kuna ajali ilitokea na watu wengi walikuwa wamezunguka eneo ambalo ajali hiyo ya gari imetokea gari ilikuwa imegonga sasa kuna mwandishi alikuwa anataka apate japo picha mbili za kwenda kutoa gazetini lakini hakupata nafasi kwa sababu watu walikua wamezunguka eneo lote akaamua kutumia ujanja akema jamani aliyegongwa ni ndugu yangu naombeni mnipishe nimuone watu wote wakamwangalia kwa mshangao huku wakimpisha jamaa kufika tu akakuta kumbe ni fisi aliyekuwa amegongwa kilichoendelea mi sijui kwa sababu niliondoka mapema