Muda wote nilikuwa najibana ili anione wa maana kumbe bure kabisa

ngonyango

JF-Expert Member
Aug 7, 2017
1,883
1,599
Jana nilikuwa mahali huku mkoani naangalia mechi ya Simba na Alliance....nikaagiza KVant na Coca cola nikamuomba Mhudumu aniletee pia limao iliyokatwa katwa na barafu ili kitu yangu ishuke kiulaini.

Ofcourse Mhudumu alitoa macho akaguna nafikiri alishangaa mambo ya barafu na limao yanatoka wapi mimi nimamkazia macho akaondoka na kurudi baada ya muda kidogo akiwa na barafu na limao. Baada ya muda kidogo meza ya jirani akaja mdada mmoja yuko decent na anaonekana yuko vizuri akakaa. Mimi nikajipanga nimtokee nikishalewa lakini nikajistukia asije akaiona ile KVant halafu akaniona wa hovyo(jinsi alivyo nilijistukia) nikailaza kiaina ili asiione.

Wakati huo huo akamwita Mhudumu na kumtuma kinywaji(sikusikia,nilikuwa bize na mpira) baada ya muda kidogo nakuja kustuka kumwangalia yule Dada, alikuwa na bapa la Konyagi na alikuwa anagonga kavu kavu nikafikicha macho nikifikiri nimelewa au sioni vizuri nikamtolea macho ni kweli alikuwa anagonga bapa kavu kavu. nikachoka kabisa.

Muda wote nilikuwa najibana ili anione wa maana kumbe bure kabisa asa hii wadau si ni dharau kabisa? manake mpaka mpira unakwisha alishamaliza bapa na kutimua sikumsemesha tena!.

Au ndiyo uwanamme wa Dar huu?
 
Back
Top Bottom