Muda sahihi wa kuiweka Dar es Salaam kwenye “lockdown” ni sasa

mike2k

JF-Expert Member
May 12, 2016
1,458
3,127
Tunaelewa umuhimu wa jiji la Dar es Salaam katika maisha ya Watanzania na nchi jirani. lakini kwenye hili suala la corona hakuna kuzubaa tena. Mamlaka husika iweke utaratibu mzuri wa kulibana hili jiji ili kuzuia na kupunguza kabisa kasi ya usambaaji wa covid19.

KWANINI NIMEWAZA HIVYO?
Interaction ya Dar na maeneo mengine ya nchi hii italeta shida sana. Sasa hivi hakuna mjadala tena sasa hivi serikali inazuia maambukizi ya ndani kwa ndani na jiji la dar ndo limekuwa na cases nyingi zaidi za huu ugonjwa.


further reading
Wuhan ends coronavirus lockdown – in pictures
Coronavirus - Quora
 
Bandari isifungwe kwani mizigo haiwezi kuambukiza Corona

Airport weka sehemu ya kupima wanaoingia na kuwakarantini
Wananchi wanatakiwa wasisogeleane karibu
 
Kama unataka lockdown si ukae kwako ujifungie wewe na familia yako kwani nani atakuzuia.
Yaani watanzania wafe kwa njaa kisa Corona hebu tutumie akili kidogo tu kuwa asilimia kubwa ya wananchi hawaijui kesho yao itakuwa vipi.

Sasa mnavyolazimisha lockdown wewe utawapelekea chakula au kisa baadhi yenu mnaotaka Hilo jambo mko vizuri kiuchumi na mmeajiriwa serikalini hali ya kuwa huko vijijini watu kula tu imekuwa shida halafu unataka wafungiwe wenzio ndani huu ni upumbavu uliopitiliza

NI KWELI CORONA INAUA NA LAZMA TUCHUKUE HATUA ILA LOCKDOWN NI JANGA KUBWA KULIKO CORONA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mike2k,
Mkuu hajali yuko huko kwao kwenye isolation macho yote yako hazina 24/7 nini kinaingia kila Siku.

Shangaa pamoja na mikorona yote hiyo Trafiki wako barabarani,wanakusanya mapato. juzi nilikutana na TRA wako bize wanakimbizana na wajasiliamali wadogo, nikauliza nyie hamwogopi mikorona?
 
Mpaka sasa serikali imeshaonyesha ulinzi wa raia dhidi ya Corona awataki kujivika hayo majukumu.

Solution ni kwamba ‘abiria chunga mzigo wako’ hakuna namna.
 
Yaaani nikisikiaga tu mtu anaongeleaga kuhusu kupitishwa Lockdown Miguu yote inakufa ganzi.

Kwani Mmelazimishwa Kutoka Jamani?

I know you want to be seen as an intelligent and a person who thinks rationally na mwenye mawazo ya tofauti But This Is Not The right Time.

BTW hujalazimishwa Kutoka mkuu. Stay Safe Indoors.
 
Anza na amri ya kufunika mdomo na pua nchi nzima muda wote hadi nyumbani ndo approach isiyokuwa na madhara kiuchumi. Tukikaa wazi midomo na pua usitegemee muujiza wa kumaliza maambukizi

.
 
PNC,
LOCKDOWN NI MUHIMU SANA KIPINDI HIKI. SISI NI NCHI MASIKINI DAWA PEKEE ITAKAYOTUSAIDIA NI KUTHIBITI HUU UGONJWA KWENYE JIJI LA DAR. HAyo mawazo yako ya chakula ni kwa sababu ya njaa tu.

lakini ugonjwa huu ni hatari kuliko njaa ukishasambaa nchi nzima ndo utakapoelewa changamoto yake. tuna cases study nzuri tu ya kinachoendelea EUROPE(ITALY NA SPAIN) Hizi nchi zime suffer licha ya utajiri wao mkubwa.

PNC uchache wa information na accurately data ndo unapelekea kuwa na mawazo kama hayo ya chakula. sawa utapata chakula, utaambukiza na utasambaza tatizo kwa sababu ya shallow mind.

FURTHER READING
India 'to extend' nationwide coronavirus lockdown
 
Mkitaka lockdown, ongeeni na CHADEMA waseme kwasababu shughuli za kawaida hazijazuiwa na wao wanaingia kwenye shughuli za kawaida za kukijenga chama. Walahi kesho haitafika bila kutangazwa total of total lockdown.
 
Kinachotakiwa kufanyika ni kusambaza vifaa vya kupimia kila kata ili watu wapimwe kwa wingi kila siku iendayo kwa Mungu
Italy wameshindwa kwa mbinu hii. Urahisi ni kufunika mdomo na pua, mgonjwa akihisi kuambukizwa asitoke nyumbani apige simu (bongo naona 199) maana akipanda mwendo kasi ataacha virusi. Tofauti na hapo tusubiri lock down tufe njaa ingawa wanasiasa wanasema hakuna lockdown.
 
Back
Top Bottom