Muelekeo wa Uongozi ndani ya nchi na siri ya viongozi wa chama tawala

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Mwana jamvi,

Utakubaliana nami au kuungana nami au unikosoe kuwa sasa imedhihirika kuwa ajenda ya sasa inaonyesha dira na muelekeo wa aina ya uongozi na siri waliyo nayo juu ya madaraka.

Utakubaliana na mimi kwamba sasa CCM wameanzisha mfumo wa kuhakikisha wao wakimaliza muda wao wanaweza wakahakikisha wanao wanashika nafasi za juu bila ya kujali kuwa nchi sio ya ukoo, vizazi vyao tu na haiwezi kuchukuliwa kama vile ya familia au ya aina fulani ya watu waliopitia uongozi ndio wanao watakuwa viongozi wa baadaye.

Mfano Ridhiwani Kikwete, Mtoto wa Mwinyi, Mtoto wa Lowassa, Mtoto wa Marehemu Sitta na wengine wengi ni vijana wanaoandaliwa kuhakikisha nao wanapita mikondo ya wazazi wao, wote hawa wamo tayari kwenye kinyang’anyiro cha kofia ya ubunge ili wasonge mbele.

Je, hili ni fundisho kwetu kuwa na sisi wengine tufuate nyayo, tupambane ili watoto wetu wawe miongoni mwa viongozi?

Mnafikiri kwanini Mke wa Rais mstaafu ana ng’angania kuwa Mbunge, ina maana hatosheki na madaraka aliyowahi kuwa nayo pindi mumewe akiwa Rais. Muangalieni sana anaweza akagombea kuwa Rais wa kwanza mwanamke ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Siri kubwa ya kufanya hili laweza kuwa, kukamisiana ili kuendeleza tamaduni ya kutunza siri ya yale Baba zao waliyafanya na kuziba ili kuhakikisha Familia inatajirika zaidi na kuficha maovu yaliyofanywa na wazazi wakiwa madarakani.

Niishie hapa kwa leo.
 
Back
Top Bottom