Muda wowote inawezekana nikawekwa rumande

Shindu Namwaka

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
4,911
3,082
Wakuu nitawajuza baadae kama nitaimaliza siku salama bila kutiwa mikononi mwa police kwani habari ni ndefu kidogo
Ila kwa kifupi kuna mtu nimezinguana nae kibiashara loading...

Update...

Kuna mtu nilikuwa nashirikiana nae kibiashara, kwa kifupi yeye anataka pesa yake na mimi kuna sehemu nimepeleka biashara hesabu tumeshafunga bado tu kugawana kila mtu awe na chake.

Nimemumbia nikamuingizie kiasi Fulani benki likilipwa deni tumalize yeye anasema amechoka kusubiri.
 
Kuna mtu nilikua nashirikiana nae kibiashara kwa kifupi yeye anataka pesa yake na mimi kuna sehemu nimepeleka biashara hesabu tumeshafunga bado tu kugawana kila mtu awe na chake

nimemumbia nikamuingizie kiasi Fulani benk likilipwa deni tumalize yeye anasema amechoka kusubiri.

Kumbe unamyeyusha haki yake...aisee jitahidi kumlipa kwani kunyea debe si mchezo! na ukizubaa utaolewa huko.
 
kwaio hapo unatetemeka mpaka unashindwa kusimulia mkasa vizuri? tulia mwanaume,,, ni swala la muda tu mambo yatakaa sawa kama kweli ishu iko kama ulivosema. ila kama umezulumu endelea tu kutetemeka mpaka nyama zidondoke maana hakuna namna.
 
Huna kesi hapo maadamu hujakataa kumlipa. Kuna watu wanadai sivyo lkn uchune tu kwa kuhamia mtaa mwingine na huko kabadiri jina,unaweza kujiita hata Shilole ili asikupate kiurahisi maana Hamna namna tena.
 
Utakamatwa utafikishwa polisi, utaandikisha kwa maandishi ni lini utampa mana hujakataa kumlipa kama msg zipo zisave zikakusaidie polisi, muhimu ukichukuliwa na polisi toa ushirikiano usianze ubishi na ubabe, na acha kuwa na woga polisi ni rafiki wa raia wema, kama wewe jambazi utaogopa kama raia mwema wanaenda kuwapatanisha ili mmmoja apate haki yake. acha woga na dawa ya deni kulipa.
 
Utakamatwa utafikishwa polisi, utaandikisha kwa maandishi ni lini utampa mana hujakataa kumlipa kama msg zipo zisave zikakusaidie polisi, muhimu ukichukuliwa na polisi toa ushirikiano usianze ubishi na ubabe, na acha kuwa na woga polisi ni rafiki wa raia wema, kama wewe jambazi utaogopa kama raia mwema wanaenda kuwapatanisha ili mmmoja apate haki yake. acha woga na dawa ya deni kulipa.
Meseji sina nawasiliana na simu na akinipigia nakwenda kuongea nae live ila napata kauli zenye msisitizo ataniweka ndani
 
Jipe moyo mambo kama haya hutokea kama unavyodai kuwa Pesa iko mbioni kupatikana lakini mwenzio kashindwa kuwa mvumilivu inaonesha kapigwa danadana muda mrefu. Vinginevyo kukusonteka ndani inaweza isiwe busara badala yake makubaliano na kuahidi mbele ya polisi itakuwa in busara.
 
akikupeleka rumande halafu akafungua kesi unaweza kumkomoa utalipa kidogo kidogo kwa muda fulani .. ila ni dhambi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom