Muda gani sahihi wa kuyafanya haya kwenye mahusiano?

Qassim14

Senior Member
Oct 10, 2017
182
202
Salaam wakuu wa idara zote,

Kama kichwa kinajieleza,

Mada ni muda gani sahihi wa kumchunguza mtu hadi unakuja kuwa na mahusiano nae ya kimapenzi? Pia ni muda gani baada ya kuwa nae katika mahusiano unafaa kukutana nae kimwili?

Ni hayo tu nawasilisha mada kaeni kwenye viti mada ipo mezani inahitaji mchango wa hali na mali kunisuru tunaolia lia na mapenzi ya kupemda sana halafu kuumia zaidi.

Karibuni.
 
Una mchunguza ili ugundue nini? Sioni haja ya kumchunguza kwa sababu utawapoteza wengi sana, kila mtu anamapungufu. Kama mtu anakupenda anakupenda tu.
Kujua tabia ya mtu ni kazi kubwa mnooo hata upewe miaka 10 hautaweza kujua vyote.
Tendo pendwa inategemeana na hisia zenu.
 
Kupata mtu sahihi kwako ni bahati tu....
Kuna watu wanakutana bar na kusex siku hio hio baada ya miaka miwili wanafunga ndoa na kuishi kwa furaha. ..

Na kuna watu wanakutana nakufanya uchumba kwa miaka mitatu bila kusex lakini wakaachana mara tu baada ya kusex hata ndoa hawajaiona..

Mke/mume mwema anatoka kwa Mungu sali sana umpate mampema..
 
Mkuu unaweza kumchunguza hata mwaka mmoja na bado akaja kuzingua mbeleni, siku hizi mapenzi kamari, tena kamari ya karata 3, unayoamini ndio sio na uliyoiacha ndiyo
 
Acha uzinzi jombaaa!
Muda sahihi wa kukutana kimwili ni baada ya kuoa na kuthibitishwa na sheikh au mchungaji au bomani!
{kama ukiweza lakini}
 
Unapotafuta Mwenza unapaswa uwe na Vigezo vyako vitakavyokuongoza.., endapo utamuona anaefikia angalau asilimia 75 huyo anafaa, ingawaje yote hayo pamoja na kuchunguza hayakupi uhakika wa kudumu ama kuishi kwenye Ndoa kwa Furaha, hivyo ni bora ukazidisha ukaribu na Muumba!!!
 
Kupata mtu sahihi kwako ni bahati tu....
Kuna watu wanakutana bar na kusex siku hio hio baada ya miaka miwili wanafunga ndoa na kuishi kwa furaha. ..

Na kuna watu wanakutana nakufanya uchumba kwa miaka mitatu bila kusex lakini wakaachana mara tu baada ya kusex hata ndoa hawajaiona..

Mke/mume mwema anatoka kwa Mungu sali sana umpate mampema..
Asante jibu ni hili
 
Una mchunguza ili ugundue nini? Sioni haja ya kumchunguza kwa sababu utawapoteza wengi sana, kila mtu anamapungufu. Kama mtu anakupenda anakupenda tu.
Kujua tabia ya mtu ni kazi kubwa mnooo hata upewe miaka 10 hautaweza kujua vyote.
Tendo pendwa inategemeana na hisia zenu.
Uko sahihi kabisa, huwezi kumchunguza mtu ukamaliza
 
Una mchunguza ili ugundue nini? Sioni haja ya kumchunguza kwa sababu utawapoteza wengi sana, kila mtu anamapungufu. Kama mtu anakupenda anakupenda tu.
Kujua tabia ya mtu ni kazi kubwa mnooo hata upewe miaka 10 hautaweza kujua vyote.
Tendo pendwa inategemeana na hisia zenu.
thanks
 
Salaam wakuu wa idara zote,

Kama kichwa kinajieleza,

Mada ni muda gani sahihi wa kumchunguza mtu hadi unakuja kuwa na mahusiano nae ya kimapenzi? Pia ni muda gani baada ya kuwa nae katika mahusiano unafaa kukutana nae kimwili?

Ni hayo tu nawasilisha mada kaeni kwenye viti mada ipo mezani inahitaji mchango wa hali na mali kunisuru tunaolia lia na mapenzi ya kupemda sana halafu kuumia zaidi.

Karibuni.
Haina kanuni mkuu na usicomplicate sana katika kutafuta mwenza wako.Mimi naamini kuwa mwenza wako yupo pale ulipo
 
Sikiliza moyo wako unasemaje unaweza mpata mwenye kila kigezo unachotaka ila moyo wako haupo kwake just unamchukulia poa tu na we utaangukia sehem ambayo unachukuliwa poa mapenzi kuna mda n zaidi ya biko
 
Nasikia ametumwa.MTU kuchunguza bombardier yetu Canada sijui ataleta majibu gani?
 
Mimi Vya kuchunguza ni Je sio mchawi? Sio uvccm? hayo mengne yanavumilika.
 
Ukimchunguza sana kuku hutamla mkuu...

Manaake katika mihangaiko yake ya kutafuta chakula huwa wanakula hadi mavi haswa haswa wale wa kienyeji ambao nyama yao huwa tamu sana.

Ukimchunguza sana mtoto wa kike/kiume hutaingia kwenye mahusiano asilani haswa hiki kizazi chetu cha dot com. Backgrounds nyingi zinatisha!
 
Unaweza kumchunguza mwaka mzima ukaridhika ukaja oa/olewa nae ndo ukagundua kumbe ulibugi! Ilhali mwenzio aliefanya tofauti mapenzi yake na mwenzio yanazidi kunoga.

Mnaweza kutana leo na mkagegedana na mahusiano yakadumu vilevile.. Mwingine akasubiri mpk ndoa akaishia kulaani tu kila siku.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom