Muda wa kumuonesha trafiki leseni ni mpaka siku tatu kama umesimamishwa na huna

Akasome Kanuni tena the lastest ambayo imeweka mpaka torch tunazopigwa nazo barabarani. Sheria mama yenyewe imesema tu lazima uwe na leseni lakini kanuni imeenda zaidi ya hapo.
Ngoja nifuatilie namm kujua zaidi hapa nimepata msingi
 
Hizo sheria ni za kitabuni. Hapa Bongo polisi he is alyways right.

Halafu mahakama zetu ni analogue hazina muda wa kusikiliza kesi kwa haraka. Huna leseni ni faini. Iwe ni robo saa, siku nzima au mwaka.

Hapa nchini polisi ndio wanatafsiri sheria, ukienda mahakamani utatoa rushwa uliyokwepa kuitoa barabarani.

Tunashukuru kwa kutuonyesha sheria inasemaje, ila ujue kuna sheria na uhalisia.
Kuna kanuni mkuu!
 
Kuna kanuni mkuu!

Kanuni ni maneno tu ya kupamba. Kama unataka kupoteza muda jifanye kwenda mahakamani uone kitakachotokea. Kwenda kutafuta haki kwenye mahakama zetu ni kujitafutia matatizo zaidi, kesi ambayo haipaswi kuchukua hata nusu saa usishangae kuchukua miaka miwili ukaishia kupoteza muda wako. Mahakama zinaendeshwa kwa hila na sio weledi.
 
Kiuhalisia kama hauna leseni na umesimamishwa na askari lazima uwe mpole na msikivu lasivyo itakula kwako.
 
Sio lazima uende kwa huyo askari ni kama zamani tu anakuandikia notification unaenda kuonesha kituo chochote na usipofika ndani ya muda ndio unahesabiwa kosa na utapaswa kulipa

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu kuna baadhi ya vitu vingi huvijui katika kuchukuliwa lesseni, inaweza kuwa anachukua ili aangalie je gari unaloendesha linaendana na lesseni yako? pili je unataka kuandikiwa kosa je unaandikiwa na lesseni ipi? kwahiyo kwenda kuchukua lesseni si kuwa wakati wote ndo unakuwa salama,
 
Mimi nashauri sheria hii ifanyiwe marekebisho, ili iendane na wakati na uhalisia. 'Kupewa siku tatu kudhibitisha kuwa una leseni inafanya mazingira ya ya kazi ya traffic kuwa ngumu'. Pia hicho kipengere cha sheria kinachotoa siku tatu kina kinzana na kipengere kingine kinachohimiza dereva kuwa na leseni ya udereva wakati wote anapoendesha chombo cha moto!

Yangu ni hayo!
swadakta mkuu na ndo maana wanasheria wanajipigiaga tuu kwa vipengele kukinzana na mara zote kilamtu atataka kuvutia kwake kwa kile kipengele kimbebacho ila mwaisho wa siku kubeba lesseni ni muhimu sana maana hata ukiambiwa kapaki gari kituoni ukachukue lesseni ila jua wakati uliomba lesseni labda ulitaka andikiwa kosa so kwenda kuileta imekuchelewesha ilihali kosa liko pale pale
 
Akasome Kanuni tena the lastest ambayo imeweka mpaka torch tunazopigwa nazo barabarani. Sheria mama yenyewe imesema tu lazima uwe na leseni lakini kanuni imeenda zaidi ya hapo.
na huko kwenye kanuni ndo inasema lazima dereva awe na leseni wakati anaendesha
 
Na sisi wapanda treli la mwakyembe huu uzi unatuhusu au tuwe wapenzi watazamaji?
 
Kwa hali ya sasa, jitahidi utembee na leseni, maana yanayoweza kukukuta si madogo. Mpaka sharia ije ikuokoe, si leo.
Waulize walioenda kudai mafao yao baada ya Rais kutoa maelekezo kuwa utaratibu mpya usitishwe uendelee wa zamani. Wahusika wanasema hawana hayo maelekezo .
 
Uzi huu lazima niubebe niwatunishie kifua askari siku nikidakwa bila leseni

Sent using Jamii Forums mobile app
Beba uzi wako ukawatunishie misuli alafu utuletee majibu hapa ila kumbuka kujua kipengele kimoja cha sheria bado sio msaada muulize aliyeandika uzi huu sheria hazina mbadala "Exception "?

Unaweza kupewa muda wa kuwapelekea leseni ili uwathibitishie kuwa unayo lakini gari yako itakua chini ya uangalizi wao maana yake utapaki gari ndipo ukalete leseni.

Jiulize kama unaenda safari ndefu utafanya nini? Yeye hukutambua wewe kwa leseni sasa basi atakuacha uende ukamletee leseni akiwa amekuachia chombo Chako?

Kwanini usitembee na leseni yako kuepusha Shari? Sasa hivi kuna limiti ya makosa ndani ya muda fulani kwaiyo ikionekana umetimiza idadi hiyo ya makosa yatokanayo na uzembe wako na sio yatokanayo na ubovu wa chombo unaweza kufutiwa leseni.
Kuna form ya Onyo ambayo wengine tumewahi kuandikiwa na tukaachiwa lakini kuandikiwa mavitu hayo sio jambo zuri ni bora kufuata sheria lakini inapotokea umesahau tumia lugha ya kistaarabu ikishindikana basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si barabarani tu hata kwa makosa mengine yakawaida sheria INASEMA vingine na maaskari wananfanya vingine,Ki kawaida hata mtuhumiwa kufungwa Pingu ili hali hajakataa kwenda kituoni huko ni kwenda kinyume na sheria lakini sasa hivi Askari akija kukudaka lazima akutie PINGU..sheria iko wapi hapo?? si Hilo tu yapo mengi mno ambayo laiti sheria ingekua inafatwa hii nchi tungeishi kwa amani sana lakini ndo ivyo tena.

Nadhani uzi huu umetufungua macho ila bado hatuko salama kabisaaa..yani nawashauri wandugu LESENI beba tuuu HUNA pa kujitetea popote..Hata kama ukionekana umewashinda watakukomoa kwa kukupotezea MUDA wako ilimradi tu wakuonyeshe wao wanaweza zaidi yako...Ukiamua kubishana na hawa watu ktk jambo lolote bhasi hakikisha
1.Huna kazi yakufanya wakati huo
2.Muda si kitu kwako

Basi kama hivyo vitu unavijua basi anza kubishana nao MFWATE SHERIA hakika UTAWASHINDA NA HAWATOKUSAHAU lakini Tofauti na HAPO jiandae KUJUTA mpk na kupoteza gharama kibao kisa kusumbuana na hawa wanaojipangia Sheria.

TANZANIA bado sanaaa kuanza itumia Sheria.
 
Back
Top Bottom