Muda wa Mtumishi wa Umma kustahili kupanda cheo ni miaka 4 mfululizo au hata kama sio mfululizo?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,905
2,000
Hivi huu utaratibu wa miaka 4 ambao bila shaka ulianza awamu ya Magufuli (mwanzoni ilikuwa miaka 3), ni mtumishi kutakiwa kuwa amefanya kazi kwa miaka 4 mfululizo tangu apande cheo kwa mara ya mwisho au awe amefanya kazi kwa angalau muda wa miaka 4 bila kujali ni kwa miaka 4 mfululizo au sio mfululizo?

Msingi wa swali langu ni kutokana na ukweli kuwa kuna watumishi tangu wapenda cheo mara ya mwisho, inaweza kuwa ni miaka 5 6 au hata 7 iliyopita lakini ndani ya miaka hiyo 6 au 7, kuna kipindi mtumishi huyo alikuwa masomoni kwa mwaka mmoja, miwili au hata mitatu. Sasa nachojiuliza mtumishi huyo anastahili kupanda cheo?

Kwa mfano, mara ya mwisho kupanda cheo ilikuwa May mwaka 2015 na ilipofika Oktoba 2016, akaenda masomoni (full time) kwa miaka 2 kwa maana ya mpaka mwaka July 2018 alipomaliza masomo na kurejea kazini

Sasa mtumishi kama huyu ambae hana miaka 4 mfululizo kufikia mwaka huu wa 2021 lakini tayari ametumika cheo hicho kwa jumla ya miaka 4(including kipindi cha June 2015 mpaka Oktoba 2016 kabla hajaenda masomoni), anastahili kupandishwa cheo?

Ukisoma standing order ya 2009 kipegele cha mambo ya promotion, naona haiko wazi kuhusu hili, hivyo kwa wanaojua, hasa Maafisa Utumishi (kama wamo humu), tunawaomba watupe ufafanuzi.

Karibuni.
 
mlimilwa

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,412
2,000
Mimi ninavyojua mtu hata akiwa masomoni pia yupo kazini, pia inaweza kua ni vizuri zaidi maana anaongeza elimu hivyo hata akipandishwa cheo sio mbaya.

Isipokua waliowengi wanajisahau kua kumbe hata akiwa masomoni pia bado ni mfanyakazi. Anasahau hata kipindi cha likizo alitakiwa aludi kwenye kituo chake chakazi na aonekane kwenye kitabu cha mahudhulio.

Na hii ndio iliwaumiza sana watu hasa walimu kuitwa wafanyakazi hewa. mtu anaenda kusoma hadi miaka mitatu hajaonekana kwenye dafatari hivyo itaonekana mkurugenz analeta hesabu ya watu vivuli na kulipwa mishahara kwa watu wasiokuwepo.
 
Tatizo ni kukosekana/kutotolewa kwa mafunzo au semina za mara kwa mara sehemu za kazi na watumishi wenyewe kutokujisomea taratibu na sheria za kazi hivyo wanakuwa hawaelewi athari za mambo wanayoyafanya.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,062
2,000
Kwenda kusoma haikuondolei haki yako mradi huna likizo ya bila malipo, maana kipindi cha likizo bado unarudi na kufanya kazi na unasoma kwa manufaa ya taasisi na siyo yako pekee.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,062
2,000
Mimi ninavyojua mtu hata akiwa masomoni pia yupo kazini, pia inaweza kua ni vizuri zaidi maana anaongeza elimu hivyo hata akipandishwa cheo sio mbaya.

Isipokua waliowengi wanajisahau kua kumbe hata akiwa masomoni pia bado ni mfanyakazi. Anasahau hata kipindi cha likizo alitakiwa aludi kwenye kituo chake chakazi na aonekane kwenye kitabu cha mahudhulio.

Na hii ndio iliwaumiza sana watu hasa walimu kuitwa wafanyakazi hewa. mtu anaenda kusoma hadi miaka mitatu hajaonekana kwenye dafatari hivyo itaonekana mkurugenz analeta hesabu ya watu vivuli na kulipwa mishahara kwa watu wasiokuwepo.
Right
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,905
2,000
Kwenda kusoma haikuondolei haki yako mradi huna likizo ya bila malipo, maana kipindi cha likizo bado unarudi na kufanya kazi na unasoma kwa manufaa ya taasisi na siyo yako pekee.
Ule waraka/barua ya Katibu Mkuu Utumishi umeweka wazi makundi ya watumishi wasiostahili kupandishwa vyeo wakiwemo waliokuwa masomoni(full time) na huu ndio msingi wa swali langu kwenye hii mada.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,062
2,000
Ule waraka/barua ya Katibu Mkuu Utumishi umeweka wazi makundi ya watumishi wasiostahili kupandishwa vyeo wakiwemo waliokuwa masomo(full time) na huu ndio msingi wa swali langu kwenye hii mada.
Weka hapa mkuu tukusaidie, watumishi kibao wanatengewa budget wakiwa masomoni, nimefanya field serikalini pamoja na kujitolea kabla ya kuamua kukaa pembeni mkuu vitu vingi navielewa kdg
 
Said Stuard Shily

JF-Expert Member
Jul 18, 2017
1,709
2,000
HUYO AKAONGEZE TENA ELIMU KWANI HAWEZI PANDISHWA KWA SABABU YA UNJAUNJA WAKE HATAKI KUFANYA KAZI MFULULIZO
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom