#COVID19 Muda ni mwalimu mzuri: Waliochoma chanjo ya Corona pekee ndio watakaoruhusiwa kufanya ibada ya hija

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,486
2,332
Tulipopiga kelele kuhusu hili suala tulionekana ni mazuzu, viongozi wa Bakwata walikuwa busy kumsifu na kumtukuza mfalme huku wakisema hili jambo ni story za kitaa. Muda ni mwalimu mzuri, haya wote tuongee lugha moja sasa.

========

Mamlaka za nchini Saudi Arabia zimesema watu waliopata chanjo ya Corona peke yake ndio wataruhusiwa kufanya ibada ya Hija mwaka huu huko Mecca.

Wizara ya Hija na Umrah imetoa taarifa kuwa watu waliopata chanjo pekee ndio watakuwa na vigezo vya kujihi mwaka huu katika mji mtakatifu wa Mecca.

"Watu ambao tayari wamepata chanjo dozi mbili za COVID-19, na wale ambao wamepata chanjo dozi moja ya Corona siku 14 kabla ya Hija au mtu ambaye ametoka kupona Corona", wizara imesema.

Wizara hiyo imesema pia kuwa itazingatia taratibu zote za kujikinga dhidi ya maambukizi ya Corona.

Haijawekwa wazi kama sera hiyo itaendelea mpaka wakati wa Hija kuu baadae mwaka huu.

Saudi Arabia imeripoti kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona zaidi vya zaidi ya watu 393,000 na zaidi ya vifo 6,700 vinavyotokana na virusi hivyo.

Wizara ya afya ya Taifa hilo imesema watu zaidi ya milioni tano wamepata chanjo dhidi ya Corona, katika Taifa lenye watu zaidi ya milioni 34.

Mwezi uliopita mfalme Salman alimbadilisha Waziri wa Hija, alafu mwezi mmoja baadae ilifanyika Hija ndogo katika mfumo mpya wa kihistoria kutokana na changamoto ya virusi vya Corona.

Mwaka jana, waislamu 10,000 ambao ni wakazi wa Saudi Arabia ndio waliruhusiwa katika Hija takatifu mwaka jana, ingawa mara zote huwa ni watu milioni 2.5 kutoka duniani kote na ndio walishiriki mwaka 2019.

Chanzo: BBC
 
Wewe ndio zuzu tunaosafiri nje ya nchi mbona wanachanjwa?

Mtu akitaka kwenda USA, Europe, Hijja au hata Burundi, choma kinga, kaa 72 hrs daka tiketi ondoka, sasa bla bla hizi za nini?

Yaani unataka serikali ianze kumdunga kila mtu mtaani?
 
Mmmmmhhh

Ibada hiyo ni kwa sharti moja kuu

Ikiwa una uwezo wa kwenda

Kama wameweka Sharti hilo,na ww huna imani na Chanjo

Basi uwajibu wa Hijjah kwako umeanguka mpaka pale utakapokubali chanjo kwa ridhaa yako au itakapo ondolewa na kutokuwa sharti la kuingia Saudia kwa ajili ya Hijjah

Uislam ni Dini nyepesi
 
Mmmmmhhh

Ibada hiyo ni kwa sharti moja kuu
Ikiwa una uwezo wa kwenda...

Kama wameweka Sharti hilo,na ww huna imani na Chanjo,
Basi uwajibu wa Hijjah kwako umeanguka mpaka pale utakapokubali chanjo kwa ridhaa yako au itakapo ondolewa na kutokuwa sharti la kuingia Saudia kwa ajili ya Hijjah

Uislam ni Dini nyepesi
Well said.....FATWA !!
 
wewe ndio zuzu tunaosafiri nje ya nchi mbona wanachanjwa?


mtu akitaka kwenda USA, Europe, hijja au hata burundi ....choma kinga, kaa 72 hrs daka tiketi ondoka


sasa bla bla hizi za nini?

yaani unataka serikali ianze kumdunga kila mtu mtaani?
Chanjo gani unapatiwa kwa hapo Tanzania?au NYUNGU...
 
Sisi wa nyungu waturuhusu tubebe tu,na majani ya mikaratusi kidogo maana hakuna namna
 
Si wangeacha tu hadi corona iishe kuna ulazima wa kiasi gani kwenda kuwakusanya mamilioni ya watu na hayo maradhi?
 
Back
Top Bottom