gwamaka aswile
Senior Member
- Mar 26, 2015
- 186
- 106
SERIKALI imeendelea kuongeza makusanyo ya mapato yake kufikia karibu Sh trilioni 1.5 katika kipindi cha Januari mwaka huu. Hii ni habari njema kwa Watanzania, kwasababu inaonesha jinsi vyanzo vyetu vya mapato vinaweza kututoa katika utegemezi wa hali ya juu kwa wahisani.
Juhudi hizi zitatufikisha kwenye utegemezi mdogo au kutuondoa huko kabisa, ikiwa vyanzo hivyo vitadhibitiwa vizuri kuhakikisha havitumiwi kujaza mifuko ya wachache. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile, makusanyo ya Januari yamevunja rekodi ya yale ya Desemba mwaka jana ambayo yalikuwa Sh trilioni 1.4.
Katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika Dar es Salaam juzi, Dk Likwelile alisema, sasa Serikali inajivunia kugharamia miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za ndani, bila kutegemea za wahisani.
Aidha, aliwaeleza kuwa, makusanyo ya mapato kwa sasa ni mazuri na kila mwenye jukumu la kusimamia mapato hayo na kuyakusanya anawajibika katika eneo analopaswa, ilimradi kuhakikisha ukusanyaji haukwami.
Pia, Dk Likwelile alisema Serikali ina uhakika wa kuvuka lengo la kukusanya mapato yake yote, lengo likiwa kupunguza utegemezi na kuendesha miradi yake muhimu ya maendeleo bila kusubiri fedha za wahisani.
Alisema hilo linawezekana kutokana na mfumo mzuri uliopo sasa wa kubana matumizi yasiyo ya lazima pamoja na kuhakikisha kila anayepaswa kulipa kodi analipa kwa wakati kwa kiasi kinachostahili, si vinginevyo.
Pamoja na Dk Likwelile kueleza mafanikio hayo ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk John Magufuli, Watanzania wamekuwa wakijionea wenyewe matokeo chanya ya utendaji wa Serikali hiyo katika kuhakikisha maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya afya, elimu, uchumi na nyingine.
Hizo zote zimeanza kufanikiwa kwasababu ya kubana matumizi yasiyo ya lazima, ambayo tunaamini watanzania wengi watakuwa mashahidi kwamba Rais Magufuli amekuwa chachu kuu ya kuyabana, hivyo kutuonesha njia nyeupe ya kuelekea kuyafikia maendeleo tunayoyataka.
Majibu ya swali hili; endapo Tanzania inaweza kufanya mambo yake ya maendeleo kwa asilimia kubwa ya fedha zake na kidogo kutoka kwa wahisani au bila kutegemea mkono wa huruma kutoka kwa yeyote nje ya mipaka yake, tayari yameanza kutolewa na Serikali hii tena kwa vitendo, kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa kwa mafanikio ikiwemo ya barabara.
Hongera Serikali kwa hatua hiyo tunayoamini kuwa itatunyanyua na kuwa kidedea miongoni mwa nchi zinazoendelea, kwamba tumethubutu na kuweza kukanyaga hatua nyingi mbele bila utegemezi.
Uthibitisho kuwa tunaweza kuleta maendeleo unaonekana kwa kila mzalendo anayeukubali ukweli, kutokana na makusanyo ya mapato na fedha zinazotengwa na Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya vipaumbele.
Dk Likwelile alisema, kwa mwezi huu wa Januari, Serikali imetenga Sh bilioni 318.406 kutoka vyanzo vya ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo iliyopewa kipaumbele. Tuunge mkono juhudi hizo kwa kulipa kodi na kutunza miradi.