Muda wa kulipwa kwa madeni ya Watumishi wa Serikalini

Kuku kwiyoyo

Member
May 7, 2020
29
15
Habari zenu wanajamii

Naomba mnisaidie kitu kimoja. Mimi kwa bahati mbaya mama yangu mzazi alifariki tangu 2016 na alikuwa mtumishi wa Serikali. Amefariki akiwa anaidai Serikali malimbikizo ya mshahara.Sasa mimi nimeamua kufuatilia hayo madeni tangu mwezi wa pili pale ofisini kwake

Sasa kiukweli nawapa hongera wanafuatilia na mara ya mwisho walidai kwamba wameshaituma Wizarani, niliwatafuta kama wiki iliyopita wakisubiri wizara yenyewe ifanye kazi yake.

Sasa mimi natamani kujua kwamba ni muda gani ambao Wizara ya Fedha inachukua mpaka deni la marehemu kulipwa.

Naombemi msaada Kwa wenye uzoefu na haya masuala ya ulipwaji wa madeni. Labda ukishakamilisha masuala ya kujaza document za marehemu na ofisi wakaituma Wizarani je Wizara hutumia maximum muda gani mpaka kulipa hilo deni la marehemu.

Nawasilisha
 
habari zenu wanajamii...naomba mnisaidie kitu kimoja.. mimi kwa bahati mbaya mama yangu mzazi alifariki tangu 2016 na alikuw mtumishi wa serikali..amefariki akiwa anaidai serikali malimbikizo ya mshahara...
Mkuu hii nchi kama huna jina kubwa wewe andika maumivu tu, gharama za kufuatilia zinaweza kuwa kubwa mara 2 ya unachodai mkuu. Hakuna usawa kama haupo CCM.
 
Serikali ilipe madeni ya watumishi. Hela wanayo kama zawadi za gari zinapatikana iweje za madai ya watumishi?.
Umeona eh yan unakuta unasumbuliwa Sana kufatilia haki yako wakat ni swala dogo sana isitoshe serikal inapesa
 
Back
Top Bottom