Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimeongeza muda wa kuomba nafasi ya kugombea Uongozi wa Kitaifa hadi tar 30/08/2014 saa kumi alasiri.
Taarifa za awali za Chama ni kuwa mwisho wa kurudisha fomu ilikuwa tarehe 25/08/2014.
Muda huo umeongezwa kutokana na maombi mengi ya wanachama mikoani ambapo chaguzi bado zinaendelea.
Mkurugenzi wa Organizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda Benson Kigaila amesema mpaka sasa kwa majimbo ni 93% yaliyomaliza uchaguzi kwa tz nzima. Majimbo yaliyosalia ni 16 tu. Kauli ya Benson ameitoa leo akizungumza na Waandishi wa habari.
Kwa upande wa Mikoa ni 19 kati ya Mikoa 32 ya Kichama tayari imemaliza Uchaguzi. Kwa hali hiyo ni asilimia 59.4 % ya mikoa imemaliza mpaka jana jioni. Leo kuna mikoa 6 inafanya uchaguzi na ukikamilika itakuwa imebaki mikao 7. Mwisho wa uchaguzi wa mikoa ni tar 30/08/2014.
Wagombea wote wameaswa kufuata Kanuni za Uchaguzi pamoja na Mwongozo wa Chadema dhidi ya rushwa ambao umeambatanishwa kwenye fomu za maombi.
Naomba kuwasilisha.
Kibaja wa Msharabwe.