Mtaka Haki
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 492
- 149
Kwa kawaida jambo la muhimu sio tu kufanya jambo la muhimu.
Ni muhimu kufanya jambo la muhimu wakati muhimu na unaofaa. HAPO NDIPO JAMBO LA MUHIMU LITAPEWA UMUHIMU.
Viongozi wengi wanalijua hili ndio maana mikutano inayowezekana kuzungumzia wizi wa kura itazuiliwa kipindi hiki kwa sababu hizo hizo za timing.
Chadema wamesikika kuwa wanajiandaa kutoa ushahidi kwa wananchi juu ya wizi wa kura na ni nani alihusika. Hayo yote ni ya muhimu. Lakini katika nchi kama hii yetu muda unapokwenda ndipo suala hilo linapoachwa kupewa kipaumbele.
Hatimaye watu watakuwa hawaoni tena kama hilo ni moja ya mambo ya muhimu kwao.
Pia muda unapoenda badala ya wao kufikiri mlikuwa mnatafuta vielelezo vya kutosha basi watadhani mnatengeneza vielelezo.
Ushauri wangu. Anzeni kutoa mifano kidogokidogo ya yaliyo wazi. Niliwahi kutoa mfano wa gazeti la mwanahalisi kuwa liliwahi kutoa mfano wa kura zilizofanana kwa wagombea wote wa uraisi katika maeneo mawili tofauti ya uchaguzi.
Kwa bahati mbaya Mwanahalisi nao hawakufafanua waliwaacha watu waone wenyewe.
Kama kuna kitu CCM ilikosea ni timing. Walikosea wakati muafaka wa kuleta hoja ya maisha binafsi ya Dr. Slaa watu wakawa wameshamkubali na pia wanaona hizo hoja zinatengenezwa, hatimaye wakaona labda kuna ukweli lakini wakapuuza kwani hoja zake na msimamo na waliyoyataka kwake yalizidi tatizo lililokuwa linatakiwa lionyeshwe kuwa ni kubwa.
Pia CCM waliwanyima viongozi wao kushiriki mdahalo wakati tayari mmoja alishashiriki na kuonekana kuwa amezidiwa katika mdahalo huo. Hivyo kunyima midahalo baada ya mmoja kulipeleka ujumbe mzito kuwa hofu ni kuwa wananchi wakihoji mambo ya msingi wengi walioomba kwa ticket ya CCM watakuwa na wakati mgumu wa kujibu tuhuma nzito za ufisadi nk.
USHAURI KWA CHADEMA. ANZENI KUTOA MFANO MIDOGO MIDOGO HUKU MKISEMA HII NI MIFANO MICHACHE KATI YA NYINGI, TAARIFA KAMILI ITATOLEWA BAADAE
Mimi siichukii CCM wala viongozi wake. Lakini nachukia dhuluma na kama ipo basi iwekwe hadharani hata kama aliyedhulumu ni baba yangu nitamhimiza kufuata misingi ya haki.
Kwa kuanzia tunaomba wenye mifano michache ya maeneo yao kama ile ya Mwanahalisi waiweke hapa.
VYAMA VYA UPINZANI ITA WAANDISHI WA HABARI WAONYESHE VIELELEZO VICHACHE VISIVYOWEZA KUKATALIWA. KISHA ENDELEA KUONGEZA KIDOGO KIDOGO then tuone yote kwa pamoja.
Time will tell if you keep on waiting. NAOMBA KUWASILISHA