Muamko wa Watanzania mwaka 1995 na 2010 ni sawa?


Chapakazi

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2009
Messages
2,880
Likes
15
Points
135
Chapakazi

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2009
2,880 15 135
Hizi ni twakimu za uchaguzi mwaka 1995, ambapo Mrema alikuwa mpinzani mkuu:

Mkapa - 61.82%
Mrema - 27.77% - Mpinzani Mkuu
Total votes - 6,846,681

Ukilinganisha na matokeo yaliyotangazwa leo:
Kikwete - 61.7%
Slaa ~ 26% - Mpinzani Mkuu
Total votes ~8.5 mil

Kwa kuangalia upesi upesi, muamko wa watanzania umekuwa mdogo sana katika kuleta demokrasia na ushindani imara katika siasi nchini. Kwa mtazamo wangu, hizi twakimu zinaonyesha mwamko hasi katika kuimarisha mchakato wa vyama vingi Tanzania. Hii inatia aibu na ni sikitiko kubwa sana!
Hatuwezi kuwa na mwamko ule ule katika kipindi cha miaka 15, na huku tunalamika ufisadi, umaskini na hali ngumu ya maisha! Lazima tuelewe umuhimu wa competition katika siasi. Angalia Marekani na nchi nyingine zilizoendelea.
Kutokana na kudorora kwa mchakato huu, ccm inaendelea kutunyanyasa, na kutuibia! Na ndio sababu kuu ya ishu kama EPA, RICHMOND, MEREMETA, KIGODA, MABANGO YA KAMPENI, nk kuendelea kupata nafasi katika taifa letu bila pingamizi.
Nadhani vyama vya upinzani vianze kampeni ya kuamsha wananchi na kuwaelimisha umuhimu wa siasi na uchaguzi na ushindani wa kweli!

Pia nadhani ni jukumu la tume ya uchaguzi kuweza kuwaamsha wananchi. Sijui bajeti yao kwa mwaka ni kiasi gani. Nadhani hilo nalo linahitaji kuangaliwa!
 

Forum statistics

Threads 1,236,927
Members 475,327
Posts 29,273,183