Muangalieni Msanii mwingine huyu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muangalieni Msanii mwingine huyu!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by BAK, May 4, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Hivi nchi ingekuwa na sheria, hawa mapapa mafisadi wangekuwa na kiburi walichokuwa nacho!? Sitta bora ukae kimya tu na kuwaacha wenye uchungu wa Tanzania kupambana na hawa mafisadi bila woga. Maana uongozi uliokuwepo unawaogopa na sababu za kuogopwa kwao zinajulikana.

  Date::5/4/2009
  Sita aonya malumbano yasiyo na tija

  Fredy Azzah

  Mwananchi

  SPIKA wa Bunge la Tanzania Samuel Sita, amewataka wafanyabiashara na wanasiasa wanaotuhumiana kupitia vyombo vya habari kuachana na tabia hiyo na kuziacha sheria za nchi zichukue mkondo wake.

  Akijibu swali kutoka kwa mmoja wa wanahabari aliyetaka kujua maoni yake kuhusiana na wafanyabiashara wanao hukumiana kwa kuitana mafisadi, Sita alisema kitendo hicho siyo kizuri kwa sababu kuna sheria.

  "Nasita kidogo kuwasema wafanyabiashara kwa sababu labda wana maslahi yao binafsi, lakini suala la kuhukumiana siyo zuri, tuache sheria zifuate mkondo wake, kama mtu tayari kafikishwa mahakamani tuache mahakama ifanye kazi na pale itokapo hukumu ndio tumuite fisadi au majina yote yale mabaya," alisema Sita.

  Sita ambaye alikuwa mgeni rasmi katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, aliyasema hayo jana nje ya ukumbi wa Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

  Mapema wakati akitoa hotuba yake Sita aliwataka wanahabari kutokubali kutumiwa na wanasiasa na matajiri ili kutoa habari zisizo na tija kwa nchi pamoja na kuingiza chuki na ubinafsi.

  Katika hatua nyingine Sita aliwataka wanahabari kushikamana kuhakikisha sheria zinazokandamiza uhuru wa vyombo vya habari nchini zinabadilishwa.

  Sita ambaye alitolea mfano sheria ya magazeti ya mwaka 1976 pamoja na sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1995, aliitaka serikali kuzipeleka bungeni sheria zinazolalamikiwa ili ziweze kufanyiwa marekebisho.

  "Natoa wito kwa serikali kuziwasilisha bungeni mapema iwezekanavyo sheria zote zinazo lalamikiwa ili ziweze kufanyiwa marekebisho, binafsi naunga mkono jitihada zote zitakazo leta uhuru wa vyombo vya habari nchini," alisema Sita.

  Siku ya uhuru wa vyombo vya habari huadhimishwa duniani kila mwaka Mei 3.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Binafsi namuunga mkono Sitta, sheria za nchi zipo zifuatwe, hakuna haja watu wazima kuwa, wasomi kuwa kama wajinga vyombo rasmi vya kumaliza tofauti zetu vipo na viachwe vifanye kazi zake. Kuna watazania wengi wanauchungu na hali ya mambo inavyokwenda tirigivyogo, na hawana chombo cha habari cha kwenda kubwatuka, wafanyeje? wachukue hatua mikononi mwao kuwapiga mawe wale wanaosababisha hali hiyo? hawana njia mbadala ya kuwashughulikia?
  kama kila mtu atakuwa na staili yake ya kumaliza tofauti na mwenzake au wenzake,na kupuuza sheria,jamani nchi hii itakalika kweli? Mbona zipo nchi zimefanikiwa kunyoosha mambo yao kwa sheria tu, kwanini watanzania washindwe.
  Nidhamu ya taifa imeondoka kwa kupuuza taratibu za nchi leo watanzania wote wanaacha kuzungumza yanayowahusu wanaongea ugomvi wa "matajiri" tu.
  Hebu nambieni tajiri gani katika mfumo huu wa kibepari anatajirika bila ya kumnyonya masikini?
  si Mengi wala hao aliowaita mafisadi papa, atakaeseama katajirika bila ya kumnyonya mnyonge wa nchi hii.
  Waache kuwatoa watu katika mood wa kuganga njaa zao na kuwaendekeza wao tu, anaehisi haridhiki sheria zipo, kama tumezikubali wenyewe basi zifuatwe.
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Sitta sio mtu wa kumuamini ni ndumila kuwili; si mnakumbuka jinsi alivyomzuia DR. Slaa asizungumzie kashfa ya EPA bungeni ikabidi aende akaifumue kule mwembeyanga na juzi juzi tena amemshambulia Slaa kuwa hoja zake ni za hovyo hovyo wakati alipozungumzia juu ya mishahara ya wabunge kuwa ni mikubwa sana! Sasa hapa anajigongagonga kwa sababu hawa wakina Rostam wamekwisha muwekea mtu wa kumuondoa ubunge kule Urambo mwaka kesho kwa hiyo anajaribu kujikomba wamuonee huruma. Sitta hana msimamo mathubuti ,he is always an opportunist and fence sitter.
   
 4. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  chuki binafsi my a... kwani wao hao matajiri wanatupenda sisi washika nepi, ndio maana wanatuuzia sumu, wanatuwekea mabomu mitaani, wanakula madini yetu, wanakula EPA, wanakula deepgreen hapendwi mtu chuki chuki mpaka kieleweke
   
 5. A

  August JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  tatizo la tanzania hio judicial independence hakuna, hivyo sheria kuchukua mkondo wake ni selective, hii ya mwenzute weka pembeni , hii sio mpeleke mahakamani, matokeo yake ndio hiyo ya kutumia pressure groups na sheria mkononi
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Hivi huyu si ndiye aliyesema kwamba mahakama zetu zimeoza, sasa anashangaa Mengi kuwatosa mafisadi hadharani? Alitaka kwenye mahakama alizozisema mwenyewe kwamba zimeoza? Vipi huyu naye tena!

  FMES!
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapa hakuna Sita wala tisa maana ukizijumlisha 6 + 9 = 69 ,uchafu mtupu ,hawa ndio hao hao wanaowakemea wabunge ,ndio hao hao wanaozuia masuali ndio hao wasio taka wengine waulizwe ,sasa wanapokuja na hoja hizi za kujisafisha ili waonekane watetezi wa wananchi huwa wamepiga mbali sana na hesabu zao ni kuyaweka mambo yaliyovurugika kwenye mstari kiasi ya kuwapa nafasi wajipange upya.

  Hawa ndio wanaopinga mabadiliko ya KATIBA hawa ndio wanaoweka vizuizi vya kurekebisha tume ,hawa ndio wanaowatilia vizingiti wanaotaka kuweka hoja binafsi ,leo wanakuja na hamrere na longolongo eti sheria za nchi zichukue mkondo wake ,mkondo gani huo ? mbona haueleweki ? Mkondo kwa nguruwe tu ?

  Wacheni kumuona mtu anasema kweli kwa kutumia mistari awapo kwenye kongamano ,jaribuni kufuata historia ya maamuzi yake awepo Bungeni , hivi kinachowasilishwa na sewrikali tu ndicho anachokiona kinafaa kuwa haki mbele ya wananchi na kuna wangapi walitaka kuwakilisha hoja na kuwekewa ngazi za kupanda na pengine hata kutishwa ,kwa kuwa tu kuna sheria ni lazima zifuatwe na ushahidi sijui na hili na lile ,watu wanataka kufikisha madai ya Katiba mbona hayasemei hapo na kusema leteni madai,kama kweli yeye anataka kufuatwa sheria basi awache demokrasia ya kuuliza masuali hapo bungeni bila ya kukingia kifua ,awache mtu atwangwe suali na awache mtu ajipapatue ,awache tabia ya kulindana ,kwa kuwa tu fulani mkuu au suali lina mtego ,jamani ndio hapo tutakapoweza kumuona kiongozi anaefahamu uongozi wake ,hata kama akitegwa ndio ujuzi wa uteguzi uonekane hapo ,kwani mikataba mingi ni mitego na wanaoingia ndio hao hao wanakingiwa kifua wanapooulizwa masuala ya mitego.

  Sita hana jipya ni mmoja wao.
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mwiba.
  siyo Sitta anaetaka sheria zifuatwe bali sheria zenyewe ndo zinataka hivyo. Hata sitta kama anayofanya bungeni kuzuia hoja ambazo wawakilishi wa wananchi wanataka zizungumzwe bila ya kufuata sheria, naye anakosea lakini kwa alichokisema katika vita hivi vya "wanene" ni sawa sawa, mtu mmoja kama Mengi anawafanya watanzania wote waache ku- focus na issue zao wamsikilize yeye, habari za anaowaita mafisadi papa nani hazijui,hapa kwenye JF walishajuulikana kabla hata Mengi hajawataja, CHADEMA wamewataja hadharani,mwembe yanga pale. Leo zogo nchi nzima kisa kasema Mengi, vitu ambavyo si vipya kwetu.
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Spika Sitta anaingilia

  1.Uhuru wa vyombo vya habari
  2.Uhuru wa wananchi kujieleza
  3.Uhuru wa wananchi kuwa na mawazo tofauti
  4.Uhuru wa mahakama

  Kwa ufupi tu.
   
 10. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Halafu isitoshe huyu mheshimiwa anataka watu wafuate mkondo upi wa sheria je ule wa kifisadi ambao umetawaliwa na rushwa na mizengwe?

  Au ule wa kuwaambia wananchi kinachoendelea kama anavyofanza mzee Mengi na kuwafumbua macho?
   
 11. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Hakuna sheria katika Tanzania ya leo. Kama kungekuwa na sheria basi wezi wote wa mali ya umma wangekuwa keko. Lakini Yona, Mramba na wenzake wangekuwa wananye debe.
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hakuna tena jina la usanii ni Mafisadi tu ,mambo mbele kwa mbele huku wakituchezesha gwaride au kwata.
   
 13. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Hivi si ndiyo huyu Sitta aliyekuwa wa kwanza kusema hadharani kwamba vyombo vya sheria vinatia aibu havitetei masilahi ya Taifa na kutumia kauri moja '' Liwalo na Liwe Potelea mbali '' Na akatoa mfano wa EWURA kufunga vituo vya mafuta Morogoro kwa kuuza mafuta machafu yenye mchanganyiko maji, mafuta ya taa na diesel na Mahakama ikasimamisha uamuzi wa EWURA na kuruhusu Wananchi watumie mafuta machafu ambayo athari zake nafikiri zinaendelea hadi leo!! Je, hadi hapo tuna vyombo vya sheria au uhuni mtupu!!!
   
 14. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kuna kipindi mzee sita alikuwa akionekana na msimamo tena usioendana na serikali saaana, utakumbuka maoni yake baada ya hotuuba ya raisi bungeni alipozungumzia EPA,alionyesha msimamo na ujasiri na uzalendo wa hali ya juu...lakini nahisi kama amepakwa mafuta ya kumlainisha kwa sasa...he is too negative about the opposition MPs..wakati wao ndio wanaojiahidi kuleta hoja za msingi za kizalendo...kuna siku waziri mkuu aliulizwa swali la deci akataka waziri wa fedha ajibu, sita akamzuia,why? PM anao uwezo wa kumhoji waziri wake...hii nchi sijui inaelekea wapi na viongozi wasio na msimamo...
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kidatu, Mpenda nchi,
  sheria zipo nchini kwa kuwa vyombo halali vilivyochaguliwa na wananchi ndivyo vilivyotunga sheria hizo, tatizo lililokuwapo hakuna wasimamizi wa kweli na wa haki wa hizo sheria. Inawezekana tukasema hao wezi ndo wasimamizi wa hizo sheria za kupambana wizi n.k
  Hili si tatizo lao ni tatizo la wananchi wenyewe waamue nani anafaa kuchaguliwa kusimamia sheria hizo kwa ukweli na haki, au angalau kwa kiasi na kipimo kitakachoonekana hivyo.
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ah mie najionea vituko tu maana kama mjuavyo kuna wakati hata mtu mzima huishiwa la kusema ilhali mdomo hautaki kufunga
   
 17. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  hii vita ishakuwa kubwa kwa hiyo naomba hawa wazee wasizeeke vibaya...wawe makini na midomo yao na mbaya zaidi ifike wakati tujuwe they are with us or against us...they come wit us or go wit 'em

  hii nchi haina sheria na hata kama ipo haina nguvu ya kushinda pesa za mapapa...ni jukumu la watanzania ku-take controll of our country

  A BULLET NEVER LIE
   
 18. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,158
  Likes Received: 5,588
  Trophy Points: 280
  Mi nilishasema hii serikali ya tanzania ilishakufa siku nyingi tumebaki na makapi yanatuongoza....
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,158
  Likes Received: 5,588
  Trophy Points: 280
  Huyu takataka anataka kutuambia nini kama mahakama zinashindwa waache wenye nchii wachukue mamlaka....
  Panchot sitta
   
 20. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Na wasiwasi na mawazo yako, kama wanaotunga sheria hawazifwati na mpaka leo hakuna kinachofanyika acha hao wenye hata kaujasiri kama puche ya ngano wajaribu kutetea nchi, kwa TZ sheria naona hazitafanikiwa kwa sababu hata mahakama zenyewe hazifwati hizo sheria, jaribu kupata kesi hata ya elfu 10 then uone hio kesi kuisha itakugharimu kiasi gani, watu wamechoka sio kwamba sheria hawazijui, na ukiona uvumilivu wa watu umefikia degree hii is bad indicator to the rulling part/gvnmnt.
   
Loading...