Muda sahihi wa kuonyesha wizi wa kura umekaribia kwisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muda sahihi wa kuonyesha wizi wa kura umekaribia kwisha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Nov 27, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kawaida jambo la muhimu sio tu kufanya jambo la muhimu.
  Ni muhimu kufanya jambo la muhimu wakati muhimu na unaofaa. HAPO NDIPO JAMBO LA MUHIMU LITAPEWA UMUHIMU.
  Viongozi wengi wanalijua hili ndio maana mikutano inayowezekana kuzungumzia wizi wa kura itazuiliwa kipindi hiki kwa sababu hizo hizo za timing.

  Chadema wamesikika kuwa wanajiandaa kutoa ushahidi kwa wananchi juu ya wizi wa kura na ni nani alihusika. Hayo yote ni ya muhimu. Lakini katika nchi kama hii yetu muda unapokwenda ndipo suala hilo linapoachwa kupewa kipaumbele.
  Hatimaye watu watakuwa hawaoni tena kama hilo ni moja ya mambo ya muhimu kwao.
  Pia muda unapoenda badala ya wao kufikiri mlikuwa mnatafuta vielelezo vya kutosha basi watadhani mnatengeneza vielelezo.

  Ushauri wangu. Anzeni kutoa mifano kidogokidogo ya yaliyo wazi. Niliwahi kutoa mfano wa gazeti la mwanahalisi kuwa liliwahi kutoa mfano wa kura zilizofanana kwa wagombea wote wa uraisi katika maeneo mawili tofauti ya uchaguzi.
  Kwa bahati mbaya Mwanahalisi nao hawakufafanua waliwaacha watu waone wenyewe.
  Kama kuna kitu CCM ilikosea ni timing. Walikosea wakati muafaka wa kuleta hoja ya maisha binafsi ya Dr. Slaa watu wakawa wameshamkubali na pia wanaona hizo hoja zinatengenezwa, hatimaye wakaona labda kuna ukweli lakini wakapuuza kwani hoja zake na msimamo na waliyoyataka kwake yalizidi tatizo lililokuwa linatakiwa lionyeshwe kuwa ni kubwa.
  Pia CCM waliwanyima viongozi wao kushiriki mdahalo wakati tayari mmoja alishashiriki na kuonekana kuwa amezidiwa katika mdahalo huo. Hivyo kunyima midahalo baada ya mmoja kulipeleka ujumbe mzito kuwa hofu ni kuwa wananchi wakihoji mambo ya msingi wengi walioomba kwa ticket ya CCM watakuwa na wakati mgumu wa kujibu tuhuma nzito za ufisadi nk.

  USHAURI KWA CHADEMA. ANZENI KUTOA MFANO MIDOGO MIDOGO HUKU MKISEMA HII NI MIFANO MICHACHE KATI YA NYINGI, TAARIFA KAMILI ITATOLEWA BAADAE
  Mimi siichukii CCM wala viongozi wake. Lakini nachukia dhuluma na kama ipo basi iwekwe hadharani hata kama aliyedhulumu ni baba yangu nitamhimiza kufuata misingi ya haki.
  Kwa kuanzia tunaomba wenye mifano michache ya maeneo yao kama ile ya Mwanahalisi waiweke hapa.
  VYAMA VYA UPINZANI ITA WAANDISHI WA HABARI WAONYESHE VIELELEZO VICHACHE VISIVYOWEZA KUKATALIWA. KISHA ENDELEA KUONGEZA KIDOGO KIDOGO then tuone yote kwa pamoja.
  Time will tell if you keep on waiting. NAOMBA KUWASILISHA
   
 2. H

  Hegelyakoni Member

  #2
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kitu kimoja unapaswa kufahamu ndugu yangu, ni kuwa Viongozi wetu wakuu wa Chadema wanahekima kuu ya utambuzi wa mambo ukiachana na zitto pekee,tena ni wasomi mahiri wa nyakati.weka masikio on .utasikia moto.
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ushauri wako unafaa hasa kwa wakati huu ambao inasemekana chadema wamezuiwa kufanya mikutano.
   
 4. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Click hapa uone Dk. Slaa: Uchaguzi wizi mtupu | Gazeti la MwanaHalisi

  Ninachomaanisha kinatakiwa kiendelee ni taarifa ikiwezekana kila kinapopatikana bila kuwa na haja ya kungojea kukusanya taarifa zote. Mnaweza mkaanza na wilaya moja huku na nyingine kule.

  Narudia tena kusema kuwa nia yangu ni kutaka Tanzania yetu itende kwa haki kwani AMANI INAZALIWA NA MATENDO YA HAKI.
  DHULUMA IKIACHWA HATA AMANI INAWEZA KUTOWEKA.
   
 5. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe Hegelyakoni, Ushauri mdogo tu wangeanza hizo cheche kisha kuwasha moto kama ambavyo ilikuwa kwenye Mwanahalisi kwa wingi sana.

  Mfano mmoja huu.

  Hapa Dr. Slaa alisema " Ninaenda kuanika kila kitu. Ingependeza wakaendelea kutoa picha kidogo kidogo hata kwa kuwatumia wabunge wake then aje na kila kitu. Sasa muda umenda sana anika kimoja kimoja kuliko kusubiri.

  AHADI YA DR. Slaa

  CHADEMA: Matokeo yetu yamehujumiwa | Gazeti la MwanaHalisi
   
 6. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HTML:
  
  
  Mbunge mmoja mmoja akiongea na vyombo vya habari kabla ya Dr. Slaa kujumlisha itakuwa ni bora kwani wengi wanasikiliza radio.
  Hawatazuia radio kutangaza.
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Unaposema muda wa kuwasilisha malalamiko mahakamani umekaribia kwisha kwani muda wa kishera ni wa miezi mingapi?
   
 8. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Muda ninaozungumzia sio wa mahakama. Kwa mfano suala la kura za uraisi huwezi kupeleka mahakamani.
  Ila ninachozungumza ni suala la kuanika irregularities na mambo yasiyokuwa ya haki. Wakati unakaribia kwisha kwani kuna wakati mood ya uchaguzi inakuwa imepita. Mfano wanaoangalia masuala ya uchaguzi hapa JF ni zaidi kidogo ya mia. Wanaoangalia makala za siasa wako zaidi ya 800 ninapoandika hapa. Hii ni kuwa muda unapoendelea kupita interest za watu juu ya jambo hushuka.
   
 9. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 10. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Please try to be reasonable and post logical threads......
   
 11. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Help me to understand what is not reasonable and illogical here!
   
 12. M

  Msharika JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kereng'ende umechakachuliwa huna macho ya kuona mambo. na ubongo wako una space 0.02MB. unadata mapema
   
 13. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kereng'ende I stood to be corrected and waiting for your correction.
   
 14. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu usiumize kichwa. Kuna watu ambao response zao huwa ni kusema tu, "Illogical, hapana etc" bila kueleza wanapinga nini. Usiumize kichwa, jishughulishe na wanaokuunga mkono au kukupinga kwa hoja.

  Binafsi bado naamini ukubwa wa jambo hutegeme na muda linapowasilishwa, kwa kifupu nakubaliana na wewe.
   
 15. g

  glojos88 Member

  #15
  Nov 27, 2010
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania yetu hii inahitaji consistency kwenye kila kitu. Ufuatiliaji bado sio mkubwa. Kwa mfano Suala la Elimu bure na Afya bure si jambo la kuacha na mifano iko mingi.
  Nimekuwa Norway na nilishangaa kuona wananchi hawalipii huduma ya Afya wala elimu kuanzia nursery hadi chuo kikuu.
  Pamoja na ukweli kuwa Norway ni nchi tajiri sana. Lakini inawezekana. Hivyo naunga mkono timing na naongeza Consistency ya hoja na isiwe ni wakati wa uchaguzi tu.
   
 16. s

  seniorita JF-Expert Member

  #16
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Is what is logical what you want to hear? Because you cannot stand the truth,the truth hurts. Plus what is logical to you cannot be logical to wapenda haki; ndio maana unaomba kusema "please"
   
 17. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuhusu kesi zinazofunguliwa mahakamani, kama mahakama kuu ikitumia vigezo vya haki juu ya kuvurugika kwa uchaguzi basi majimbo mengi yatakuwa nulified. Kwani vielelezo vya kukosekana kwa haki na rushwa ni vingi mno.
  Kesi za takukuru zimeishia wapi?
   
 18. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  watawakilisha ushahidi gani wakati hamna kitu? kilichobaki ni propaganda na kulia wezi wezi ili waonewe huruma.

  utakuja kuniambia slaa hana ushahidi wa kuibiwa zaidi ya haya wapambe wake mnayoyaongea hapa jamvini.

  wewe uliona wapi aliyeibiwa anamtaka aliyemwibia aende mahakamani?

  endelea kusubiri na kuamini daktari wenu wa ukweli alishinda. viti 23 vya ubunge katika 239 na viti kama 500 vya udiwani katika viti 5000. urais eti daktari wa ukweli ameshinda. nyie mnahitaji mkapime akili zenu kama ziko salama
   
 19. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #19
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jenifa, Hutaweza kupima kutokuwepo kwa wizi kwa kuangalia watu walivyoshinda viti kadhaa kati ya vilivyokuwepo kwani watabakia wakisema ndio maana kuna wizi. La muhimu bado na la haki ni kuanza kuweka ushahidi hadharani angalao kidogo kidogo.
   
Loading...