texaz mc
JF-Expert Member
- Jan 15, 2016
- 371
- 203
Habari wadau wote wa elimu.
Swala langu ni kuhusu hii kozi ya AIRCRAFT ENGINEERING inaonekana itakua na soko kubwa mpk kufikia 2025-2030. Huu mtazamo wangu ni kutokana na haya yafuatayo;
1. Leo kwenye hotuba ya Rais ameainisha kwamba kwenye hii kozi mwaka huu imetoa wahitimu 16 tu. Hivyo inaonekana watu hawajaijua au hawajajikita kuisomea wakiamini kwa Tanzania itakua ngumu kupata kazi zake.
2. Mimi naamini hao wahitimu 16 woote watapata ajira kwenye sekta hiyo kutokana na kutokuwepo kwa upinzani kwenye kozi hii.
3. Kuwepo na chuo kimoja tu kinachotoa kozi hii ambacho ni NIT hivyo kupelekea kudahili wanafunzi wachache tofauti na kozi zingine kama comp eng ambayo inapatikana vyu vingi kama MUST, DIT n.k.
4. Ugumu wa kozi hii ambapo watu wengi hudhani kuwa ni mojawapo ya kozi ngumu sana.
5. Kununuliwa kwa ndege nyingi kwa miaka ijayo.
6. Pia mh. Rais amesema, kutokana na ndege hizo kuhitaji maintanance kila baada ya miezi kadhaa hivyo serikali itahitaji kutumia kiasi kikubwa cha fedha takribni dola million 3 kuzipeleka nje ya nchi kutokana na UPUNGUFU WA WATAALAMU KATIKA FANI HII.
Hivyo hapa ameahidi kukiboresha chuo cha NIT kimiundombinu na kuwapatia ndege ndogo kwa ajili ya mafunzo ya vitendo(KWA SABABU WATAANZISHA KOZI YA URUBANI MIAKA IJAYO)
Mimi nimeona hivyo kwa mtazamo wangu, karibuni wadau wote wa elimu tulijadili hili.