Mudhihir M. Mudhihir Awataka Akina Zitto Waachane Na Siasa Za Matukio

JINOME

JF-Expert Member
May 29, 2017
958
1,424
MUDHIHIR M MUDHIHIR

Linapojiri tukio lenye kuumiza nyoyo na kuhuzunisha nafsi, wanadamu waungwana hutarajiwa waingiwe na simanzi na huruma ya kuwafariji wenzao waliyoathiriwa na madhara ya tukio husika. Kufurahia mikasa inayowafika wenzako ili ugugumie damu yao, ung’wafue minofu yao na ugugune mifupa yao ni hulka ya fisi kwa mizoga. Huu ni ufisi ndani ya ubinadamu. Ni hulka ambayo haipendezi na haikubaliki hata kidogo.

Unaweza usipate tabu sana iwapo utamuona mtu anafurahia dhiki ya hasimu wake chambilecho waswahili, adui yako muombee njaa. Lakini inashangaza na kustusha sana unapomuona mwanasiasa ambaye dhima yake kubwa ni kupigania ustawi wa nchi yake na watu wake, ati naye anafurahia tukio linaloleta dhiki kwa raia wenzake. Wanasiasa wa aina hii ambao matukio kwao huwa ni mtaji wa kisiasa ni wa kupuuzwa.

Umashuhuri na umaarufu ni dhana mbili zinazokurubiana lakini zenye mpaka baina yao. Umashuhuri unahitaji kunena na kutenda yenye murua na manufaa. Lakini umaarufu unaweza kupatikana kwa kusema na kutenda lolote lijalo kichwani. Mtu hujisemea tu bila ya kuchuja karaha na furaha, na akiongea hakumbuki kuweka akiba ya maneno. Ndiyo sababu hata wehu na watu waovu huweza pia kuwa watu maarufu. Umashuhuri ni hadhi yenye kutukuka.

Chini ya jua la Mwenyezi Mungu watu mashuhuri wakivurugwa na tumbo hutafuta stara wakajistiri, na wakivurugwa kichwani ndimi zao huzungumza na nyoyo zao kwanza. Mambo huwaje kwa watu maarufu? Masalale! Wakivurugwa na tumbo hawachagui mahali pa kufusa, na wakivurugwa kichwani ndimi huboboja maneno yasiyo na kichwa wala miguu. Japo kupata umaarufu ni zoezi rahisi na jepesi, mbele ya watu wenye mazingatio gharama yake ni kubwa mno.

Wapo wanaopendezwa kuitwa wanasiasa machachari. Aghalabu hawa ni wale wanaostahabu umaarufu kuliko umashuhuri. Wanajitahidi kuondosha rihi ya uvundo uliyomo ndani yao na ndani ya vyama vyao kwa kupulizia manukato. Hawatambui masikini kuwa ukiupamba uchafu unalichafua pambo. Hawa ndiyo wanaodandia kila tukio ndani ya jamii na kuligeuza kuwa mtaji wa kisiasa. Ni wanasiasa na wanasihasa mumo humo.

Katika msimu huu wa soko la korosho unaotarajiwa kukamilika mwezi Machi, kumejitokeza tatizo kubwa la kuyumba kwa bei ya zao hili. Ni tukio ambalo halikusalimika kudandiwa na wanasiasa na kuligeuza kuwa mtaji wa kisiasa. Walihoji uhalali wa serikali kufanya biashara. Walihoji uhalali wa serikali kutumia fedha nje ya bajeti. Walihoji uwezo wa serikali kusomba korosho kutoka kwa wakulima hadi maghala makuu.

Wanasiasa machachari sasa wamebaini kuwa yale waliyokuwa wameyashikia mabango kwamba serikali itafeli, kwa kiasi kikubwa serikali imefuzu. Mabingwa wetu hawa wa siasa sasa wameibuka na agenda ya kuporomoka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola. Wanadai kuwa laiti serikali isingeingilia kati sakata la soko la korosho, korosho zote muda huu zingekuwa zimeshauzwa nje ya nchi na kuingiza fedha za kigeni na bila ya shaka shilingi yetu isingeporomoka.

Hatuwezi kufanya tathimini ikawa ni yenye manufaa kwa kuangalia matokeo ya tukio peke yake bila kwanza kukitazama kwa kina kiini cha tukio lenyewe. Rais Magufuli hakufikia uamuzi wa serikali kununua korosho kutoka kwa wakulima kwa sababu ya ubabe au chuki dhidi ya wanunuzi binafsi wa korosho. Dhamira ya msingi ilikuwa ni ya kumnasua mkulima ili aweze kurejesha gharama za uzalishaji na kupata faida kidogo.

Husemwa kuwa mbweha akiingia ndani ya ua wa nyumba yako mdhibiti yeye kwanza kwa kumtoa mbio, ndipo uanze kuwarejesha kuku wako tunduni. Hii ndiyo ilikuwa busara ya Rais Magufuli na serikali yake. Kuwaondosha kwanza waliyotaka kuwalalia wakulima kwa kuzinunua korosho zote. Wengi wetu tuliwatarajia wanasiasa machachari waiunge mkono hatua hii na washauri namna bora ya utekelezaji wake.

Hayupo abishaye kuwa zoezi hili limeleta usumbufu kwa wakulima kwa kucheleweshwa kuuza na kupokea malipo ya korosho zao. Usumbufu huu umetokana na ukweli kwamba zoezi zima lilitokana na udharula, na dharula ni ghafla ambayo siku zote haina kinaume. Kuimiliki ghafla kunamhitaji jasiri mwerevu amkate jongoo kwa meno japo huleta kichefuchefu, na nyakati nyingine mtu hulazimika kukata pua ili aunge wajihi.
Wanaomlaumu Rais Magufuli na serikali yake kwa hatua hii ya kuwanasua wakulima walipenda kifanyike nini? Au walitaka wakulima wabaki na korosho zao majumbani au walipendezwa wafanyabiashara wajinafasi kununua korosho kwa bei ya kuwakamua wakulima jasho na ngama? Ni nani mpenzi na mtetezi wa wakulima kati ya Rais Magufuli na wanasiasa machachari?

Mwenye kutwanga mpunga kinuni hupata mchele safi, chenga, chuya na makapi. Na katika zoezi letu hili la kuwakwamua wakulima wa korosho tumepata manufaa si haba, tumekutana na matatizo na changamoto kadhaa, na tumepata fursa na sababu za ku ichambua tasnia ya korosho ili tuweze kuchukua hatua mujarabu za muda mfupi, muda wa kati na za muda mrefu. Kwa kawaida, matatizo huwa shida kwa zoba lakini kwa mwerevu shida ni fursa na hamasa ya kusonga mbele.

Wanasiasa machachari kwa nini hamjiulizi hawa wanaoshobokea kuuza korosho zetu ghafi nje ya nchi yetu ni akina nani na agenda zao ni zipi! Na kwa nini hamjiulizi mazimwi yanayozuia ubanguaji wa korosho zetu hapa nyumbani ni kabila gani! Basi ikiwa kabila yao ni majini au vibwengo tusiendelee kuwapunga kwa chano cha shira, halua na maziwa. Rada ya mapepo ni kukemewa hadi yalegee na kushindwa.

Wanasiasa machachari hamna budi kutambua kuwa vita tunayopambana ndani ya medani ya korosho ina maadui wenye nguvu na ushawishi mkubwa ndani na nje ya mipaka yetu. Huko nje ya nchi wapo wafanyabiashara wanaozoa na kujikusanyia faida kemkem. Wapo wenye viwanda wanaozitia korosho ghafi thamani na kujizolea mapesa ya kigeni. Huko nje korosho zetu ghafi zinamwaga ajira na kuingiza kodi na ushuru.

Kwa muktadha na mnasaba huu wa mpambano wetu dhidi ya wapinzani wetu katika tasnia ya korosho huko nje ya mipaka yetu, tusitaraji kuwa dhamira yetu ya kubangua korosho zetu hapa nchini itatekelezeka bila ya upinzani wenye nguvu na vitimbwi. Wanasiasa wetu chonde msiingiwe na mapepo na kuwa abiria katika mtumbwi wa vibwengo halafu zumari likipulizwa baharini mnahemkwa wa nchi kavu.

Na humu nchini mwetu wamo makuwadi wa soko la korosho daraja kwa daraja. Wapo wa daraja la kwanza wanaochuruza mafuta mwilini wakiwa ndani ya viyoyozi maofisini mwao. Wapo manyapara wanaowasimamia kangomba na chomachoma kuwabamiza wakulima. Mlolongo ni mrefu. Na hawa pia hawataki kusikia habari ya Tanzania kubangua korosho. Ikiwa wanasiasa machachari mna nia njema kwa nchi yenu na watu wake, acheni kuligeuza tatizo la soko la korosho kuwa mtaji wa kisiasa.

Mwanasiasa wa Tanzania akiandika mtandaoni kwa lugha yenye stihizai tele juu ya kampuni ya Kenya iliyotiliana saini na serikali kununua korosho, hivyo kutoka ndani ya pachipachi za nafsi yake anatupa ujumbe gani Watanzania wenzake? Anaicheka serikali katika juhudi yake ya kuuza korosho ilizozinunua kwa wakulima ili kuwanusuru na hasara ambayo ingewahasiri? Anayestahili kuchekwa naye anapocheka huchekesha sana.

Mwanasiasa wa Tanzania anapolishupalia suala la kuporomoka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola kwa sababu ya korosho zetu kutonunuliwa huko nje, hivyo kutoka ndani ya nafsi yake anadhani na kuamini kuwa hiyo ndiyo namna iliyo bora katika kuleta suluhisho la tatizo la soko la korosho zetu? Huu ndiyo ule umaarufu usiyo na chembe ya umashuhuri.
Ukimuona mwanasiasa ana udhaifu wa kudandia matukio na kuyageuza kuwa mtaji wake wa kisiasa, basi fahamu kuwa huyo ameishiwa nguvu za kufikiri na kapoteza mwelekeo. Huyo anakwenda arijojo. Basi usihangaike ukimsikia anaghani mistari ya Air Tanzania, Reli ya Kati, Stigler’s Gauge, madaraja ya juu ya Tazara na Ubungo na sasa Mzee Lowassa. Kumbe tulitaraji wafunue vinywa ili watueleze nini?

Mimi nadhani na nashawishika kuamini kuwa siasa za vyama vingi nchini mwetu zitakuwa na agenda zenye mashiko na mwelekeo wenye tija, iwapo tutaanza na kuweka sawa taratibu na kanuni muhimu ndani ya vyama vyetu. Tunahitaji agenda na mwelekeo, siyo siasa za kudandia matukio.

Tuacheni siasa za matukio | Gazeti la Rai
 
Mimi nadhani na nashawishika kuamini kuwa siasa za vyama vingi nchini mwetu zitakuwa na agenda zenye mashiko na mwelekeo wenye tija, iwapo tutaanza na kuweka sawa taratibu na kanuni muhimu ndani ya vyama vyetu. Tunahitaji agenda na mwelekeo, siyo siasa za kudandia matukio
Rubbish!
 
Maudhui yanaonesha muelekeo
Ametumia lugha ya kiswahili vizuri sana,its time now asiingie huko anako elekea na abadilishe mwelekeo kwenda kwenye ukuzwaji wa matumizi ya lugha ya kiswahili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakuwa teuzi sasa zinapatikana kwa kusifia upumbavu nahuyu MTU njaa imeanza kumyoosha inabidi arudi kwa namna hii akumbukwe pumbaf haonei huruma chinga wenzie wanavyokufa njaa kwa maamuzi yakipuuzi

ujinga mtupu, anakwambia zoezi la ununuzi wa korosho limefanikiwa sana kuliko kufeli.

jamaa kadata ama anatafuta teuzi, maana alicho fanya ni kusifia mwanzo mwisho kana kwamba sie hatupati/hatukupata kujua kinacho jili kwenye korosho.

Kashindwa kutwambia kwa nini shilingi imeshuka kaishia kulaumu wanasiasa kusema shilingi imeshuka kwa sababu ya korosho.

zaidi ya matumizi fasaha ya kiswahili hakuna la maana.hoja zake ni za kibwege (ananyemelea teuzi)
 
Back
Top Bottom