MUAFRIKA anapojivua UAFRIKA wake kwa sababu ya dini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MUAFRIKA anapojivua UAFRIKA wake kwa sababu ya dini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakende, Oct 22, 2012.

 1. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Karibu katika uzi huu
  Nimekaa nikajaribu kufikiria, nikajaribu kusoma matukio mbalimbali yanayotokea Africa nikaona kweli Waafrika tuna safari ndefu.  Kwanini bara la Afrika linakumbwa na machafuko ya kidini kwa mfano, NIGERIA, MALI, SUDAN na sasa TANZANIA na KENYA. ninaposema mwafrika namaanisha mtu mweusi  Sababu kubwa ni kwamba Waafrica tumepoteza uafrica wetu, udugu wetu kwa sababu ya dini. Kabla ya ukoloni Africa ilikuwa neutral, yaani hatukuwa na dini hadi hapo Waarabu na Wazungu walipotuletea dini zao.

  Kimsingi kama kuna watu wanatakiwa na umoja basi ni Waafrika kwani tumeonewa sana, tukafanywa watumwa, na mpaka sasa bado tunadharauliwa kwa kutupiwa ndizi eti sisi ni nyani na hawa waliotuletea dini ambazo sasa zinatugombanisha.


  Ni jambo la ajabu kuona mwaafrika anapomuua mwafrika mwenzake, mwafrika hana historia ya kuishi maisha mazuri hata siku moja. Baada ya kung’atuka kwenye mikono ya wakoloni sasa anakabiliwa na wimbi la mauaji yanatosababishwa na dini, mfano polisi aliyeuawa pale zanzibar na wengineo huko NIGERIA, KENYA nk.

  Swali la kujiuliza,kwa sababu ya dini kwanini unaua mwafrika ambaye ni maskini mwenzako, mtumwa mwenzako ambaye kwa sasa anakabiliwa na wimbi la umasikini? Waafrika tusipoweka uafrika wetu na kuweka maslahi ya uafrika mbele na kusahau tulikotoka tutafia kubaya.

  Mfano Wanzazibar wanataka kuwatenga waafrika wenzao kwa sababu ya dini, yaani ili wajiunge na OIC kwa kuwa waafrika wenzao(Tanganyika) wamesema nchi haina dini sasa wanataka kujitenga kwa kuwa wanapata ugumu kujiunga na OIC


  Sikatai Waafrika kuwa na dini za nje bali tusitumie dini hizi kuuana kwami tayari tumeteswa vya kutosha na tunabaguliwa na hao weupe kuliko hata mbwa wa ulaya maana mbwa wao wanawatunza vizuri.  Kwa mfano kulikuwa na umuhimu gani wa kupigana kwa sababu ya Qaran wakati maliyekojolea Qaran ameisha kamatwa, kwanini Wakristo wachome Qauran eti kwa kuwa alieokoka ni mwislam?. Tusiuane kwa sababu ya dini maana wale waliotuletea hizo dini wanatuona wapumbavu.  Kwanini Waarabu na Wazungu wanaishi kwa amani wakati ngozi nyeusi ikiuana?


  Kimsingi wenzetu wana dini moja ambaya ni kubwa, mfano ukienda ulaya asilimia kubwa ni wakristo na uarabuni ni waislam.

  Hawa wenzetu hawatapigana kwa sababu ya kidini kwani dini moja kati ya hizi mbili (waislam na wakristu) ni dominant, mfano mwislam hawezi kwenda Uingereza na kuhoji kwanini nchi haitawaliwi kwa misingi ya dini?. Vivyo hivyo mkristo hawezi kwenda Saudí arabia akahoji kwanini wanawake hawaruhusiwi kuendesha gari?. Kwa hiyo wenzetu disturi yao ni moja tu, hawana ushindani wa kidini


  Ninapoangalia bara la Afrika na hizi dini za kuletewa nasikitika sana, asilimia kubwa ya Waafrika hawajaenda shule kwa hiyo ukichanganya na hizi dini walizoletewa, watu wazima tunakuwa kama (BIG BABIES)


  Kweli kama waafrika tukiweka mbele uafrika wetu na tukatumia mbinu nzuri kutatua matatizo yetu tutaendelea la sivyo tutatwangana matokeo yake MAREKANI akija kulinda amani tutajikuta madini yetu, mafuta yetu yanachukuliwa maana kipindi cha vita huwa hakuna anaweza kusimamia rasilimali.  Hivi kwanini umuue mwafriaka mwenzako ambaye miaka ya 1960 alikuwa mtumwa na mmeteseka wote? Kwa sababu ya dini, kwanini umuue mwafrika mwenzako ambaye anakabiliwa na umasikini wa kutupa, ambaye mavazi yake ni mitumba kutoka kwa weupe?, kwanini umuue mwafrika mwenzako ambaye anabaguliwa na hao waliomletea dini?, kwanini umuue mwafrika mwenzako ambaye hajui akiugua kama atapata matibabu?  Tuache ujinga, tutumie njia za amani kutatua migogoro ya kidini, mwache mwafrika mwenzako apumzike ameteseka kwa kuda mrefu. Wenzetu wana umoja ndiyo maana rais MUGABE alipoanza kuwatimua Zimbabwe wazungu wote walimuwekea vikwazo kwani wao wanaamini ni ndugu tofauti na sisi tunaowindana kwa sababu ya dini, tunafika hatua ya kaka na dada kutotembeleana eti kwa sababu ya mmoja alipoolewa alibadili dini, upumbavu  Sikatai dini, lakini tutumie njia za amani kutatua migogoro ya kidini, heshimu imani ya mwenzio kwani wewe umekuwa mwislam au mkristo kwa sababu ulikuta wazazi wako tayari ni waumini wa dini moja wapo, la sivyo hao weupe wataendelea kusema “AFRICAN ARE STUPID, GIVE THEM GUNS THEY WILL KILL THEMSELVES”

  That is what I see
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  I praise greeks.
   
 3. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mwanangu usishangae. Hayo ndiyo matunda ya ukoloni na kujikana. Tunapwakia mambo ya watu. Tunageuza vitu vya hovyo kuwa muhimu na vya muhimu kuwa hovyo. Nilidhani waswahili wangepandwa na hasira kuona mafisadi kama Edward Lowassa wanavyowahonga pesa walioyowaibia. Badala yake wako tayari kutoana roho kwa imani za kigeni ambazo msingi wake ni kuwagawana na kuwanyonya. Mie naamini Afrika ni sehemu takatifu kuliko huko jangwani watu wanapounguza pesa zao kwenda eti kuhiji kwenye makaburi na mawe wakati makaburi ya wazazi na babu zao yamejaa Afrika. Wanangu jifunzeni sasa nawaasa.
   
 4. mapugilo

  mapugilo Senior Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  You think great,support you
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ngozi nyeupe ikichafuka inakua nyeusi ukiisafisha vizuri inarudia uweupe wake...ngozi nyeusi ikichafuka inakua nyeusi ukiisafisha na sabuni, unga, dawa ukatumia mpaka na jiwe kukwangua uchafu bado ngozi nyeusi itabakia kua ngozi nyeusi hakutakua na mabadiliko yoyote... nadhani nimeshakujibu swali lako
   
 6. K

  KITENGE KOFIA Member

  #6
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 14, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shenz kabisa,,pumbavu,,,,,,,,,,,,,,,,,,wajinga wanatubagua halafu na sisi kwa ushenz wetu tunauana,sisi waafrika tuna shida gani?
   
 7. m

  magohe JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2012
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Niliwahi zungumzia suala hili kuwa dini hizi ni mapokeo kutoka huko ughaibuni.cha ajabu wengine wanauana au wanataka kuuana eti kisa dini kwa kuamini kuwa kufa ukitetea dini ni moja ya njia ya kupata thawabu kwa mungu.Swali ni mungu gani huyo anayependa watu wake kuuawa kwa unyama na ukatili wa kiasi hicho? kwa akili nyepesi haina hata haja ya kuumiza kichwa kujua kwa hali kama hiyo hapo hakuna hata chembe ndogo ya roho wa dini wa kweli ambao kwayo busara,huruma,unyenyekevu na upendo kwa wengine ni miongoni mwa mafundisho wajifunzayo kwa mujibu wa imani ya kweli na si kinyume chake .
  Akili ya kuambiwa changanya na yako!!
  kaka well spoken!!!!!!!
   
 8. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ktk masuala ya dini huwa sichangii sana kwa sababu nina imani ya kipekee, ngoja niwe msomaji tu wa huu uzi.
   
 9. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  gaddafi aliwaambia live kuwa uislam ni dini ya asili ya mwafrika.Na wengi tuu wanamini hivi bongo.
   
 10. Capital

  Capital JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,036
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Fikra nzuri. mambo tunayoyaona siyo ya leo, binaadam hususan wazungu wamefanya kampeni ya kummaliza mtu mweusi tokea miaka mingi sana, hata zaidi ya miaka elfu nne. nikumbushe machache: Afrika ni mahali palikuwa na kila kitu, na watu wake walikuwa wazuri sana na watu hawa, kulikuwepo rangi zao zilikuwa mchanganyiko, weusi kwa weupe (light). miaka mingi sana kabla, watu walikuwa wamehama toka barani humu na kwenda mabara mengine, wengine wakibadilika rangi na kuwa weupe zaidi, wengine walibakia na rangi zao (maeneo ya arabia, india na australia). waliobakia waliendelea na kazi huku wakijifunza ili kuelewa mazingira yao. kazi za uvumbuzi hazikuachwa nyuma, kuanzia kufua chuma, hisabati na unajimu. kulikuwa na dola kuu, hata kuliko ile ya Rumi. mtakumbuka yale mapiramidi na sphynx za egypt na sudan, na majengo makubwa ya mawe huko zimbabwe.

  katika karne ya tatu kwk, watu weupe waitwao assyrians, walivutiwa na maendeleo yaliyokuwa yamepatikana sehem kadhaa za afrika, hivyo walipenda kuja kujifunza. pamoja na ujuzi waliouona, walishangazwa na utajiri wa dhahabu na ustaarabu. waafrika kawaida ni watu soft hearted na huwa wanadhani watu wa rangi zingine wako kama wao. mbinu mbali mbali zilitumika ikiwemo vita. afrika ilipigana vita nyingi sana na wageni toka nje kuliko vita ya wenyewe kwa wenyewe. Wakati afrika imeharibiwa kabisa, madola makuu yameanguka, dola la Rumi likaibuka na zengwe la Yesu. dola hili lilishaanza kuwatoza ushuru watu wote katika maeneo waliyotwaa katika vita. kwa vile dola halikuwa na uwezo wa kufanya vita sehemu zote, ilifanyika soft war, kuwafanya watu wote wajikane, na silaha kali ktk vita hii ilikuwa ni dini. waafrika tumetozwa ushuru kwa njia ya sadaka na zaka tukidhani tunampa Mungu kumbe tunawapa washenzi na wezi. tumekuwa mabuda hadi tunakataana ili kumtukuza tumpaye sadaka.
   
 11. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Hapo ndipo nawapongeza wachina kwa kutoshadadia dini za kigeni angalia sasa maendeleo yao mpaka wamekuwa tishio kwa nchi za magharibi. Ebu fikiria idadi ya watu waliyokuwa nayo endapo wangeanza malumbano ya Yesu si Mungu au Mohamed si Mtume huo moto ungezimwa na nani iwapo mpaka leo Assad wa Syria anawaumiza vichwa watawala wa dunia.
  Kwa sababu hiyo taifa la Uchina limeweza kukaa bila vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu kujitosheleza kwa chakula mpaka kuuza chakula nje ya nchi,lakini kwa upande mwingine unakuta vinchi kama Zanzibar ambavyo hata kwenye ramani ya dunia ni kama vichunusi wanakimbizana mitaani kila kukicha kwa minajiri ya dini za kigeni.
  Kwa ufupi hizi dini ni kama zililetwa kutufarakanisha zaidi ya kutuunganisha na kibaya zaidi wanatubagua kwa rangi zetu
  .
   
 12. kamatembo

  kamatembo JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 538
  Trophy Points: 180
  dini ni upumbavu pumbavu fulani hv
   
 13. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hakuna sehemu iliyokuwa imechafuka kama kwa waarabu je wanapigania nini sasa dini au?Jiulize mbona wazungu mambo yao wanamaliza bila ya fujo.Mfano Scotland wanadai uvunjwe muungano na England wameamua kukubali kupitisha maoni kwa wananchi.Sasa kwanini nchi za kiafrika mpaka kwa kuchimbiana mikwara na virungu,maji ya washawasha,mabomu ya machozi na kamata kamata nyingi sanaaa.Jibu rahisi tu,serikali ikae na walalamikaji na kusuluhisha mambo na watu waendelee na kazi zao.Wanao sali kanisani wakasali,wanaosali misikitini wakasali,wanaosali kwenye masinagogi wakasali.Mbona wazungu wengi wanabadili dini na kuingia ktk uisilamu,hindu,sigh na mengineyo ambayo hawajazaliwa nayo.Binaadamu yupo huru kuamini akipendacho na hata yule asie amini vilevile yupo huru ilimraadi tu usimchokonoe mwenzako na imani yake.Utakuta humu mtu anaandika tena kwa kushangaa masuala ya imani tofauti na yake huwa najiuliza WHY? Kwanini usiandike ile unayoiamini kwakuwa utakuwa unaijua kwa marefu na mapana.Huwezi ukaijua dini ya mwenzako kama anavoijua anaeifuata.Hizo ndio chokochoko kwasababu ya kufuatilia au kuizungumzia dini ya mtu mwengine.Tuwe huru kujielezea na kuzipamba dini zetu na sio tuwe huru kutukana dini za wengine lazima tujue namna ya kuweka heshima kwa wengine.
   
 14. B

  BADO MMOJA JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 1,767
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Kaka wangepatikana watu kama mia hivi wenye akili kama zako tza tusingekuwa na migogoro kama iliyopo leo maana ukiangalia hata viongozi wetu wameshaangukia kwenye tope la dini ambazo sisi tumekuwa na uchungu kuliko hata walizileta maana unakuta mtu yuko tayari kufa eti kwa sababu dini yake imekashifiwa wakati wazungu wenyewe siku hizi hata huko kanisani wanakwenda wazee tu

  Hasa kwa mfano nchi ya Nethaerland (Uholanzi) nenda kanisani hakuna anayehangaika na dini kiasi cha kuvuruga uchumi wa nchi yake nenda Saudi bia zinanyweka kama kawaida na ndege ya mfalme wa Saudia inaendeshwa na kuhudumiwa na Makafiri wamarekani na Riyadhi pale kuna Military Base ya USA wanachukua watoto wakiarabu kama ilivyo Ulaya lakini leo wenzetu zenji wanachoma moto bar za ndugu zao jambo ambalo hata huyo Mtume S.A.W hakuagiza wala kufundisha hivyo haikutosha hiyo wamemtoa roho ndugu yao wa damu askari polisi yule kisa eti dini.

  Nakuunga mkono kaka hoja yako haiwezekani sisi tuwe na uchungu zaidi na hizo dini tulizoaminishwa kuliko hao waliozileta ni UNAFIKI NA UJINGA WA HALI YA JUU SANA TUBADILIKE WAAFRIKA. Jambo la kusikitisha dini imekuwa kikwazo hata watu kuoana japo wanapendana lakini wanatenganishwa na dini inauma sana matokeo yAKE MTU anaoa au kuolewa na mtu ambaye siyo chaguo lake na mwisho kutoa kizazi kibovu
   
 15. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2014
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mbona tayari umeisha changia hoja? Bora usingeandika chochote.
   
Loading...