Mubarak, Gbagbo walikuwa ni Zaidi ya DC wa Igunga

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,443
Tukio la kukamatwa na kuwekwa chini ya Ulinzi la Mkuu wa Wilaya ya Igunga Fatuma Kimario limezua Mjadala Mzito sana. Asubuhi hii nimeamkia Mada iliyoanzishwa na Mzee Mwanakijiji iliyokuwa na Kichwa cha Habri "Je Unaijua Misingi iliyounda Taifa letu?" Yeye aliguswa na Picha za Igunga na Maisha ya wana Igunga kiujumla ukilinganisha na Maisha ya "Watanzania wa Dar Es Salaam". Amezungumzia juu ya haki inayojengwa juu ya UTU na si SHERIA.

Binafsi nmeguswa na tukio la Mkuu wa Wilaya ya Igunga kukamatwa akiwa na Nyaraka za Tume ya Uchaguzi ilhali yeye si mtumishi wa tume ya Uchaguzi. Vile vile nikaangalia hatua zilizochukuliwa dhidi ya Wabunge wa Chadema na Kauli MbaliMbali zilizotolewa na Makada Maarufu wa CCM

Wengi wao wanaonekana kuguswa na suala hili kwa Kigezo Cha Udhalilishaji wa Mwanamke lakini hawa hawa Hawakupiga kelele Pale Jeshi la Posili lilipowadhalilisha Viongozi wanawake wa Chadema kule Arusha kwa kuwapiga na kuwajeruhi vibaya na hata kuwadhalilisha Kijinsia. Kwa Hawa Vipofu wa CCM Mwanamke ni zaidi ya Viongozi wa Kike wa Upinzani ( This is animal farm principle)

Lakini kuna kipofu wa CCM amenadika kwenye wall yake ya Facebook kwamba "Haya ndiyo watakayo wenzetu" huku ameshika gazeti linalomwonesha DC akiwa chini ya Ulinzi. Alikuwa anamaanisha kwamba wale wananchi wametumwa na CDM, kwamba CDM ndiyo wanawachochea wananchi. Huu ni upofu kwa Kiongozi wa Calibre yake. Kwamba anataka kutuainisha kwamba Binadamu wanaishi katika Kipande cha Dunia kiitwacho Tanzania ni Tofauti sana na Wanaishi Libya, Tunisia, Sudan, Misri, Syria na kwengine. Kwamba Binadamu hawa wanaweza kuvumilia Unyanyasaji wa kila aina Pasi kuchukua hatua. Siwezi kumshangaa maana hata Gadaf mwaka mmoja uliopita alikuwa anawaza hivyo hivyo.

Wengine wamesikitika eti kwa Sababu aliyefanyiwa kitendo hicho ni Mkuu wa Wilaya, Hivi kama Bagbo na Jeshi lake aliweza kukamatwa na kutiwa chini ya Ulinzi akiwa na Kitaulo itakuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga?

Jana wananchi wamemkimbiza Msoma mita ya maji just because since june maji hayajatoka hata tone halafu kila mwezi wanakuja kusoma mita sasa utasema hao nao wametumwa na CDM

Hivi wanafikiri watanzania ni Wajinga mpaka washindwe kuelewa na Kupambanua nini Maana ya kumkuta Mkuu wa Wilaya na Barua za Maombi ya kusimamia Uchaguzi? Hivi wanatufanya sisi ni Mazoba sana au?

Hivi wanafikiri Wananchi wa Libya hawakuona wenzao wa Misri walipokuwa kufa wakati wanamkimbiza Mubarak? Au Wamisri hawakuona Kilichawkuta wapigania haki Tunisia? Hivi wanafikiri kwamba kwa Kukumbushiakumbushia yaliyotokea Libya kunaweza kuwafanya Watanzania Kurudia Uoga wao?

Uvunjivu wa Amani uko mikononi mwa Viongozi kama wasipokuwa tayari kutoa haki kwa Hiyari Basi wajiandae KULAZIMISHWA

Hakuna Silaha iliyowahi Kuzuia Nguvu ya Uma, tumeona Venezuela, tukaona Misri, Tunisia na hata Libya na kote kilichosabisha ni Viongozi kulewa Ugimbi wa Madaraka

Kilichotokea Igunga kinatoa Ishara tu kwamba Watanzania wako tayari kuchukua Hatua Nyingine zaidi kama watahisi Haki zao za Msingi zinaminywa


[h=1][/h]
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom