Muda wa wabunge uwe vipindi viwili tu

Boney E.M.

JF-Expert Member
Jan 22, 2007
425
35
Ninapendekeza katika Katiba mpya suala la Mbunge kuwa kwenye uongozi kwa vipindi zaidi ya viwili lisipewe nafasi. Mbunge ahudumie wananchi wake kwa vipindi viwili tu vya miaka mitano mitano. Na akishakuwa mbunge kwa vipindi hivyo haruhusiwi tena kugombea. Hili ni kwasababu wengi wameonyesha kuwa wanakalia uzoefu hakuna la maana wanalowawezesha wananchi. Wengine nao wapewe nafasi ya Ubunge.
 
ushauri mzuri mana ilifika kipindi mzee kingunge alikua anatafuniwa nyama ndo anapewa ameze ila bungeni yuumo,
 
Hii itakuwa nzuri ili kutoa nafasi kwa vijna waweze kukewa nafasi nao waoneshe maarifa na umahili wao kwenye uongozi
 
Kama sheria za nchi hii zinatungiwa kwenye JF then hili linawezekana. Shida ni moja tu, wanaotunga sheria nchi hii ni wabunge. Unadhani watatunga sheria isiyo na maslahi kwao?
 
ni mawazo mazuri lakini je mna mfano wowote duniani wa kutufanya tushawishika na hili? tutofautishe mbunge na rais ni watu wabe tofauti kabisa ukija katika suala la awamu za kuongoza nchi!
 
Naunga mkono kwa kigezo kuwa watanzania wenye uwezo wa kuongoza wamekuwa wengi na wote ni vyema wakapewa uwezo wa kutoa mchango kwa taifa lao. Kama mtu ataruhusiwa kugombea bila kikomo hata kama ni mzuri kiasi gani atakuwa anazibia wengine fursa ya kutimiza haki yao ya kuongoza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom