Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 10,323
- 6,848
Hivi muda huu wa takribani mwaka 1 na miezi 10 uliobaki kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu unaruhusu kufanyika kwa uchaguzi mdogo ili kujaza nafasi ya kiti cha ubunge kilichoachwa wazi na marehemu Mgimwa ambae alikuwa ni mbunge wa kuchaguliwa kupitia chama cha mapinduzi(CCM)?
Kwakweli kuna umuhimu wa kubadili sheria ili kuepuka gharama za uchagzi mdogo kwa nchi kama hii liyokubuhu kwa umasikini.
Hivi ndiyo vitu kati ya mambo makubwa sana na ya msingi ambayo inabidi yawe addressed kwenye katiba mpya, kwa sababu chaguzi ndogo zinatugharimu sana kifedha kama nchi. Haya majimbo sasa inabidi yawe yanakuwa under trusteeship ya wabunge wa kuteuliwa wawili au mmoja, wayashilkilie hadi uchaguzi mkuu mwingine utakapofika. Na kwa kuwa kwenye katiba ijayo panaweza pasiwe na viti maalum, ingekuwa vizuri kama Rais atapewa mamlaka ya kuteua watu kushika majimbo haya (mmoja au wawili), na watu hawa wathibitishwe na Bunge la JMT baada ya Rais kuwa amefanya uteuzi wao. Yaani chaguzi ndogo zifutwe kabisa kwa sababu zimetugharimu mno mpaka sasa hivi. Mimi kwa kweli huwa nikisikia uchaguzi mdogo, huwa napata mawazo na bashasha utadhani hela inayokwenda kutumika kule inatoka mfukoni mwangu, huwa tunatumia hela nyingi mno kwenye chaguzi ndogo ukilinganisha proportion yake na fedha ile ambayo huwa tunatumia kwenye uchaguzi mkuu