Muafaka Wa Kenya, Wa Zenji Je?

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
It is interesting to hear and see that our 2 Presidents Mkapa na Kikwete have devouted so much of their time, energy and efforts using our tax money to have Kibaki and Raila agree to have Serikali ya Mseto.

One may sit down and wonder; it is now 2 years since Kikwete promised to find Muafaka on Zanzibar, kukutanisha Sefu na Karume. Why were Mkapa and Kikwete quick to their feet to resolve Kenya crisis, while they are continuosly for the past 12 years playing blind eye to Zanzibar/Pemba division that is a threat to Muungano and new bloodshed if we were to have elections even tomorrow?

Can they take a lesson from what happened in Kenya for the last 90 days to make sure that we are resolving issues at home front before we send both of them to Bashir or Mugabe?

I am glad they were able to have Raila and Kibaki to come to terms and agree on powersharing.
 
Rais Kikwete na Rais Mstaafu Mkapa hongereni kwa kusaidia muafaka wa jirani zetu Kenya kufanikiwa ktk kipindi cha siku 60!! kwa kweli sikutegemea kabisa kama mungeweza kusaidia juhudi hizo kushika kasi kwa kipindi hicho kifupi! kwani nikikumbuka muafaka wa wananchi wenzetu Zanzibar unaofikia miaka 12 sasa tena ktk kisiwa kidogo kama hicho nashindwa kuelewa!

Mimi sasa nakaribia kuamini kuwa huwenda sababu na uwezo wa kusaidia muafaka wa Zenji ufanikiwe tunao ila nia ndio hatuna!
 
Hivi Zanzibar kuna tatizo gani hadi wahitaji muafaka kama wa Kenya? Au ni muafaka wa kuanza kulipia umeme?
 
Kadogoo umesahau kuwa "Kinyozi hajinyoi" na "Mganga hajigangi"? Hebu tembelea nyumbani kwa fundi seremala akuoneshe fenicha zilizoko sebuleni kwake!
 
Hivi Zanzibar kuna tatizo gani hadi wahitaji muafaka kama wa Kenya? Au ni muafaka wa kuanza kulipia umeme?

Mimi nimelelewa na nimefundishwa kuheshimu wakubwa - na Mkuu wewe ni Senior kwangu katika JF, lakini naona unatoa point utumbo au ndio unafurahisha Ukumbi?

Tueleze kweli huelewi tatizo la Zanzibar, kwa kuthibitisha kuwa hakuna tatizo.
 
Hivi Zanzibar kuna tatizo gani hadi wahitaji muafaka kama wa Kenya? Au ni muafaka wa kuanza kulipia umeme?

Unaenda kinyume na Mwenyekiti wako wa Chama(Sisim) ambaye anakiri kuwa Znz kuna tatizo ( hotuba yake aloitoa bungeni)
 
Kadogoo umesahau kuwa "Kinyozi hajinyoi" na "Mganga hajigangi"? Hebu tembelea nyumbani kwa fundi seremala akuoneshe fenicha zilizoko sebuleni kwake!

Ndio misemo inayoturejesha nyuma na hutumika pale panapokuwa hapana hoja au dharau - Haraka haraka haina baraka, Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza( wakati watu wanatumia mamilionikutangaza bidhaa zao.

Hili ni la Zanzibar hakuna anayejali kwani walipouliwa watu kule nani alipiga kelele lakini vurugu za juzi Kenya wasomi wa chuo kikuu walitaka kufanya maandamano na mifano ni mingi tu, mmoja wapo ni huu wa hii thread hata uchangiaji wake ni mdogo kuna nini?
 
Rais Kikwete na Rais Mstaafu Mkapa hongereni kwa kusaidia muafaka wa jirani zetu Kenya kufanikiwa ktk kipindi cha siku 60!! kwa kweli sikutegemea kabisa kama mungeweza kusaidia juhudi hizo kushika kasi kwa kipindi hicho kifupi! kwani nikikumbuka muafaka wa wananchi wenzetu Zanzibar unaofikia miaka 12 sasa tena ktk kisiwa kidogo kama hicho nashindwa kuelewa!

Mimi sasa nakaribia kuamini kuwa huwenda sababu na uwezo wa kusaidia muafaka wa Zenji ufanikiwe tunao ila nia ndio hatuna!

Walienda kushuhudia mwafaka ukiwekwa kama majirani,usiwape vichwa bila sababu.

Wao kama viongozi wa SISIEMU ni sehemu ya tatizo. Wao wajinga wakate tawi wakiwa bado wamelikalia?

Ushindi wa vyama vya upinzani ndiyo utakao maliza tatizo la Zanzibar.
 
Walienda kushuhudia mwafaka ukiwekwa kama majirani,usiwape vichwa bila sababu.

Wao kama viongozi wa SISIEMU ni sehemu ya tatizo. Wao wajinga wakate tawi wakiwa bado wamelikalia?

Ushindi wa vyama vya upinzani ndiyo utakao maliza tatizo la Zanzibar.

Na kama hili wanalijua Wapinzani basi wangeelekeza nguvu zao zote Znz na kuhakikisha ushindi unapatikana, kwani ingalisaidia kuonyesha wananchi ni jinsi gani wapinzani wanatawala - kama wataboronga basi ndio wameshaua upinzani na kama watafanya vizuri basi itakuwa chachu ya kuingoa CCM na huku Bara.( Anyway nitaandikia thread hii kwa upana bado nakusanya mawazo)
 
CUF ndo wasanii kwani kwani kama wangekuwa serious kama ODM hali ya Zanzibar ingekuwa shwari na KARUME angekuwa waziri kiongozi labda. Zanzibar matatizo yataendelea kuwepo kwasababu watanzania tunajiona hatuna tatizo kumbe haki za binadamu haziheshimiwi.
 
Ili Zanzibar kuwe shwali basi tuwaachie wapastane wenyewe!!
Bara tunawavuruga hawataki Wao wanapenda wafikie muafaka wenyewe
tofauti na hivyo hawatapatana milele.
 
Mods,

Naomba muunganishe ile thread yangu ya Effort Muafaka na hii hapa maana zina shabihiana!
 
CUF ndo wasanii kwani kwani kama wangekuwa serious kama ODM hali ya Zanzibar ingekuwa shwari na KARUME angekuwa waziri kiongozi labda. Zanzibar matatizo yataendelea kuwepo kwasababu watanzania tunajiona hatuna tatizo kumbe haki za binadamu haziheshimiwi.

Hapa nakubaliana na wewe mzee, hao jamaa usanii umewazidi lakini kama WTZ wenzetu hatuna budi kuwasaidia na kuwaonyesha njia, ingawa inatakiwa wajitahidi kwanza - watu wanasema - mshikemshike na mwenyewe uko nyuma.
 
So Karume is still yo yo ing the Muafaka? what will Kikwete say?


jumanne, 11 Machi 2008 CUF yatoa kauli


na Saada Said, Zanzibar


SIKU chache baada ya kuibuka kwa taarifa kuwa Rais Amani Abeid Karume, amekataa mapendekezo ya kuundwa kwa serikali ya pamoja visiwani humo, iliyotolewa na kamati inayosimamia mazungumzo ya kusaka muafaka wa kisiasa, Chama cha Wananchi (CUF) kimetoa kauli rasmi kumpinga Rais Karume.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya chama hicho iliyokutana kisiwani hapa jana, na kujadili ripoti ya maendeleo ya mazungumzo ya muafakaa, ilisema baada ya kikao chake kuwa iwapo ni mstaarabu, Rais Karume anapaswa kukubaliana na mapendekezo ya kamati ya muafaka.
Hata hivyo, kamati hiyo ilikwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa hata kama atakataa, Rais Karume anapaswa kutambua kuwa yeye si mmoja wa wajumbe wa kamati ya muafaka, hivyo hana uwezo wowote wa kukwamisha mazungumzo yanayoendelea kati ya chama hicho na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Mazsons mjini hapa, Makamu Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali, alisema mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa mpasuko wa kisiasa uliopo Zanzibar ni ya Watanzania wote na si ya CUF wala ya CCM.
Alisema kwa maana hiyo, mazungumzo hayo yanamgusa kila Mtanzania.
“Kama Rais Karume atakuwa mstaarabu, basi atakubaliana na maamuzi, kwa sababu wajumbe wote watakuwa wameamua na wengine wanatoka ndani ya chama chake… ni maamuzi ya pamoja kwa manufaa ya taifa,” alisema Machano ambaye alikaimu Uenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya CUF kutokana na kutokuwepo kwa Ibrahim Lipumba, ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo na chama hicho.
Alimkumbusha Rais Karume kuwa uamuzi wa kukaa katika meza ya mazungumzo ni wa busara na ni ustaarabu unaofuatwa na nchi nyingi dunaini zinazotatua matatizo yao kidiplomasia.
Alisema machafuko yaliyotokea Kenya ni tofauti na ya Zanzibar, kwa kuwa Kenya ilifikia hatua ya mauaji kabla hawajakaa kuzungumza, wakati Zanzibar wameamua kuanza mazungumzo kabla hali haijawa mbaya, ingawa kinachozungumzwa kimekuwa kikijirudia kila mara.
Alisema kwa kukubali kukaa mezani na kuzungumza, CUF haijashindwa katika harakati za kusaka haki, bali ni ustaarabu utakaosaidia kumaliza uhasama na migogoro iliyopo kwa njia ya mazungumzo bila ya kupigana na kumwaga damu kama inavyofanyika nchi nyingine.
Akizungumzia hatua iliyofikiwa, alisema kuwa hakutakuwa na haja tena na kuendeleza mazungumzo baada ya maafikiano, bali utekelezaji wa kile kilichoafikiwa katika vikao.
“Katika mazungumzo sasa tumefikia tamati, kilichobaki ni utekelezaji wa makubaliano, hivi sasa tunataka Baraza Kuu la Uongozi litoe maamuzi ya mwisho kwa upande wa CUF,” alisema Machano.
Alisema CUF wameamua kuitisha kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama, ili kupata ufafanuzi juu ya mwenendo mzima wa mazungumzo yalipofikiwa, ikizingatiwa kwamba sasa ni miezi 14 tangu kuanza kwa mazungumzo hayo.
“Sisi tumeridhika na mazungumzo, tunahitaji kuyabainisha yale tuliyokubaliana, ila tu la msingi tunahimiza subira na kuwaomba wananchi wawe watulivu katika kipindi hiki kifupi kilichobakia kabla ya kupokea taarifa ya mwisho ya mazungumzo haya,” alifafanua.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Taifa ya CUF imeagiza rasmi kwamba taarifa hiyo kamili ya mazungumzo ifikishwe mbele ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa katika kikao chake cha Machi 17 mwaka huu, ili kupata maamuzi ya mwisho ya chama hicho.
Hatua hii ya sasa inakuja baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama kuibana Kamati ya Kutafuta Muafaka ya chama, kubainisha kile kilichoafikiwa katika mazungumzo hayo.
Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, alisema Rais Kikwete alikuwa karibu na mazungumzo ya muafaka baada ya kuombwa na chama chake kutokana na kusuasua kwa mazungumzo hayo.
Maalim Seif alitoa kauli hiyo baada ya kutakiwa na waandishi wa habari kubainisha ushiriki wa Rais Kikwete katika mazungumzo hayo, hasa baada ya kufanikiwa kwa juhudi zake za kupatanisha mahasimu nchini Kenya.
“Rais Kikwete alikuwa karibu kwa kiasi fulani na ndiyo maana tukafikia hapa tulipofikia, kweli tulimuomba awe karibu yetu na amekuwa karibu kwa kupitia kwa wajumbe wa chama chake kumuarifu kila kinachojadiliwa katika mazungumzo,” alisema Maalim Seif.
Maalim Seif alisema ni kweli walilazimika kumuomba Rais Kikwete baada ya kuona mazungumzo hayo yanasita sita. Hata hivyo, hali hiyo ilisababishwa na uchaguzi ndani ya CCM, kwani kuna masuala ambayo yalihitaji maamuzi ya kisiasa kutoka ngazi za juu, hivyo CCM waliomba wapewe muda kupisha uchaguzi wao.
Kati ya mambo yaliyojadiliwa katika mazungumzo hayo ni pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2005 na tathmini zake, usawa na haki katika uendeshaji wa siasa, utawala wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, njia za kuimarisha mazingira ya maelewano na uendeshaji wa uchaguzi huru na wa haki Zanzibar, pamoja na utaratibu wa utekelezaji na programu ya utekelezaji wa makubaliano yatakayofikiwa. Kamati ya Ulinzi na Usalama ya CUF imearifu kupokea na kuridhishwa na taarifa ya mazungumzo kati ya CCM na CUF, ikihusu ajenda hizo tano za msingi. Wakati huo huo, Kamati Kuu ya CCM imepanga kukutana leo jijini Dar es Salaam na inaaminika kuwa moja kati ya mambo yatakayojadiliwa ni maendeleo ya mazungumzo hayo ya muafaka.
 
Back
Top Bottom