Muda wa kuapishwa kwa rais baada ya uchaguzi, nataka probation kwa rais mtarajiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muda wa kuapishwa kwa rais baada ya uchaguzi, nataka probation kwa rais mtarajiwa

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Chitu, Dec 22, 2011.

 1. Chitu

  Chitu Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutokana na mchakato wa kuandika katiba mpya mie nina 'oni' moja tu nalo ni kuhusu kula kiapo kwa Rais, katika nchi zinazoendelea rais akitangazwa tu jioni kala kiap. Kwa mtazamo wangu hii kwa kiasi fulani nadhani inachangia katika uibaji kura hasa kwa wale ambao wapo madarakani.
  Kwavile tuna rule of law basi kama uchaguzi wetu unakuwa October, rais aapishwe tarehe 1 ya mwaka unaofuata, yaani kuwe na kipindi cha miezi 3 kutafakari nini kimetokea kabla ya rais mpya kuingia madarakani pia kutoa nafasi ya kubadirishana mawazo kati ya rais mtarajiwa na anayepita, ndivyo tufanyavya tunapoingia kwenye kazi mpya, au siyo jamaani?.
  Kwanini hakuna probation ya urais? Jamani tuliangalie hili nadhani kama tunaweza kulisimamia ipasavyo basi kuweka miezi mitatu ya kusubiri kuapishwa kwa rais kutasaidia kupunguza rushwa kwenye uchaguzi, Ki vipi? ni kwa vile wagombea watajuwa kuwa baada ya uchaguzi kuna miezi mitatu ya watu kudadavua nini kimetokea na nani kaiba kura ila kwa utaratibu mgombea anaiba kura, unakula deal na tume, anatangazwa na kuapishwa kitendo ambacho kinampa kinga ya kutoshitakiwa tena. Kwa maana nyingine, wagombea wengine wanabaki kunung'unika tu na kuandika kwenye magazeti, tunaitaji mabadiriko kwa ili pia. Ila kama tukiweka sheria kama hii, kila mgombea atakuwa na discipline kuwa hata akishinda kuna miezi 3 ambayo ni mingi kugundua kichafu alichokifanya na kumdisqualify hata kama tume itakuwa imemtangaza. Sasa ni bora wajuwe hao wanaotaka urais kuwa atakuwa under scruitine and surveilance kwa miezi mitatu. Hii inatufaa kwa nchi kama yetu ambayo kila mgombea anatoa rushwa: why not sisi, au sisi ni uchu wa madaraka?
  Tukumbuke utaratibu huu wa sasa uliwekwa kwa sababu zamani Nyerere na Mwinyi walikuwa wanagombea na Vivuli, kwa sasa tunavyama vingi why tuendelee na mifumo ya aina hii ya kizamani bila hata kutafakari ilikotokea?

  Nawakalisha maoni!!!!
   
Loading...