Muda wa kumkumbuka John Okello

Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
2,125
3,130
Mganda kiongozi wa kikosi cha Mapinduzi ya Zanzibar. Wakati anampindua Mwarabu, Hayati Karume alikuwa Tanganyika amejificha. Okello aliongoza mapinduzi na akatangaza baraza la mapinduzi kisha akamtangaza Karume kama Rais wa Zanzibar.

Usiku wa Mapinduzi Karume hakuwepo Zanzibar wakati JOHN OKELLO akiongoza kikosi cha askari kuelekea Ikulu ya Mwarabu.

Historia ya Zanzibar imemsahau huyu shujaa.
 
Alifanya uvamizi siyo mapinduzi. Mapinduzi yanafanywa na raia wa nchi siyo wageni na bunduki wanazopewa na Nyerere.
 
Hayo maelezo ni kwa mujibu wa Okello mwenyewe lakini wanamapinduzi wengine wanapingana nae. Kwenye kitabu cha Abeid Karume kilichoandikwa Ali shaaban Juma, kinaeleza kuwa Okello alikuwa miongoni mwa kamati ya watu 14 iliyoundwa na Abeid Karume ili kutekeleza Mapinduzi. Karume alikuja Dar es salaam kesho yake baada ya mapinduzi kufanikiwa.

Ismail Jussa amekielezea hicho kitabu hapa,

Ismail Jussa akielezea kitabu cha Okello,

Ukisikiliza maelezo ya Okello kuhusu Mapinduzi, hakuna ubishi kuhusu ushiriki wake ila kuna chumvi nyingi ameongeza ikiwa pamoja na kujiweka kuwa kiongozi wa mapinduzi hayo.
 
tunavyojua sisi kiongozi wa mapinduzi ni john okelo na A A karume

basi
 
Back
Top Bottom