Muafaka wa zanzibar waanza kuitafuna ccm

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
Miaka kadhaa imepita baada ya ule unaitwa 'muafaka' kati ya vyama viwili yaani ccm na cuf.
Nakubali kuwa hili lilikuwa ni jambo jema kwa amani ya nchi lakini mimi au wewe kama watanzania hatujui ni makubaliano gani yaliyopelekea muafaka huu.
Inawezekana ccm iliingia 'muafaka' na cuf kwa lengo moja tu,yaani kuendelea kubaki madarakani !kwa upande wa cuf pamoja na sisi kuwabeza sana inawezekana waliingia makubaliano haya wakiwa na malengo ya mbali,ambayo kwa sasa wameanza kuyafaidi.

Nikijaribu kufuatilia kauli na mwenendo wa viongozi wa cuf zanzibar hasa maalim seif nachelea kusema kuwa wana nia thabiti ya kuuvunja muungano na kuhakikisha zanzibar ni taifa huru.

Kama ccm hawakujua hili basi wameumia sana kwani cuf wamedhamiria kusukuma hoja yao hasa ukizingatia wao ni sehemu ya SMZ.

Nampongeza maalim seif kwa kumuingiza kingi makamba!
Ccm wamenasa kwenye tope zito na hawana njia ya kujinasua.
 
Nianavyo mimi kwenye issue ya kuvunja muungano cuf wanatumiwa na viongozi wa ccm zanzibar, kwamba wako pamoja kwenye madai ya kujitenga. Kama ccm hawana mkono kwenye huu msukumo, basi tungetegemea haya yanayoitwa maridhiano yavunjwe, maana seif yuko serikalini, sina hakika aliposimama jukwaani alisimama kama kiongozi wa serikali au kiongozi wa chama maana mkutano haukuwa wa cuf bali ulikuwa wa wazanzibar.
 
Ipo hadithi kwamba, Moi alipoona Raila anamtesa kisiasa akamkaribisha kwenye chama chake cha KANU. Hali hiyo ilifananishwa na mtu aliemchukua mtoto wa TEMBO akamweka chumbani kupitia mlango mdogo wa ile nyumba na kumlisha majani na chakula cha kila aina. Tembo mtoto aliendelea kunywa na kula na kisha akaongezeka akawa mkubwa wakati mwenye nyumba akili yake alidhani bado ni tembo mtoto tu. Baadaye tembo yule alianza kuona chumba chake ni kidogo na ule mlango alioingilia sasa ni mdogo na alitamani kuona uko nje kukoje. Ndipo siku moja mwenye nyumba hakuyaamini macho yake alipoona nyumba inaanguka yote ilimradi Tembo atoke.

Maalimu Seif ni Tembo aliyekwisha komaa na sasa anataka kutoka sasa CCM wajipange ndo nyumba yao inabomoka hivyo, mwanzoni walitamba kwamba CUF sasa imekwisha kwa vile Seif alikuwa anataka ujiko wa Ving'ora na msafara kweli anao lakini mwenzao sasa kapata fursa ya kuwashawishi CCM Zanzibar nao wamegundua kuwa CCM bara ndo mkoloni ambaye amewanyima UHURU na nchi yao waliyoidai jana kwa zidi ya miaka 50 sasa.

Swali la msingi sasa CCM itafanyaje maana yafuatayo ni dhahiri kwao,
1. Upande huu CHADEMA inamtesa na operation Sangara na M4C
2. hUKU mBIO za Urais 2015
3. Pesa za Uswsiss
4. Katiba mpya ambayo haikuwa ajenda yao kwenye ilani yao
6. Ujio wa Rais wa China, na Obama wiki chache zijazo
7. Suala la gesi asilia
8. Utekaji, uteswaji wa watu maarufu
9. Kufeli kwa watoto wa kidato cha nne
10. Mawaziri hawawajibiki sawasawa
11. Ziara kibao za nje za Mh. JK
12. Nape, Kinana na Mwigulu na Mwampamba
13. Mang'ula na single ya waliotoa rushwa nk
14. Warioba na Tume ya Katiba Mpya

Orodha haiwezi kuisha ila endelea kutafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Seif c mara ya kwanza kuwemo kwenye serekali ya ccm zanzibar,pale mwanzo walimfukuza kwa ccm mwenzao lakini kwa sasa haiwezekani kumfukuza coz kaingia na tiketi ya cuf na yupo pale kwenye serekali kisheria,sasa naanza kuamini wazbr wapo juu kisiasa kuliko watanganyika.
 
Seif c mara ya kwanza kuwemo kwenye serekali ya ccm zanzibar,pale mwanzo walimfukuza kwa ccm mwenzao lakini kwa sasa haiwezekani kumfukuza coz kaingia na tiketi ya cuf na yupo pale kwenye serekali kisheria,sasa naanza kuamini wazbr wapo juu kisiasa kuliko watanganyika.
Hilo ni wazi kwamba ni hitaji la zanzibar yote kama taifa ila maalimu seif asiue viongozi wa dini kama agenda ya kuvunja muungano...tunajua kwamba Ccm sio chama cha wenye akili kama zamani ila ni genge la mafisadi na wasio na akili hata kidogo so halahala kuhusu dini maana dini haina mipaka hao wakristo huko zenji waliingia na ukristo wao na hao waislamu walislimishwa na sultani wakiwa hapo zanzibar hivyo hakuna dini mwenyeji wa zanzibar mkijaribu kuumiza wengine kwa sababu ni wachache basi tegemeeni kukosa amani milele yote..
 
Hilo ni wazi kwamba ni hitaji la zanzibar yote kama taifa ila maalimu seif asiue viongozi wa dini kama agenda ya kuvunja muungano...tunajua kwamba Ccm sio chama cha wenye akili kama zamani ila ni genge la mafisadi na wasio na akili hata kidogo so halahala kuhusu dini maana dini haina mipaka hao wakristo huko zenji waliingia na ukristo wao na hao waislamu walislimishwa na sultani wakiwa hapo zanzibar hivyo hakuna dini mwenyeji wa zanzibar mkijaribu kuumiza wengine kwa sababu ni wachache basi tegemeeni kukosa amani milele yote..

ukiandika tumia akili na mkono sio miguu na makalio. utaleta machafuko nchini ukiendelea na pumba zako. eti sultan ameslimisha watu zanzibar
 
ccm na serikali imejikuta katika wakati mgumu kwani kumnyamazisha seif ni ngumu kwa kuwa ni 'rais' wa zanzibar.
 
Swala la muungano si swala la chama cha siasa hivyo kudai ccm yanawatokea puani kwa Zanzibar kutaka kujitenga si sahihi. kama watanzania tunafaidika na muungano basi zanzibari kujitenga yanakuwa yametutokea puani sisi watanzania. kama ingekuwa kwamba ccm kuikaribisha cuf katika serikali huko Zanzibar kumeiimarisha cuf kisiasa kiasi cha kutishia kuiondoa ccm madarakani basi hiyo ingekuwa hoja inayokubalika kuwa ccm yanawatokea puani. sioni haja ya kuibana Zanzibar ingawa vilevile sioni haja kuwaruhusu viongozi wachache watuvuruge. tunategemea kwenye katiba mya tuundiwe mfumo wa utawala ambao utatuimarisha zaidi.
 
Back
Top Bottom