Muamar Gadafi mmiliki wa Bahari Beach Hotel? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muamar Gadafi mmiliki wa Bahari Beach Hotel?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, May 2, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  WAKATI mataifa ya Magharibi yakitafuta kumning’iniza kitanzini kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, kiongozi huyo ametajwa kuwa na hoteli nchini Tanzania.

  Hii ni hoteli ya Bahari Beach ambayo sasa inafahamika kwa jina la LAICO Bahari Beach Hotel. Hoteli ipo katika eneo la Kunduchi Mtongani, kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, yapata kilometa 14 kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam. Kwa taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam, hoteli hiyo ilinunuliwa na Gaddafi kupitia kampuni ya LAICO, yapata miaka minane sasa. Hoteli hii ilikuwa ikimilikiwa na serikali.

  LAICO ni kifupi cha Libya Africa Investment Company, kampuni iliyoanzishwa na serikali ya Gaddafi kwa lengo la kukuza biashara baina ya mataifa ya Afrika na nchi hiyo tajiri kwa mafuta. Tayari Umoja wa Mataifa (UN) umetaja LAICO kuwa miongoni mwa mali za Gaddafi zinazopaswa kuzuiliwa kwa madai kuwa, yeye na maswahiba zake ndio wananufaika na uwekezaji unaofanywa na kampuni hiyo.

  Aidha, serikali imekana kufahamu kuwa kuna mali za Libya au Gaddafi nchini. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, ameliambia MwanaHALISI kuwa hafahamu iwapo kiongozi huyo ana mali zozote nchini. “Mimi sifahamu kama Gaddafi ana mali zozote hapa nchini. Siwezi kusema hana kwa vile sina uhakika na ndiyo maana siwezi pia kusema zipo. “Na hata kama atakuwa nazo (mali), basi uwekezaji utakuwa si mkubwa sana kama ilivyo katika baadhi ya nchi ambazo zimetangaza kuzuia mali zake,” alisema Mahadhi. Hoteli ya Bahari Beach iliwekwa katika kundi la mali za umma ambazo zilitakiwa kubinafsishwa chini ya Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) katika miaka ya 1990.

  Wakati serikali ya Tanzania ikiwa bubu kuhusiana na mali za Gaddafi zilizopo nchini, Uganda tayari imetangaza mali za kiongozi huyo ambaye mataifa makubwa, kwa kutumia UN, yamedhamiria kumwondoa madarakani kupitia wapinzani wake wa ndani. LAICO imewekeza katika sekta ya hoteli, mabenki na mawasiliano nchini Uganda na serikali ya Yoweri Museveni inakadiria mali za LAICO kuwa na thamani ya dola milioni 345 (Sh.517 bilioni).

  Azimio Na. 1973 la UN lililotolewa Februari mwaka huu, lilizitaka nchi wanachama wa umoja huo “…kuwa makini na kufanya biashara na makampuni au taasisi za Libya” kwa vile hilo linaweza kuzifanya nchi hizo zionekane zinamsaidia Gaddafi kukandamiza wananchi wake. Kwenye tovuti ya LAICO, kuna taarifa kwamba kampuni hiyo inamiliki hoteli katika nchi 11 barani Afrika. Nchi hizo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Tunisia, Gambia, Mali, Burkina Faso, Gabon, Congo naGuinea. Kwa ujumla, LAICO inajidai katika tovuti yake kuwa ina vitegauchumi katika nchi 25 za bara la Afrika; katika maeneo ya utalii, mawasiliano, uchimbaji madini na hoteli.

  Akizungumzia vitega uchumi vya Libya vilivyopo nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Emmanuel ole Naiko, amesema ofisi yake haina taarifa yoyote kuhusu Gaddafi kununua mali nchini bali ana taarifa kuhusu mali za Libya. Amesema kwa mujibu wa rekodi zilizopo katika ofisi yake, kuna makampuni matatu ya Libya yaliyosajiliwa kufanya kazi zake hapa nchini. Ameyataja makampuni hayo kuwa ni LAICO, Pearl Investmant Limited na Tan Fruit Processing. “Sina taarifa zozote kuhusu mali za Gaddafi hapa nchini. Ninachojua ni kwamba kuna makampuni ya Libya ambayo yanafanya shughuli zake hapa nchini,” amesema.

  Bahari Beach hotel ilikuwa miongoni mwa hoteli kubwa zilizojengwa na serikali ya awamu ya kwanza.
   
 2. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  tusije tukalipa faini tu kwa kujifanya hatujui wakati tunajua ukweli wa mambo
  kam vipo ni kupiga stop tu au mkuu wa kaya anamuogopa conali Gaddafi

   
 3. D

  DOCTORMO Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Africa tunagawanywa NA KUPELEKEA kuchUkiana wenyewe kwa wenyewe maana tunapenda tuishi kama marekani ngoja tuvune tunachopandikizwa hapa. Leo hii nchi za africa zitaogopa kuwekeza kwakuogopa kuwa coloni la UN. Kwani ni nchi inayowekeza au ni raisi? Nchi za magharibi hazimpendi gaddaf sasa zinatuforce kwakutumia sheria hiyo KUSHIKILIA MALI ZA LIBYA NA WAASI KUONEKANA NDIYO WENYE HAKI na leo hii kumuona ni adui wetu. Kesho wataenda zimbabwe na eritrea ambazo siyo maadui wenu lakini mtafanywa nanyi mzichukie na muwe kundi moja na hao wakoloni. Africa tutakuwa under control ya magharibi baada ya kuanguka kwa libya, eritrea na zimbabwe hayo ndiyo yaliyo baki africa.
   
 4. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Waache waendelee kukana kuwa Gadafi hana mali nchini hadi waje wapigwe kama yeye mwenyewe ndiyo watasema
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Daa ule ukarabati wa ile hotel unatisha lazima ni pesa za petrol zile maana hazina auditor wala nini jamaa anazimwaga tu ukienda unasisimka kabisa kufuru!!
   
 6. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kampuni ya Libya siyo LIBYA AFRICAN, NI LIBYA ARAB INVESTMENT COMPANY, labda awe amebadilisha jina, lakini ninavyokumbuka mimi tangu walipoinunua na hatimaye hoteli kuanguka mpaka wafanyakazi wanakugombania kukuomba uwaachie tips, ilipokuwa ya serikali ilikuwa top mwanzoni mwa miaka ya 90, ndege zote zilipileka crew pale, baada ya gaddafi kununua ndio ikafa.
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2011
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Vipi status ya hii Hotel kwa sasa?
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hii hoteli wanipe mimi nitaiendesha vizuri tuu tena nitatoa ofa kila ijumaa
   
 9. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  mi nilihisi tu there is something unusual there. Afu ukarabati umeshamalizika longtime sijui kwanini hawafungui....labda wanasikilizia mtiti wa huko kwao kwanza kama utamfwata mpaka TZ kama zimwi.
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,912
  Trophy Points: 280
  kumbe serikali inauzaga hoteli xzake?
   
 11. bysange

  bysange JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2013
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 4,378
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu kwa hiyo waasi wa libya wameshakabidhi hoteli yao?
   
 12. m

  mahakama ya kazi JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2013
  Joined: Feb 20, 2013
  Messages: 1,469
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  tz kwa kuzuga kama hatujui vile
   
Loading...