Muafaka wa kitaifa ni lazima kwa tulipifikia

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,601
8,741
Kwa tulipofikia muafaka wa kitaifa sio matakwa ya chama chochote au hata Rais ni kitu cha lazima kama ilivyokuwa Zanzibar.

Zanzibar muafaka haujaja mpaka watu wamekufa hii ni kwasababu njia zote za kutisha mpaka kuuwa hazijafanikiwa hivyo sio hiari ni lazima ingekuwa hivyo au kuwa na vita vya wenyewe

Huku Bara tumeshafikia hapo vyama havina wabunge, ruzuku na wamezuiwa mikutano ya wazi kwa miaka! Lakini bado wapo na nguvu ileile . Pamoja na watu kipigwa risasi na kufugwa bado kuna watu tena wengi tu ambao wanaunga mkono hivi vyama.

Ushauri wangu ni kwamba ni bora mijadala ifanyike sasa badala ya kusubiri watu wafe kama Zanzibar halafu ndiyo tuwe na muafaka. Tusiwe kama kenya au ndugu zetu wa Zanzibar. Upinzani inaekea umesha komaa kiasi cha kwenda huko ingawa tofauti na Zanzibar huku bara ni 30% wakati Zanzibar walikuwa kama 55% ya watu wote. Lakini hii 30% ni imara sana nashauri muafaka kufanyika sasa hivi jeshi na Polisi itaishia kulekule kwa Magu ambako ni bure.

webmaster nisaidie kubadilisha typo hapo “tulipofika” mambo ya simu haya
 
Back
Top Bottom