuwa mkombozi wao kwa kuwahonga mapesa kwenye uchaguzi.
Mfano wa huto mmongolia unanipa mashaka sana hata huku Afriaka huenda kuna watu wanatumia udhaifu wa sheria ya maadili kuwa kama Bunge la gizani kuficha udhaifu wao. Mbele ya jamii wakajipambanua kama wapambanaji.

Kama alivyo Mkuu wa nchi tunamuona akipambana na kuonekana kukosa usingizi kwa kuwatafuta majizi na mafisadi.
Ni vema na tume ya maadili nayo ikawa na wapambanaji kama alivyo Rais kwa kutoka maofisini ili kuwabaini viongozi wasio na Historia ya uadilifu au wanaojificha na kuficha Mali zao lakini jamii inawajua.

Tume ikisubiri waje kujaza form wenyewe ofisini itakua inasubiri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi mimi ni mpenzi wa mpira wa miguu.
Unajua kawaida ukiona unaanza kuchezewa rafu unanyoosha mikono juu ili refa aone mapema.
Kwenye mpira ukijifanya tafu sana unaweza kuvunjwa na refa asitoe kadi!

Mimi nimeona hii game imeanza na rafu dakika za mwanzo tu!
1.Kwanza RC Mwanza alishaihukumu
2.Kisha mheshimiwa rais akaelezea 'mchezo ulivyokuwa' na kumuelekeza waziri kwamba hiyo dhahabu inaweza kutuongezea fedha za kigeni.
3.Leo CP. Boaz amegongea msumari mwingine kwenye jeneza wakati kesi imeshatajwa.

Nadhani wakili wa hawa watuhumiwa anapaswa kuraise his concerns mapema mahakamani!
Tena kwavile mheshimiwa rais alimwambia jaji mkuu kwamba 'anampa fedha anayoomba halafu aone serikali ikishindwa kesi mahakamani!' na ukiangalia mwenendo wa issue yenyewe mpaka sasa unapata wasiwasi kuwa kinachoendelea mahakamani ni formality tu!
Game ilishaisha.


Sent using Jamii Forums mobile app
Je unadhani kuwa hao watuhumiwa wamebambikiwa kesi?
 
NAWAONA KWA MBAAALI WATUHUMIWA WAKIWA HURU.
Wasipotoshe jamii,hakuna wizi hapo ni Mali halali za watu.,Nijuavyo process ya Gold,malipo serikalini hatua za awali. Hiyo ni Mali halali ya master dealer.

Hao wadau wadogo wanazo risiti nyingi za malipo serikalini kupitia Dilution plants, zinazowekwa seal muda wote na team madini na usalama mkoa husika, kisha hatua ya kupakua mzigo,wahusika wote wapo,mzigo hupimwa,malipo kodi, Mrahaba hulipwa, kisha wadau wa kati wengi kupeleka mzigo kwa master dealer,na mara nyingi biashara hiyo inakua na malipo ya awali toka juu mpaka chini. Hayo madai ya rushwa sina hakika nayo!
 
You couldn't be more right
Wasipotoshe jamii,hakuna wizi hapo ni Mali halali za watu.,Nijuavyo process ya Gold,malipo serikalini hatua za awali. Hiyo ni Mali halali ya master dealer.

Hao wadau wadogo wanazo risiti nyingi za malipo serikalini kupitia Dilution plants, zinazowekwa seal muda wote na team madini na usalama mkoa husika, kisha hatua ya kupakua mzigo,wahusika wote wapo,mzigo hupimwa,malipo kodi, Mrahaba hulipwa, kisha wadau wa kati wengi kupeleka mzigo kwa master dealer,na mara nyingi biashara hiyo inakua na malipo ya awali toka juu mpaka chini. Hayo madai ya rushwa sina hakika nayo!
 
Paul Alex wewe una maslahi gani na hii kesi, ni vyema chini ya kila andiko lako uwe unaweka uhusiano wako na watuhumiwa. Hakuna kesi yoyote ambayo Polisi wataipeleka mahakamani huku waliofanikisha kazi hiyo kutopongezwa. Kazi ya mahakamani si ya Polisi tena bali DPP na wanasheria wake.

Jambazi akikamatwa Polisi watasifiwa hata kabla jambazi hajahukumiwa na mahakama, tofauti ni nini na hii kesi ?
 
Labda kuna laana! Unajua uongozi wowote hata wa familia kama kuna damu imemwagika basis nishida tupu
Hamna Cha laana wala kitu Kinacho karibiana Na hicho, na hata katika tawala zilizo pita kuna matukio ya damu kumwagika lakini maisha yaliendelea bila kelele.
Mwanzo wa utawala wa Mkapa napo palitokea ajali ajali , watu walianza kusema mambo Kama haya ya laana
 
Wasipotoshe jamii,hakuna wizi hapo ni Mali halali za watu.,Nijuavyo process ya Gold,malipo serikalini hatua za awali. Hiyo ni Mali halali ya master dealer.

Hao wadau wadogo wanazo risiti nyingi za malipo serikalini kupitia Dilution plants, zinazowekwa seal muda wote na team madini na usalama mkoa husika, kisha hatua ya kupakua mzigo,wahusika wote wapo,mzigo hupimwa,malipo kodi, Mrahaba hulipwa, kisha wadau wa kati wengi kupeleka mzigo kwa master dealer,na mara nyingi biashara hiyo inakua na malipo ya awali toka juu mpaka chini. Hayo madai ya rushwa sina hakika nayo!
Sasa huyu master dealer Hana storage area ambayo inajulikana Na serikali. ?
Na siku anataka kusafirisha nje ya nchi serikali inakuwa haijui??? Au hatoi taarifa. Kwa Maneno mengine serikali haijui wala hawatakiwa kujua kwamba master dealer Fulani Mwezi huu amenunua dhahabu ya kiasi fulani Na akiuza nje master dealer Fulani ameuza nje kiasi Fulani Na fedha ya kigeni au madafu imepatikana Na kodi zimelipwa
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom