Muda Uwaziri mkuu wa Mh. Pinda wahesabika

Pinda hatihati kubeba zigo la rais JK kama ilivyokuwa kwa Lowassa. Wabunge CCM waache unafiki. Tatizo ni rais mbabaishaji...
 
Ni kupoteza muda hata kujadili mambo ya jk...huyu ni failed president amalize muda wake aondoke
 
Kutokana na riport ya kamati maalumu kuchunguza mwenendo wa oparation maalumu ya kutokomeza ujangili kufichua uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu ni dhahiri sasa muda wa Mh. Pinda mtoto wa mkulima kuwa waziri mkuu unafika ukingoni, hii imejidhihirisha kutokana na michango ya wabunge mbalimbali na iwapo mh hatajiuzulu atakua amepoteza imani kubwa ya utendani wake kwa wananchi.

kituo cha sheria na haki za binadamu Tanganyika law society walipo mpeleka pinda mahakamani Baadhi ya watanzania waliwadhihaki wataalamu wale waliyoenda mahakamani kwa kauli wapigwe tu. Mnachoshangaa leo bungeni ni nini? Ukipofu wetu ndiyo unaotumaliza na propaganda za kipuuzi kwenye mambo ya msingi. Kauli ya wapigwe tu ilitosha kumtoa pinda uwaziri mkuu, watu wenye nia njema yatupasa tuwaunge mkono ma siyo kuleta majungu.

Bunge litimize wajibu wake kwakumvua pinda uwaziri mkuu kwani kauli yake ya wapigwe tu imegharimu taifa na watu wamepigwa kweli.
 
Hebu tuelezeeni kilichojiri huko maana wengine tulikuwa mbali na tv

Ni kwamba: bungeni siku ya leo walikuwa wanapokea taarifa ya Kamati ya Maliasili ndipo baada ya mawasilisho ya kamati ikafuata muda wa wabunge kuchangia. Kutokana na ukatili uliotendwa na waliopewa dhamana kwe Operation Tokemeza Ujangiri. Kwa kuwa watu wameuwawa, watu wamebakwa, watu wamelazimishwa kuzini na wanyama waliokufa, mifugo imeuwawa nk. Ndipo wabunge wakachangia kwa uchungu huku wakimkalia kooni Waziri mkuu achie ngazi. Ila Mh. Msigwa akaenda mbali na mwisho akawataka Mh. Nchimbi, Mh. Pinda, Waziri wa Ulinzi na waziri wa Maliasili waachie ngazi pia wamuombe ladhi Mh. Maige kwa kumuwajibisha bila hatia.
 
"tatizo ni sisi kuwaajiri wezi, wauaji na bado tunachekacheka tu"
 
Karata pekee itakayomuokoa ni kwa Kagasheki,Shamsi na Nchimbi kujiuzulu kabla ya bunge kuhairishwa
 
Unazania waziri mkuu kumuondoa ni kama vil;e kumuondoa Zitto ?

Mkuu huwa nafuatiliaga posts zako humu na kuona mashambulizi na kejeli unazopata.Ila leo kwa hii post yako nimejiridhisha kwamba una tatizo maana kama umesikia mchana huu yaliyosemwa kwenye ripoti ya Lembeli na michango ya wabunge wengi wanaochangia usingethubutu kuja na kauli kama hiyo. Hili linawezekana tu kwa mtu anayefikiri kwa staili tofauti.
 
Ni kwamba: bungeni siku ya leo walikuwa wanapokea taarifa ya Kamati ya Maliasili ndipo baada ya mawasilisho ya kamati ikafuata muda wa wabunge kuchangia. Kutokana na ukatili uliotendwa na waliopewa dhamana kwe Operation Tokemeza Ujangiri. Kwa kuwa watu wameuwawa, watu wamebakwa, watu wamelazimishwa kuzini na wanyama waliokufa, mifugo imeuwawa nk. Ndipo wabunge wakachangia kwa uchungu huku wakimkalia kooni Waziri mkuu achie ngazi. Ila Mh. Msigwa akaenda mbali na mwisho akawataka Mh. Nchimbi, Mh. Pinda, Waziri wa Ulinzi na waziri wa Maliasili waachie ngazi pia wamuombe ladhi Mh. Maige kwa kumuwajibisha bila hatia.

Asante sana kiongozi
 
Ni kweli operesheni imefanywa kwa namna isiyo sahihi kabisa na wahusika wanapaswa kuwajibishwa, kuanzia viongozi na wale waliokuwa wakitekeleza zoezi hili. Viongozi inawapasa kuwajibika kwa kutowawajibisha watu wao wa chini ambao walifanya mambo kinyume na mwongozo wa operesheni.

Nikiachana na madudu yaliyotokea kwenye Operesheni husika, Bunge lina nafasi nzuri sana kama mhimili mmoja wapo wa Serikali kuonyesha kuwa kile kilichofanyika si sahihi na hivyo wahusika wanapaswa kuwajibishwa na mhimili mwingine wa Serikali yaani Judiciary, haitoshi kuwavua madaraka tu lakini lazima mkondo wa sheria uchukue nafasi yake kwa kuwakilichofanyika ni uhalifu. Legal actions has to follow.

Lakini pia kisiasa naona kuna namna ambavyo hata ndani ya CCM kuwepo kwa mgawanyiko tofauti na kile tulichozoea cha kuunga mkono kila jambo linalofanywa na Serikali kuu. Hapa naweza kuona kuna ukomavu wa kisiasa kwa baadhi ya Wabunge wa CCM lakini pia naweza kuona siasa za chuki na kulipiza kisasi ambazo katika hili zina faida kwa sababu ya kuweka wazi uhalifu uliofanyika kwa baadhi ya Wabunge wa CCM ambao kwa namna moja waliathirika na uteuzi wa mawaziri na baadhi kukuta wakiachwa kwenye baraza la mawaziri kwa sababu ya tuhuma mbalimbali.

Wabunge wa vyama pinzani nao wana role ya kufanya katika hili maana waliothirika ni Watanzania ambao wanawategemea wawakilishi wao kulisemea hili.

Watanzania wengine hawapaswi kujiona kuwa wapo salama dhidi ya udhalimu huu, hili likipita kimya kimya, wengine pia watajikuta kwenye uonevu wa namna hii katika maeneo mengine ya nchi.

Poleni mliofikwa na maswahibu haya. Tuombe haki itendeke kwa wahalifu hawa wa haki kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwa mabaya waliyoyatenda.
 
Wabunge wa ccm hawana ubavu wa kumtoa pinda hata kidogo, labda wa upinzani na bahati mbaya ni wachache bungeni!
 
Back
Top Bottom