Muda gani umvumilie mwanaume ambaye hana kazi

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,311
7,494
Kawaida inajulikana mwanaume ndio baba wa familia kuanzia huduma hadi ulinzi. Kama hana kazi, mkewe au mpenzie avumilie na kumhudumia mpaka atakapopata kazi au kibarua cha kumpatia pesa.

Lakini unaweza kuhudumia familia mpaka mwanaume akajisahau kuwa nini wajibu wake na ukahisi kuchoka kumhudumia.

Ni muda gani mwanaume apewe ili apate kazi au kibarua muda huo mwanamke ahudumie familia?
 
Si chini ya miaka 3, ndani ya hiyo miaka utaanza kuona mabadiliko lazima, ikipita hiyo miaka bila kazi za uhakika basi hata ubongo wake utaanza kuchoka na kuwaza vitu ambavyo hakutegemea kufanya na hapo ndio anapoukaribisha umasikini.
 
Inategemea hana kazi kwa sababu gani, kama anaumwa au kafukuzwa kazi haina shida sana, mvumilie mpaka akili ikae sawa.

Lakini kama mwanaume ni Kiazi tu anakaa ndani sebuleni kazi yake ni kuangalia katuni na kuchapa watoto, piga chini.

Nb.Wanawake acheni ubinafsi.
 
We miaka 3 unaona mingi sana?? Kwamba una haraka sana?? Wanawake mna haraka sana ya kufanikiwa na ndio maana mnatumika sana.
Silaha ya mafanikio ni UVUMILIVU tu.
Miaka 3 atasahau wajibu wake walai
 
Inategemea hana kazi kwa sababu gani,kama anaumwa au kafukuzwa kazi haina shida sana.

Lakini kama mwanaume ni kiazi tu anakaa ndani kuangalia katu na kuchapa watoto,piga chini.

Nb.Wanawake acheni ubinafsi.
Asante
 
Kawaida inajulikana mwanaume ndo baba wa familia kuanzia huduma hadi ulinzi

Kama hana kazi,mkewe au mpenzie avumilie na kumhudumia mpaka atakapopata kazi au kibarua cha kumpatia pesa

Lakini unaweza kuhudumia familia mpaka mwanaume akajisahau kuwa nini wajibu wake na ukahisi kuchoka kumhudumia

Ni muda gani mwanaume apewe ili apate kazi au kibarua muda huo mwanamke ahudumie familia ?
Wewe hudumia familia suala la muda gani muachie Mungu.
 
Inategemea kama unafahamu

Dhumuni la Ndoa yenu.
Ni kanisani au laaa.

Ndoa ya Kikristo haivunjikagii.

Kumbuka viapo vyenu.

Kifo ndio kitanganishi kikuuu.

Sasa wewe unazungumza habari ya hela .

Hakuna eneo lolote nimeona ktk kiapo cha ndoa kikisema pesa kiwatenganishe.

Vumilia hata hiyo pesa ya kuhudumia Familia unapata kupitia yeye
 
Kawaida inajulikana mwanaume ndo baba wa familia kuanzia huduma hadi ulinzi

Kama hana kazi,mkewe au mpenzie avumilie na kumhudumia mpaka atakapopata kazi au kibarua cha kumpatia pesa

Lakini unaweza kuhudumia familia mpaka mwanaume akajisahau kuwa nini wajibu wake na ukahisi kuchoka kumhudumia

Ni muda gani mwanaume apewe ili apate kazi au kibarua muda huo mwanamke ahudumie familia ?
Mkuu, kuna tofauit ya kuhudumia familia na kuhudumia mwanamume. Kazi ya kuhudumia familia sio ya mwanaume peke yake na wale sio ya mwanamke peke yake bali ni ya wana familia.Inapotokea mwanaume hana kazi au ajira haimaanishi kwamba wajibu wake wa kuhudumia familia umekoma na kwamba sasa apate pumziko bali anapaswa kuendelea kutimiza wajibu wake kwa namna yoyote kwa kadiri ya uwezo wake na pale atakapofikia ndipo hapo mtaishi kwa kadiri ya uwezo wenu.

So jibu langu ni kwamba kama unao uwezo wa kuhudumia huyo ni wako milele na kama unahisi unamuendekeza hilo ni tatizo lingine sio tatizo la pesa au matunzo.Ni kwamba umenza kumchoka na kumuona ndezi na halina uhusiano na matunzo bali ni kisingizio chako tu ambacho umekipata cha kwa nini huoni umuhimu wake kwako.

Ikiwa unahisi hivo kaeni mzungumze mtafuta suluhu ya kudumu ya hiyo hali ninyi pamoja.Pembeni ya hapo endeleeni kupambana.Kumbuka siku ukiachana naye kwa sababu ya kukosa uvumilivu ndo siku atafanikiwa kupata kazi. na pisi nyingine mpya
 
Mkuu,kuna tofauit ya kuhudumia familia na kuhudumia mwanamume.Kazi ya kuhudumia familia sio ya mwanaume peke yake na wale sio ya mwanamke peke yake bali ni ya wana familia.Inapotokea mwanaume hana kazi au ajira haimaanishi
Kama haonyeshi nia ya kutafuta kazi
 
Inategemea mpo kwenye hatua gani ya mahusiano yenu, kama ni uchumba piga chini fasta huyo mtu, wote tunajua jukumu la kuhudumia mahusiano ni la mwanaume, kama hana mishe muda wake na akili yake yote awekeze kwenye kusimama kimaisha na sio mahusiano.

Unajua mwanamke hajaumbwa kuhudumia familia na ndio maana wengi wakifanya ivyo mwishowe wanakuwa na contempt na huyo mwanaume.
 
Inategemea kama unafahamu

Dhumuni la Ndoa yenu.
Ni kanisani au laaa.

Ndoa ya Kikristo haivunjikagii.

Kumbuka viapo vyenu.

Kifo ndio kitanganishi kikuuu.

Sasa wewe unazungumza habari ya hela .

Hakuna eneo lolote nimeona ktk kiapo cha ndoa kikisema pesa kiwatenganishe.

Vumilia hata hiyo pesa ya kuhudumia Familia unapata kupitia yeye
Samahani mkuu, hivi hili suala la kusema kuwa ndoa za kikristo hazivunjiki huwa mnalitoa wapi?
 
Kawaida inajulikana mwanaume ndo baba wa familia kuanzia huduma hadi ulinzi

Kama hana kazi,mkewe au mpenzie avumilie na kumhudumia mpaka atakapopata kazi au kibarua cha kumpatia pesa

Lakini unaweza kuhudumia familia mpaka mwanaume akajisahau kuwa nini wajibu wake na ukahisi kuchoka kumhudumia

Ni muda gani mwanaume apewe ili apate kazi au kibarua muda huo mwanamke ahudumie familia ?

Utaolewaje na Mwanaume asiye na kazi?
Hiyo ni Dalili ya ujinga na upumbavu,
Labda uniambie kipato kidogo lakini mwanaume hawezi kosa kazi,

Yaani akae nyumbani Kama mwali!
Hakuna vibarua, hakuna udalali, hakuna Bodaboda, hakuna kazi yoyote, hiyo haipo.

Hiyo sio mwanaume wa kumuoa mwanamke anayejielewa.

Ikiwa mwanamke anayejielewa hakosi kazi hata ya kuuza vitumbua sembuse Dume zima.

Huwezi mvumilia mtu anayevunja sheria ya Mungu ya kufanya Kazi,
Huyo lazima atakuwa anadharau kazi.
 
Back
Top Bottom