Mubashara: Mauzo ya vito vya madini ya Tanzanite

PseudoDar186

Member
Mar 18, 2017
89
224
Wanajamvi,

Niko hapa nimetulia naangalia jinsi hereni, bangili, pete na cheni za madini ya Tanzanite yakiuzwa mubashara kwenye channel ya Shop LC nchini marekani.

Ndani dakika takriban tano, pete 20 za carat 0.35 ya AAA grade Tanzanite ziliuzwa kwa US$ 1,600 kila moja kwa ujumla wa US$ 32,000 (TShs 73.5 million). Watu wanapiga simu, wanaweka credit card number na kununua live - halafu wanaletewa nyumbani.

IMG_5847.JPG

IMG_5840.JPG

IMG_5851.JPG

Inabidi tujitahidi kufanya ‘value-addition’, ‘marketing’ and ‘branding’ - tusijikite kwenye kuchimba tu. Yani hawa wanaouza hawajawahi kufika mgodini.

IMG_5845.JPG

IMG_0012.JPG
 
Tulioko bongo tuangalie kwa njia ipi?.
?
Wanajamvi,

Niko hapa nimetulia naangalia jinsi hereni, bangili, pete na cheni za madini ya Tanzanite yakiuzwa mubashara kwenye channel ya Shop LC nchini marekani.

Ndani dakika takriban tano, pete 20 za carat 0.35 ya AAA grade Tanzanite ziliuzwa kwa US$ 1,600 kila moja kwa ujumla wa US$ 32,000 (TShs 73.5 million). Watu wanapiga simu, wanaweka credit card number na kununua live - halafu wanaletewa nyumbani.

View attachment 1147632

View attachment 1147633

View attachment 1147634

Inabidi tujitahidi kufanya ‘value-addition’, ‘marketing’ and ‘branding’ - tusijikite kwenye kuchimba tu. Yani hawa wanaouza hawajawahi kufika mgodini.

View attachment 1147649

View attachment 1147647
 
Magufuli ana mapungufu yake lakini nilikua nawashangaa sana watu waliokua wakipinga ukuta wa mererani na reforms za mikataba na sheria za madini, kile kituo cha uuzaji wa madini pale Arusha nasikia ndani ya wiki mbili baada ya kufunguliwa kilifanya biashara ya zaidi ya billion 3.7
 
Haya mambo ndo inatakiwa tuelimishane na kuendelea mbele zaidi lakini watu wanapinga haya mambo mazuri hawana hata hoja za msingi.
 
Magufuli ana mapungufu yake lakini nilikua nawashangaa sana watu waliokua wakipinga ukuta wa mererani na reforms za mikataba na sheria za madini, kile kituo cha uuzaji wa madini pale Arusha nasikia ndani ya wiki mbili baada ya kufunguliwa kilifanya biashara ya zaidi ya billion 3.7
Mkuu mbona mauzo ayo ufanyika kila baada ya miezi mitatu huko USA...Jiulize pamoja na kujenga ukuta kipi kimebadirika..maana ata Korosho tumeshindwa kulipa
 
Mkuu mbona mauzo ayo ufanyika kila baada ya miezi mitatu huko USA...Jiulize pamoja na kujenga ukuta kipi kimebadirika..maana ata Korosho tumeshindwa kulipa
Tanzanite imepanda bei sana, hata makusanyo ya kodi yake yamekuwa Makubwa tatizo Watanzania pamoja na magufuli tulifikiri tutapata trillions kwenye haya mawe yaani tulikuwa na mategemeo Makubwa sana kuliko uhalisia wa mambo

Japo pamoja na hivyo hali kwa sasa ni nzuri tofauti na zamani shamba la bibi.
 
Ukweli ni kwamba sisi kama watanzania hatuna kipato cha kutosha cha kununua madini yetu wenyewe. Ila akili tunazo za kutosha tu. Tufanye kitu kimoja - tuwekeze kwenye masonara katika masoko yenye uwezo wa kununua haya madini jamani. Imagine madini ya Tanzanite yanapatikana nchi yetu peke yake - tukitaka kuyapandisha bei tunapunguza uzalishaji. Halafu yawe yanapatikana kwenye maduka yetu peke yake!

Mbona China wameweka patent / IP protection kwenye Panda? Yani kila panda, popote alipo duniani ni wa Mchina. Tujiongeze!
 
Back
Top Bottom