Mubashara Buyungu: Nape aeleza sifa za mbunge, asema Chiza anatosha, wananchi wamuitika

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009
Wananchi wa jimbo la Buyungu kwa kauli moja wameahidi kumpa ushindi wa kishindo mgombea ubunge jimbo la buyungu kupitia CCM mhandisi Christofa Chiza. Wana buyungu kata ya katanga wametoa ahadi hiyo mbele ya mbunge wa mtama Nape Moses Nnauye alipowapa sifa za mbunge anayetakiwa kuliongoza jimbo lao. Nape alizitaja sifa hizo kuwa ni wananchi kumjua, naye kuwajua wananchi, uwezo wa kueleza matatizo, uwezo wa kujua sehemu ya kuyapeleka matatizo hayo na uwezo wa kutafuta majibu na kuyarudisna kwa wananchi. Naye mgombea ubunge eng. Chiza alipopata fursa ya kuomba kura aliahidi kuenenda katika sifa hizo na kutatua kero za wananchi huku vipaumbele vyake vikiwa ni elimu,maji,afya na barabara
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom