Muda wa kujadili mfumo wa Muungano ni sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muda wa kujadili mfumo wa Muungano ni sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Apr 27, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 26 April 2012 09:31 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]Profesa Maina

  Peter SarambaLEO tunaadhimisha miaka 48 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar iliyozaa taifa la Tanzania mnamo mwaka 1964.
  Miaka 48 ni umri ya utu uzima ingekuwa ni kumzungumzia mwanadamu. Ni umri ambao mambo mengi yamekuwa yametokea, yakiwemo mazuri na mabaya.
  Ni kipindi kinachotosha kujitathmini kwa nia ya kusonga mbele kwa kurekebisha kasoro na kuboresha mafanikio kwa lengo la kusonga mbele zaidi.
  Tangu kuasisiwa kwa Muungano, wengi wamekuwa na maoni, mawazo na pengine fikra tofauti na zile za waasisi wa Taifa letu, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume ambao wote wametangulia mbele za haki.
  Moja ya changamoto zinazoikabili muungano wetu ambao kwa hakika hakuna anayeweza kuuondoa kwa kutumia mipaka, sera au mfumo wa uongozi kutokana na kuingia na kuzama katika mifupa ya wakaazi wa sehemu hizi mbili za bara na visiwani ni aina au mfumo wa Muungano wa serikali mbili tuliyonayo sasa.
  Wakili wa Mahakama Kuu, Method Kimomogoro ameitaka serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMS) na ile ya Muungano kuacha hofu ya kuvunjika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iwapo mjadala huru na wa wazi utaruhusiwa kuhusu mfumo na aina ya Muungano tunaopaswa kuwa nao miaka mingine 48 ijayo.
  Akizungumza katika mahojiano maalum mjini Arusha juzi, kufuatia harakati na vuguvugu kuhusu muungano unaoendelea Zanzibar ambako watu 12 wanashikiliwa na polisi kwa kuvamia viwanja vya Baraza la Wawakilishi kushinikiza kuonana na Spika wa baraza hilo, Pandu Ameir Kificho, Kimomogoro alisema njia salama ni kuruhusu na kuongoza mjadala huo badala ya kutumia dola kuuzuia.
  “Viongozi waache watu wajadili kwa uhuru aina ya Muungano tulionao sasa kwa nia ya kuuboresha, wasikimbilie wala kukumbatia hofu kuwa watu kujadili Muungano na mfumo uliopo una nia ya kuvunja. Kinachotakiwa sasa ni kuongoza jadala huo badala ya kutumia nguvu kuuzuia,” anasema Kimomogoro.
  Akifafanua, wakili huyo alisema hakuna chombo, kikundi wala nguvu yoyote inayoweza kuvunja mahusiano ya kindugu kati ya Wazanzibari na Watanganyika uliokuwepo tangu enzi za mababu kwa sababu ni vigumu kuwatofautisha watu kutoka sehemu hizo mbili ndiyo maana kuna koo kubwa na maarufu zinazopatikana pande zote mbili.
  Anasema ushirikiano uliopo kati ya wananchi wa bara na visiwani pamoja na ukanda mzima wa Afrika Mashariki unadhihirishwa na uamuzi wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyekuwa tayari kuchelewesha uhuru wa Tanganyika kuzisubiri nchi za Kenya na Uganda.
  “Baada ya uhuru na Tanganyika kuamua kufuata siasa za kijamaa, Kenya ilionekana kama maadui wetu kutokana na kukumbatia ubepari wakati kiongozi wa Uganda Marehemu Idd Amin Dada tulikuwa tukimwimba na kumwita Nduli, joka na majini mengine mabaya, lakini leo tuko nao kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki,” anasema.
  Anahoji hofu ya viongozi na watawala kuhusu kuvunjika Muungano ambao tayari umo ndani ya Jumuiya ya EAC ambao inaelekea kwenye Muungano wa kisiasa.
  Wakili Komomogoro alisema ni haki kwa Watanzania kujadili na kukubalia aina na mfumo wa Muungano watakaoingia nao kwenye shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki iwapo ni ya serikali moja, mbili au tatu, yenye shirikisho itakayoshughulikia na kusimamia mambo yote ya EAC.
  Anasema hata kama wananchi wataamua kuunda serikali ya Tanganyika sambamba na ile ya Zanzibar iliyopo sasa pamoja na serikali ya shirikisho, bado Muungano utaendelea kudumu ndani ya EAC kama ambavyo nchi zingine wanachama watajiunga lakini serikali zao zikiendelea kusimamia mambo yasiyo kwenye mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na itakapoundwa shirkisho la kisiasa.
  “Hofu ya serikali moja au tatu inatoka wapi wakati tayari tuna mfano hai wa watu kuendelea kushirikiana katika mambo ya msingi baada ya vyama vya Afro Shirazi (ASP) na Tanganyika African Union (TANU) kuungana na kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwaka 1977?” Anahoji Kimomogoro.
  Anasema kama ambavyo muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeendelea kudumu na kubaki imara baada ya vyama hivyo kuungana na kuunda chama kimoja, ndivyo pia uwepo wa serikali moja au tatu utaendelea kudumumisha muungano kwa sababu kinachoungana siyo vyama wala serikali bali watu.
  “Nani anaweza sasa kusimama na kuwatenganisha Watanzania kwa misingi ya ubara na Uvisiwani? Hakuna. Wananchi wameungana kwa kiwango ambacho hawawezi kutengana tena, wameoleana na hakika hivi sasa wapo Watanzania wengi wasiojua Tanganyika wala Zanzibar zaidi Tanzania,” anasema Kimomogoro.
  Anahoji iwapo mtu atajitokeza na kutaka kuuvunja Muungano Watanzania hao waliozaliwa ndani ya Muungano atawapeleka wapi.
  Anatoa mfano wa muingiliano wa kindugu uliopo katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo makabila ya Waluo, Wamaasai, Wahaya, Wahangaza, Wamakonde, Wanyasa, Wameru na wengine kadhaa hujikuta wakiwa na ndugu
  wa damu katika nchi zote.
  “Ukienda Kenya na Tanzania utawakuta wajaluo na Wamaasai, kama ambavyo Wahaya, Wahangaza, Wanyambo wa Tanzania walivyo na undugu na Waganda wa Uganda na Watusi na Wahutu wa Rwanda na Burundi. Sasa hawa utawatenganishaje kwa kutumia mipaka ya nchi?” Anahoji Wakili Kimomogoro.
  Akitangaza orodha ya wajumbe wa Tume ya Katiba mpya, Rais Jakaya Kikwete alisema licha ya watu kuwa huru kujadili Muungano. Lakini mjadala huo hautahusu mfumo na aina ya muungano uliopo, hoja inayopingwa na watu wenye kutilia shaka mfumo wa serikali mbili wakipendekeza serikali moja au tatu.
  Wakati zikiungana mwaka 1964, Zanzibar ilisalia na serikali yake inayoshughulikia na kusimamia mambo yote yasiyo ya Muungano wakati Tanganyika ilipoteza serikali yake ikabaki kuhudumiwa na ile ya Muungano.
  Pamoja na kuwa na viti vingi vinavyotambulisha utaifa wake kama bendera, wimbo wa Taifa, timu za taifa katika michezo mbalimbali, serikali (SMZ) na vikosi vya ulinzi na usalama (vikosi vya SMZ), Zanzibar bado haitambuliki kimataifa kama nchi.
  Akiahirisha kikao cha Baraza la Wawakilishi mwishoni mwa wiki iliyopita, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd alipiga marufuku kongamano, warsha na mihadhara ya kujadili mfumo wa muungano uliopo akiyaita ya kichochezi yenye lengo la kuhatarisha amani na utulivu huku akiahidi kuwa serikali itakabiliana kikamilifu na watakaokaidi amri hiyo.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...