Muafrika kuwa mwendesha mashtaka mkuu wa ICC

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Mataifa wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, yamekubali kumteua Fatou Bensouda kutoka Gambia, kuwa mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo, inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita. Kwa sasa Bensouda, mwenye miaka 50, ni naibu wa mwendesha mashtaka mkuu, Luis Moreno-Ocampo, ambaye anamaliza kipindi chake cha miaka tisa mwakani. Bensouda ameibuka kama chaguo la karibuni wanachama wote 120 wa mahakama hiyo, baada ya mgombea mwengine aliyekuwa akipewa nafasi kushikilia wadhifa huo, Jaji Mkuu* wa Tanzania Mohammed Chande Othman, kuondoa jina lake.
 
Aliondoaje jina wakati alikuwa anaungwa mkono na mkulu kuwa nchi itapata heshima kama angeipata ile kazi; ukweli nadhani upepo uliovuma haukuwa mzuri kwa jaji mkuu wetu na ikabidi to save face atoe jina lake!!
 
kwa nini aliondoa jina lake?

Intelligensia, aliambiwa hakuna mtu anamuunga mkono.

Habari nzuri kwa Tanzania, pamoja na kwamba ni vizuri kwa mtanzania mwenzetu kupeperusha bendera kwenye ofisi za kimataifa lakini huyu judge angetuletea balaa. Hapa nyumbani amekaa kimya wakati sheria zinakiukwa mahakama zinaendeshwa kwa utashi wa kisiasa. Ingekuwaje kama kesi ya marafiki zake ingepelekwa huko the Hague?
 
chande jina lenyewe limekaa kizoba zoba sana bana...chande ndo nini? aaagh mitanzania bana ..basi huyu angechaguliwa tungetengeneza noti yenye sura yake kumuenzi
 
Mataifa wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, yamekubali kumteua Fatou Bensouda kutoka Gambia, kuwa mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo, inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita. Kwa sasa Bensouda, mwenye miaka 50, ni naibu wa mwendesha mashtaka mkuu, Luis Moreno-Ocampo, ambaye anamaliza kipindi chake cha miaka tisa mwakani. Bensouda ameibuka kama chaguo la karibuni wanachama wote 120 wa mahakama hiyo, baada ya mgombea mwengine aliyekuwa akipewa nafasi kushikilia wadhifa huo, Jaji Mkuu* wa Tanzania Mohammed Chande Othman, kuondoa jina lake.

Hopefully, we will start seeing George Bush and the like being prosecuted at ICC
 
inawezekama vipi kujitoa mwenyewe? na kama alijua atajitoa kwanini aliingia kwenye kinyang'anyiro?
 
Hopefully, we will start seeing George Bush and the like being prosecuted at ICC

Mkuu Nyandaigobeko. Goerge Bush ilikuwa ni lazima atende hivyo. Naye kama angeogopa lawama kama watangulizi wake baada ya Reagan sijui leo hii Dunia ingekuwa na wababe wangapi?! Dunia yetuu ina watu,watawala wa nchi wa ajabu ajabu,wenye chuki za udini,rangi na mambo mengi ya hovyo. Jiulize kama watu walikuwa na uwezo wa kifedha kulipua ndege,balozi na maeneo ya biashara kwanini siku moja wasingelipua hata nyumba zetu za ibada kwasababu tu sisi wengine siyo wenzao,ni makafir?
 
Tusidanganywe kitoto hajajitoa amechemka,toka lini mbongo akajitoa kwenye boom?si unamwona Ngeleja hadi leo bado anaendesha wizara.
 
Mkuu Nyandaigobeko. Goerge Bush ilikuwa ni lazima atende hivyo. Naye kama angeogopa lawama kama watangulizi wake baada ya Reagan sijui leo hii Dunia ingekuwa na wababe wangapi?! Dunia yetuu ina watu,watawala wa nchi wa ajabu ajabu,wenye chuki za udini,rangi na mambo mengi ya hovyo. Jiulize kama watu walikuwa na uwezo wa kifedha kulipua ndege,balozi na maeneo ya biashara kwanini siku moja wasingelipua hata nyumba zetu za ibada kwasababu tu sisi wengine siyo wenzao,ni makafir?

Unaamini kuna hao unaoita "wababe"?!?

Realities can be constructed mkuu.

Hata kama wapo, je njia alizotumia Bush ndizo sahihi? Kulikua hakuna njia nyingine mpaka afanye abuses kama zile?!?!
 
Back
Top Bottom