Boflo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 4,384
- 4,409
Muafrika Kusini Atwaa Taji la Urembo wa Mashoga wa Dunia
Charl Van den BergMonday, February 15, 2010 12:40 AM
Mwanaume toka Afrika Kusini amefanikiwa kulitwaa taji la mashindano ya urembo wa mashoga wa dunia 'Mr Gay World Pageant' yaliyofanyika jana jumapili mjini Oslo nchini Norway.Charl Van den Berg, 28, shoga toka Afrika Kusini aliwafunika mashoga wenzake toka Australia, Hong Kong, China na Hispania na kutwaa taji la dunia la kumtafuta mwanaume shoga mrembo kuliko wote duniani kwa mwaka 2010.
Charl ambaye anaendesha mgahawa wa chakula mjini Cape Town nchini Afrika Kusini alitwaa taji hilo baada ya mashindano ya siku nne ya kuvaa mavazi mbalimbali yakiwemo mavazi ya kuogelea.
Taarifa ya waandaaji wa mashindano hayo ilisema kuwa dhumuni kubwa la mashindano haya ni kumtafuta mtu atakayekuwa kiongozi wao katika kutetea haki za mashoga duniani.
Xiaodai Muyi, 26, shoga toka China alishiriki na kushika nafasi ya nne katika mashindano hayo pamoja na hatua za China kumzuia asishiriki mashindano hayo.
Mamlaka za China ziliyapiga marufuku mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa China katika mashindano hayo.
Xiaodai aliingizwa kisiri kwenye mashindano hayo ambayo wanaume 20 toka nchi mbali mbali duniani walishiriki kumtafuta mrembo baina yao.
Ushoga ulikuwa ni kosa la jinai nchini China hadi mwaka 1997 wakati sheria zilipobadilishwa na kuwahesabu mashoga ni watu wenye matatizo ya akili.
Raia wa Australia Byron Adu, 25, alishika nafasi ya pili akifuatiwa na Rick Dean Twombley, 33, mcheza dansi toka Hong Kong aliyeshika nafasi ya tatu huku Mhispania Sergio Lara, 26, akishika nafasi ya tano.
Mashindano ya kwanza ya kumtafuta mrembo wa dunia wa mashoga yalifanyika mwaka jana nchini Kanada ambapo mwanaume toka Ireland alitwaa taji hilo.