Muda wa ukomo wa tume ya kuchunguza utekwaji wa dr. Ulimboka ni lini?

KOMBAJR

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
5,827
1,271
Heshima kwenu wanabodi katika miezi ya karibuni issue ya dr. Uli imetawala vichwani mwa watu wengi.pamoja na issue yenyewe ikigubikwa na sintofahamu kuanzia utekwaji,uundwaji wa tume na ushaidi wa tukio lenyewe.wote tunajua wananchi hawajafuraishwa na tume iliyoundwa na kova kwa misingi kuwa siyo huru coz baadhi ya wajumbe wa tume hiyo ni wahisiwa lakini kova amehamua kuweka pamba masikio.Maswali ambayo bado yanagonga vichwa wa walio wengi ni:
1. Tume ilikuwa na Adidu rejea(TOR)?
2. Muda wa Ukomo wa tume hiyo unaisha lini?
3. Issue ya utekaji wa ulimboka ipo mahakamani?
4. Wale wanaohusishwa na tukio wanapogundulika wanatangazwa?au tume wanaendelea na uchunguzi zaidi ili watoe majumuiosho?
5. Hayo matokeo yatakuwa ya tume na aliyeichagua au ya wananchi?
Mytake. Indepent Tume ya wananchi kupitia kwa Kubenea imeshamaliza kazi timely.tunasubiri ya kova
 
Walishasema Tume ya uchunguzi hufanywa polepole ili majibu yake yawe ya uhakika so endelea kusubiri tu pengine wanaweza kutoa majibu kabla hujafikisha umri wa miaka 55 ule wa kustaafu
 
tume siimekwishamaliza kazi yake! Kwani hujui mhusika mkuu wa utekaji wa Dr Ulimboka alikamatwa na tayari amefikishwa mahakamani. Na inasemekana hivi majuzi alifanya utambuzi wa wale alioshirikiana nao miongoni mwa maiti zilizookolewa baada ya kuzama kwa meli
 
Back
Top Bottom