Muda wa Urais ni Miaka kumi, ikitokea akazidisha mtafanyaje wananchi

Usipopiga kura maana yake ni kumchagua usiyemtaka. Pigs tu hata zikiibiwa unakuwa ujumbe umewafikia kuwa hawapendwi, na kuwa iko siku zitawapinga nyingi hadi washindwe kuiba ka ma Jirani hapo DRC amelazimika kumpa mpinzani ambaye hakushinda maana chama tawala kimeshindwa kuziiba hadi Tshisekedi kapewa ushindi Wa Fayulu. Hapo imekuwa nafuu , lakini unasusia kura halafu unasema bararbarani eti Mimi sikupiga, ujue hata hivyo ulishindwa kumwambia kuwa unatwala lakini kura yangu hukuipata, huo ndio kujitambua . Hapana kususia kupiga unakuwa umetenda dhambi mbaya ya kutoweka wazi dhamira (conscience ) yako. JITAMBUE

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha wanasahau ule msemo kwamba ukisusa wenzako wanakula.
 
Naliwaona Watu wakipigwa 'na mijeledi 'na kung'atwa na nyoka hadi miaka iyoo kadri ya umri wa kukaa duniani
 
Naliwaona Watu wakipigwa 'na mijeledi 'na kung'atwa na nyoka hadi miaka iyoo kadri ya umri wa kukaa duniani
Hahaha yapo yaliyopangwa yatokee ili kutimiza maandiko, hata yeye alisema hakuja kuibadiri torati bali kuitimiza. Na yatokeayo yawezekana yalipangwa yatokee.
Hata kifo chake kiliandikwa lakini wapo waliopinga na kuumizwa kwa kifo kile, ila walio fahamu walishangilia na kusema yametimia.
 
Je hili la kuongeza muda baada ya miaka kumi kuisha bado wapo wanosema HAIWEZEKANI? na ikiwa LITAWEZEKANA wao watafanya nini? au tutalialia humu basi tunazoea siku zinaenda.
wadau karibuni tujadiri.
acha kuchachawa wewe,Tunamsubiri Rais wetu lissu kasema atayaruhusu mashoga
 
Nyerere alitawala tangu 1961 mpaka 1985, sijui ni kwanini ilikuwa hivyo. Ila marais waliofuatia wamekuwa na utaratibu wao wa kukaa miaka 10 kila mmoja. Kunadhana kwamba hiwezekani akazidisha muda, eti katiba inamkataza, sawa. lakini ikitokea aka kaa zaidi ya miaka kumi kwa kisingizio chochote, mtafanya nini wananchi. Kua haijawahi kutokea Tanzania sio hoja hapa, kwasababu hata huko ilikotokea hawakuomba, bali mazingira yalitengenezwa na ikawa hivyo. Huwa wansema nitaondoka nikiona mambo yako sawa lakini hayo mambo hawayasemi.

Ikiwa hujaambukizwa ukimwi, huwa unasema mimi siwezi kuupata, haiwezekani. Lakini ukimwi huwa unapata wateja wapya kila siku na kila dakika, na hata wale waliowahi kusema mimi haiwezekani nao wamekumbwa na gharika hilo. Sasa assume inatokea kwetu Tanzania Magufuli naongeza muda, anasema aliyoyapanga kuyafanya hayajaisha ataondoka atakapo jiridhisha yeye kwamba yamefanyika.

Kabla hajazuia Bunge live ilianza minong'ono na wapo wale waliosema HAIWEZEKANI, na hata kabla hajazuia mikutano ya siasa wapo wale waliosema HIWEZEKANI mengine mengi walisema hayawezekani lakini yamewezekana na kila mtu yuko kimyaaaaa. Sasa kuna muswaada wa vyama vya siasa, ilianza minong'ono ,hadi sasa tunauona muswaada na watu wanapeleka maoni yao na maoni yanakusanywa kwa mtindo huohuo tusioufahamu lakini mambo yanakwenda na mwisho utapitishwa. Muswaada wa katiba mpya uliisha tupwa, kuna waliobisha wakasema imetumika pesa nyingi sana na muda HAIWEZEKANI tukauacha na haitawezekana, lakini sasa ni historia, na maisha yanasonga mbele.

Je hili la kuongeza muda baada ya miaka kumi kuisha bado wapo wanosema HAIWEZEKANI? na ikiwa LITAWEZEKANA wao watafanya nini? au tutalialia humu basi tunazoea siku zinaenda.
wadau karibuni tujadiri.
Kaiulize katiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeona ramani kwenye shule moja imeandikwa "Administrative period in Tz"
1964-1985- Ndg. JK Nyerere
1985-1995 -Ndg. Ali Hassan Mwinyi
1995 -2005 - Ndg. Benjamini Mkapa
2005 -2015- Ndg. JK Kikwete
2015- 2025 - Ndg. J. Magufuli.

!!!!!! Hii ndiyo zana ya kuwafundishia watoto wetu huko mashuleni. Je,ikitokea wamekuwa wakubwa na kupata uongozi kama nafasi ya Spika au waziri then wakichukia bunge kuitwa dhaifu wakati kweli ni dhaifu tutawalaumu?
Inategemea ni shule gani mwanao anasoma. Kama ni ya jumuiya ya wazazi wa ccm, ni sawa ulichoandika. Wao wanatumia ILANI na lazima itekelezwe. Kama anasoma IST inaweza kuwa tofauti. Ila hiyo sasa inazoeleka nchi nzima kwamba rais lazima akae vipindi viwili yani miaka kumi. Kwasababu haihawahi kutokea kukaa miaka 5, sasa hata inapokuwa inayaka kutokea inalazimishwa iwe tofauti.
 
Lissu I doubt kama baada upasuaji mwingi hivyo kwa risasi nyingi vile, ataweza mikiki mikikiya urais.? Halafu Afrika kuna nchi chache zenye kura halali na yetu kama imo katika hizo chache kama mfano Ghana. Mzee Kawawa aliwahi kusematulpoanzisha chama kimoja miaka ya 60's kuwa democrasia no anasa ya matajiri( a luxury of the rich.) Nasiktika kutamka tuandae mindset zetu kutawliwa na cham kimoja. Sasa ikiwa China na Russia matajiri vile hawajawa na mfumo bora Wa demokrsia , sembuse sisi wachovu Wa kila hali kiuchumi. Ni ukweli mchungu kuumeza . Mpaka inakatisha tamaa watu wazima kudanganyana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lisu anaweza kuwa anapenda, lakini usalama wake utakuwa mgumu hata kusimama jukwaani kuwasema hao. Na demokrasia sasa imeanza kuzoeleka kwamba 5x2 ni lazima. Wao wanataka tukubali hivyo, na hata inapokuwa sivyo kama ilivyotaka kuwa Zanzibar basi ilazimishwe.
Sasa sijui wananchi ndio wameshakubali au wanaendelea kulazimishwa kukubali kwamba hiyo ndiyo sahihi. Sasa hili la kuongeza muda likitokea kwa kigezo atimize aliyoyapanga, watapipinga au nalo watakubali.
 
Na kwa madhambi aliyofanya miaka hii mitatu hatotaka kuachia madaraka. Ila jumuiya ya kimataifa itakaposema hafai atatoka tu.
Nkrumah alibanwa kiuchumi akabakiwa na pound 60000 tu hazina, haikupita muda wananchi na wanajeshi walimchukia akapinduliwa.
Aisee!
 
Back
Top Bottom