Muafaka: Uamuzi wa CCM Butiama wafananishwa na ufisadi wa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,004
Posted Date::4/1/2008

Muafaka: Uamuzi wa CCM Butiama wafananishwa na ufisadi wa kisiasa

*Wasomi wasema utachochea uhasama

*Warioba asema ana mashaka na kura za maoni

*Awataka viongozi kuacha kukwepa wajibu wao

*CUF wataka mataifa ya nje yaiokoe Z'bar

Waandishi Wetu
Mwananchi

TAMKO la Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), kuhusu hatima ya Mwafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar, limezua mapya, baada ya wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chama cha Wananchi (CUF), kuliita kuwa ni ufisadi na usanii wa kisiasa.

Kauli hiyo ilitolewa kwa nyakati tofauti na baadhi ya wahadhiri wa UDSM waliozungumza na Mwananchi na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alipozungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu chama hicho, jijini Dar es Salaam jana.

Wakati wasomi na CUF wakitoa maoni yao, Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Joseph Sinde Warioba aliiambia Mwananchi jana kuwa uamuzi wa CCM kuamua kuendesha kura za maoni utazidi kuwagawa Wazanzibari badala ya kuwaunganisha.

Wahadhiri hao, Maalim Seif na Jaji Warioba walitoa kauli hiyo kufuatia tamko la NEC juu ya suala la Mwafaka lililotolewa juzi baada ya kuhitimisha kikao chake katika Kijiji cha Butiama, mkoani Mara, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo ilitaka ifanyike kura ya maoni visiwani Zanzibar ili kupata ridhaa ya wananchi kuhusu kuundwa kwa serikali ya mseto visiwani humo.

Warioba alisema kwamba suala la maamuzi wa serikali ya mseto liko ndani ya viongozi na kwamba wasikwepe majukumu yao." Suala la kutekeleza Mwafaka liko ndani ya uongozi, hivyo wasikwepe wajibu wao," alisema.

Alisema kimsingi hana matatizo kama viongozi wana nia ya kuboresha mchakato wa Mwafaka, lakini ana wasiwasi kwamba mchakato huo ukifika hadi wakati wa uchaguzi unaweza usiwe na maana inayokusudiwa.

"Matatizo ya Zanzibar yanatokana na uchaguzi, hivyo hayawezi kutatuliwa kwa uchaguzi," alisisitiza Jaji Warioba.

Warioba alitoa mfano wa Chama cha ANC cha Afrika Kusini ambacho kilishinda kwa wingi wa kura, lakini kikashirikisha vyama vingine kwa lengo la kuunganisha wananchi. "Vyama vikiungana kwa mtindo wa serikali ya mseto, hata wananchi pia wataungana," alisema.

Alisema mfano mzuri ni visiwani Zanzibar ambapo kabla ya viongozi wa CUF na CCM kuanza mazungumzo ya kuleta Mwafaka visiwani humo, wananchi walikuwa hawazikani kwa sababu za kiitikadi, lakini viongozi wao walipoanza kuzungumza na wananchi nao walipunguza chuki baina yao.

Profesa Mwesiga Baregu wa Sayansi ya Jamii, Idara ya Siasa ya UDSM, alisema kitendo cha CCM kutaka suala la Mwafaka kupigiwa kura ya maoni na wananchi baada ya kukaa nalo kwa miaka miwili sasa, ni uhuni unaoweza kulipeleka taifa katika migogoro.

CCM wanafanya uhuni na huu ni mchezo mbaya sana kwa sababu yaliyoharibika Kenya yalitokana na wananchi kukosa imani na serikali kutokana na uhuni wa aina hiyo,? alisema Profesa Baregu.

Alisema tabia ya Serikali ya CCM kuanzisha michakato mizito ya kitaifa na kufanya ghiliba za makusudi kisha kuiacha kwenye utata, ni ufisadi wa kisiasa na hatari kwa uhai wake na maendeleo ya taifa.

Tofauti na ufisadi wa uchumi ambao bado unazungumzwa, kitendo hicho ni ufisadi wa kisiasa na kama serikali haisimamii haki, haistahili kuaminiwa wala kuheshimika na matokeo hayo yote ni watu kuchukua sheria mkononi,? alisema.

Alisema uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM kurudisha mjadala wa mwafaka kwa Wananchi wa Zanzibar wakati wajumbe wake ni viongozi wa CUF na CCM Taifa ni ujanja wa kuukataa mwafaka.

Uamuzi huo unaondoa imani na dhamira njema ya CCM kuhusu mwafaka. Kwa nini hatima ya mazungumzo hayo yakafanywe na Wazanzibari tu wakati walioshiriki ni makatibu Wakuu wa vyama vyenye wanachama Bara na Zanzibar?? alihoji Baregu.

Profesa Baregu alisema kama kuna umuhimu kura za maoni ziendeshwe kuhusiana na kutungwa kwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar badala ya kupoteza fedha nyingi kuendesha kura za maoni kuhusu mwafaka tena katika mazingira ambayo jamii inafahamu kuwa CCM inaukataa.

Profesa mwingine wa kitivo hicho, Ernest Mallya alisema uamuzi wa CCM kutaka hatma ya mwafaka kuamriwa na wananchi wa Zanzibar kwa kura za maoni, ni ishara kuwa hawakuwa na nia thabiti kuutafuta.

Alisema kura za maoni haziwezi kutoa mwelekeo unaotarajiwa kuhusu mwafaka badala yake zitaongeza uhasama baina ya pande mbili zinazovutana kuhusu suala hilo.

Kura ya maoni ni uchaguzi ambao ni wazi CCM itashinda kwa mbinu zilezile wanazotumia kushinda chaguzi zingine. Hiki ni kigezo ambacho chama hicho kinataka kukitumia kuukataa na CUF wasikubali, wakatae,? alisema Profesa Mallya.

Profesa Mallya alitaka CCM kuanzisha mchakato wa kura za maoni katika kero zote za muungano kama ina nia njema na taifa badala ya kukazania kura za maoni kuhusu mwafaka ambazo tayari imejiandalia ushindi wa kuukataa.

Kauli ya Profesa Mallya iliungwa mkono na Mhadhiri Msaidizi wa idara hiyo Bashiru Ally aliyesema kuwa kura za maoni haziwezi kuleta mwafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Alisema kama suala hilo limeshindwa kufikia tamati katika mikutano ya viongozi wa vyama viwili vinavyopingana, halitaweza pia kukamilika kwa kura za maoni kwani kura ndizo zilizokuwa chanzo cha mgogoro huo.

Alieleza kuwa utaratibu wa kura za maoni hauna tofauti na kampeni za Uchaguzi Mkuu unaowagawa watu katika makundi mawili yanavutana na kuongeza mgogoro badala ya suhulisho.

Ally alisema hakuna maana nyingine zaidi ya ?danganya toto? kuanzisha mchakato wa kura za maoni kuhusu mwafaka wakati kuna matatizo mengi ya kitaifa yanayotakiwa kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Kwa nini tutumie fedha kuwauliza wananchi kuhusu mwafaka na kuacha mambo ya msingi kama matatizo ya ardhi, madini, uraia na maeneo mengine yenye utata kama siyo kuvuta subiri na kuwadanganya wenzao wa CUF alihoji.

Kuwauliza wananchi kuhusu mwafaka ni kuongeza chumvi kwenye kidonda, kwani hadi sasa Watanzania bado hawajajua hatima ya wizi wa EPA na kamati za madini, alisema.

Mhadhiri wa sheria chuoni hapo, Dk Sengondo Mvungi alisema matumizi ya rasilimali za umma katika mpango wa kupata kura za maoni ni aina nyingine ya ufisadi katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

Alisema hakuna sababu za msingi kuitisha kura za maoni kuhusu serikali ya mseto visiwani Zanzibar wakati Katiba haikatazi.

Tunawauliza wananchi ili watupe majibu gani kuhusu serikali ya mseto wakati tayari Katiba haipingani nayo?? Kama watafanya na wakatumia fedha za umma tutawapigie kelele kwani huo ni ufisadi, alisema

Dk Mvungi alisema kuitisha kura za maoni sio kosa na inaruhusiwa kikatiba, alibainisha kuwa matumizi ya rasilimali za umma katika mambo binafsi ya wanasiasa ni kosa kisheria.

Mhadhiri Msaidizi wa kitivo hicho cha sheria, Makarios Tairo alisema kura za maoni VIsiwani Zanzibar zisiendeshwe kwa ajili ya mwafaka bali ziendeshwe kwa upana zaidi kulinda maslahi ya Wazanzibari na Watanzania wote.

Alisema historia inaonyesha kuwa tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi visiwani Zanzibar vyama vya CUF na CCM vimekuwa vikishindana kwa tofauti ndogo ya kura jambo ambalo linaleta umuhimu wa kuwa na serikali ya mseto baina ya vyama hivyo viwili.

Wakati wahadhiri hao wakisema hayo, CUF, imepinga hoja ya CCM ya kutaka ifanyike kura ya maoni Zanzibar ili kupata ridhaa ya wananchi ya ama iundwe au isiundwe serikali ya mseto visiwani humo.

Badala yake, CUF imeitaka CCM kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya Vyama hivyo, ikiwa ni pamoja na kutia saini makubaliano hayo na kuyatekeleza mara moja.

Katika mazungumzo yao yaliyochukua takriban miezi 14 na vikao 21, pamoja na mambo mengine, CUF ilidai kuwa walikubaliana na CCM kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, maarufu kama "serikali ya mseto" itakayoshirikisha pande mbili za vyama hivyo.

Mbali na hilo, CUF pia imepinga hoja ya kufanywa kwa marekebisho katika baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Mazungumzo ya Vyama hivyo, ambayo CCM imeiagiza kamati yake kukutana na wajumbe wa CUF ili kujadili mapendekezo hayo.

Katika tamko lake lilisomwa na Maalim Seif jana, CUF imesema hoja hizo ni usanii wa kisiasa, ubabaishaji na upotoshaji uliofanywa na CCM kwa lengo la ama kuendelea kurefusha muda hadi mwaka 2010 au kuyakataa makubaliano ambayo wajumbe wake wameshiriki kuyaandaa katika miezi 14 ya mazungumzo kati ya vyama hivyo.

"Kwa msingi huo CUF haikubaliani na hoja hizo zote mbili," alisema Maalim Seif.

Maalim Seif alisema kinachosikitisha zaidi ni kuwa tofauti na ilivyoelekezwa, pendekezo la kutaka kura ya maoni, halikuwa limeibuliwa na wajumbe wa NEC, bali lilikuwamo katika taarifa ya Kamati ya CCM inayoshiriki mazungumzo, likiwa ni pendekezo walilotaka liridhiwe na Kamati Kuu (CC) ya NEC.

"Hivyo, ni wazi liliandaliwa mapema kutokana na kile kamati hiyo ya CCM ilichokiita 'kuipiku CUF katika ubunifu wa kujenga'," alisema Maalim Seif.

Alisema kitendo cha Kamati ya CCM kuwasilisha kitu kipya nje ya makubaliano yaliyofikiwa, ni upotoshaji mkubwa wenye lengo la kulifanyia usanii wa kisiasa suala kubwa linalogusa maslahi ya taifa na watu wake moja kwa moja.

Alihoji kama pendekezo la kura ya maoni lina nia njema ya kuwashirikisha wananchi, kwa nini wajumbe wa Kamati ya CCM wasiliwasilishe katika vikao vya mazungumzo na badala yake wakaamua kuliingiza kama mtego wa kisiasa wenye lengo la kuipiku CUF

Maalim Seif pia alihoji iwapo kura ya maoni itaendeshwa na chombo kipi na kwa utaratibu upi, hasa ikitiliwa maanani tayari CCM na CUF wamekubaliana kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Daftari la Kudumu la Wapigakura, vina matatizo ya msingi ambayo yanahitaji kurekebishwa

"Ni vipi basi tume hiyo chini ya daftari bovu lililopo itaweza kuendesha kura ya maoni ambayo itakuwa huru na ya haki?," alisema Maalim Seif na kuongeza:

"Sisi tunaona suala hilo ni mbinu chafu yenye lengo la kuendelea kupoteza muda ili makubaliano yaliyofikiwa yasiweze kutiwa saini na utekelezaji kuanza. Kwa lugha yao CCM waliyoandika katika waraka wao ni njia ya kuipiku CUF na kamwe haikusudiwi kupata maoni ya wananchi".

Kuhusu marekebisho katika baadhi ya mapendekezo ya Kamati ya Mazungumzo ya Vyama hivyo ambayo CCM imeiagiza kamati yake kukutana na wajumbe wa CUF kujadili mapendekezo hayo, Maalim Seif alisema hawaungi mkono suala hilo kwa kuwa CCM haijataja ni maeneo gani inataka yafanyiwe marekebisho.

Alisema hoja hiyo inashangaza kwa sababu wajumbe wa Kamati ya Mazungumzo kutoka CCM, walikuwa wakiwaarifu wajumbe kutoka CUF kwamba, walikuwa wakiwasilisha taarifa kwa kila hatua inayofikiwa katika vikao vya CC na NEC na kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na kupata maelekezo na miongozo inayohitajika.

"Hata taarifa ya karibuni kabisa ya CCM iliyokuwa ikikanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba mheshimiwa Amani Karume si kikwazo cha kufikiwa makubaliano ya mwafaka iliweka mkazo na msisitizo kwamba katika kila hatua viongozi hao wameshauriwa ipasavyo. Hatua hii ya mwisho ilikusudia kubariki makubaliano hayo yaliyokuwa yakifikiwa hatua kwa hatua na siyo kufungua mjadala mpya kupitia mpya ya mazungumzo," alisema Maalim.

Hata hivyo, alisema pamoja na kushtushwa na usanii wa kisiasa katika suala hilo, wamepata faraja kwa kuwa suala hilo limewawezesha Watanzania kujua ni nani kati ya CCM na CUF asiyeitakia nchi mema, amani, utulivu na siasa za maelewano na mashirikiano.

Alisema jambo hilo limeonyesha kuwa CCM iliingia katika mazungumzo hayo ikiwa haina dhamira ya kweli na ya dhati ya kuupatia ufumbuzi wa kweli mpasuko wa kisiasa Zanzibar.

Badala yake, alisema imeonekana kuwa lengo pekee la CCM katika mazungumzo hayo, lilikuwa ni kuwahadaa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kwa kujidanganya kwamba wangeweza kuidhibiti kisiasa CUF kupitia utaratibu wa kuwapa matumaini ya uongo na kurefusha mazungumzo kadri inavyowezekana hadi kipindi kinachokaribia Uchaguzi Mkuu ujao pasi na kuchukua hatua zozote za maana kwa lengo la kutoa ufumbuzi wa kweli wa mpasuko huo.

Kutokana na hali hiyo, alisema CUF ambayo imefanya kila lililomo katika uwezo wake kuinusuru hali tete ya kisiasa Zanzibar isichafuke, imevunjwa moyo na Rais Kikwete akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM.

"Imani tuliyokuwa nayo kwake kama kiongozi wa nchi na ambayo tulibaki nayo hadi CCM inaelekea katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa imetetereka sana," alisema Maalim Seif na kuongeza:

Kutokana na hali hiyo, alisema CUF haiko tayari kushirikiana na CCM kuwafanyia Watanzania usanii wa kisiasa akisema kwamba huo sio utaratibu wa CUF katika uendeshaji wa siasa na akaitaka CCM kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya vyama.

Alisema kinyume na hayo, CUF inatoa wito kwa marafiki wa Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua madhubuti za uhakika na za haraka kuingilia kati suala hilo ili kuhakikisa makubaliano yaliyofikiwa yanatiwa saini.

Aliwashukuru viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, taasisi na jumuiya za kijamii, mabalozi na vyombo vya habari, hususan magazeti huru kwa mchango wao mkubwa walioutoa na ambao ulisaidia kufanikisha mazungumzo hadi hatua za kukamilishwa na kuwataka wanachama na wapenzi wa CUF kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki wakijua chama hicho kiko upande wa amani, ukweli na haki.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema kwamba uamuzi wa CCM kuhusu mwafaka ni hatari kwa taifa na kuishiwa kisiasa. " Maamuzi ya CCM yanaonyesha kwamba viongozi wengi wa chama hicho wamefilisika kisiasa na uwezo wao una mashaka makubwa," alisema Zitto

Suala la mwafaka lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kuamuliwa na NEC baada ya kudumu kwa takribani miaka miwili chini ya makatibu wakuu wa vyama hivyo, Yusuf Makamba na Maalim Seif Sharrif Hamad.

Imeandaliwa na Muhibu Said, Kizito Noya na Rehema Rajabu
 
Mie nafikiri CUF wasikubali kuchezewa hivi. Hivi jamani CCM wanafikiri watanzania wa 1922 ndio wa sasa?? Tatizo la Zanzibar ni uendeshwaji wa jinsi ya kupata KURA HALALI, leo hii unasema upeleke hili suala tena kwa wananchi, Bulls***. Wananchi wa Pemba na Unguja (Zanzibar) walishasema na kuamua kupitia kwenye masunduku ya kura ambayo mnataka muendeshe: Wanahitaji kile ambacho wali-indicate kwenye kura zao. Sasa leo mje na usanii wenu na kuiweka AMANI yetu rehani, mmhh mmh hatukubali ujinga huu. Sasa kama suala lilikuwa kura ya maoni kwa nini mlipoteza hela za walipa kodi kuendesha hivi vikao kwa muda wote???? Yaani hakuna ambaye alikuwa na Busara ya kusema hili suala tulipeleke kwa wananchi wenyewe KWA WAKATI HUO??? Huo nao naweza kuuita UFISADI. Wape wananchi wanachostahili, hii nchi si ya SISIEMU peke yake bali ya watanzania wote. Kumbukeni kuwa CUF inawakilisha wananchi vilevile. Acheni U-ROHO wa MADARAKA na mtangulize maslahi ya Taifa mbele.

Kikwete jaribu kuwa serious for a minute, kama nchi imekushinda kwa nini usiwe jasiri na wazi wa kusema kazi imekushinda? Mmepewa dhamana ya kuongoza nchi kwa kipindi fulani na si maisha. Wananchi ambao wamekupeni hiyo dhamana wanahitaji serikali yenye mshikamano, walishatamka tangu kipindi cha Dr. Salmin lakini mnataka kupindisha ooh mrudishe kwa wananchi wenyewe. Jamani pesa zinazidi tu kutumiwa ovyo wakati wenye nchi walishaonyesha hiyo dhamira ya serikali ya umoja.
Mkuki kwa nguruwe bwana kwa binadamu mmmh sijui ni mtamu. Ilipoibuka gasia huko Kenya, watu wakapanda ndege kwenda kusuluhisha huo mgogoro na matokeo yake Katiba ya Kenya ikafanyiwa marekebisho na amani ikarejea nchini Kenya, That was really good kwa sababu sisi hatupendi machafuko nchini au kwa majirani na duniani. Ndiyo maana JK ulidiriki kupeleka majeshi yetu Comoro bila taarifa kwa Watanzania. Sasa leo hapa Zanzibar yanakuwaje magumu??????????????????????? Watu kama akina MKAPA walishindwa kwenda Butiama kujadili suala kama hilo lakini walikuwa wa kwanza kwenda Kenya kuwapatanisha Kibaki na Odinga. Nini tofauti ya Kenya na Zanzibar?? Kenya wananchi waliamua kupitia masanduku ya kura kuwa wanahitaji mabadiliko. Waliamua kwa njia halali tena na ya kiungwana, lakini Kibaki na genge lake walibatilisha maamuzi ya wananchi matokeo yake mnayajua. Sasa Zanzibar nako walishatamka kwa njia halali na ya kiungwana lakini sisi hatutaki kuona hili suala linapewa utatuzi baada ya watu kupoteza maisha yao ingawa tulishuhudia (Mimi kwa macho yangu maana nilikuwa mtumishi wa serikali) watu wakipoteza maisha kwa kudai haki zao.

Mnatakiwa kusoma alama za nyakati na kutumia Busara. Tulisikia mambo mengi eti ooh isingekuwa busara za Kingunge na Makamba hayo majadiliano yasingefika huko. Sasa hizo busara zimeishia wapi??? Au wenyewe hawakuwa katika hivyo vikao vya Butiama. Mie nafikiri umefika wakati sasa mnatakiwa mkae pembeni maana kazi imewashinda.
ACHENI USANII KWA HAYA MAMBO MAZITO. MMLETA USANII NA PESA ZA EPA SASA MNALETA USANII KWENYE AMANI AMBAYO TUMEBARIKIWA UKILINGANISHA NA NCHI ZINGINE. PLS BE SERIOUS FOR A MINUTE FOR THE SAKE OF OUR UNITY.
 
Mie nafikiri CUF wasikubali kuchezewa hivi. Hivi jamani CCM wanafikiri watanzania wa 1922 ndio wa sasa?? Tatizo la Zanzibar ni uendeshwaji wa jinsi ya kupata KURA HALALI, leo hii unasema upeleke hili suala tena kwa wananchi, Bulls***. Wananchi wa Pemba na Unguja (Zanzibar) walishasema na kuamua kupitia kwenye masunduku ya kura ambayo mnataka muendeshe: Wanahitaji kile ambacho wali-indicate kwenye kura zao. Sasa leo mje na usanii wenu na kuiweka AMANI yetu rehani, mmhh mmh hatukubali ujinga huu. Sasa kama suala lilikuwa kura ya maoni kwa nini mlipoteza hela za walipa kodi kuendesha hivi vikao kwa muda wote???? Yaani hakuna ambaye alikuwa na Busara ya kusema hili suala tulipeleke kwa wananchi wenyewe KWA WAKATI HUO??? Huo nao naweza kuuita UFISADI. Wape wananchi wanachostahili, hii nchi si ya SISIEMU peke yake bali ya watanzania wote. Kumbukeni kuwa CUF inawakilisha wananchi vilevile. Acheni U-ROHO wa MADARAKA na mtangulize maslahi ya Taifa mbele.

Kikwete jaribu kuwa serious for a minute, kama nchi imekushinda kwa nini usiwe jasiri na wazi wa kusema kazi imekushinda? Mmepewa dhamana ya kuongoza nchi kwa kipindi fulani na si maisha. Wananchi ambao wamekupeni hiyo dhamana wanahitaji serikali yenye mshikamano, walishatamka tangu kipindi cha Dr. Salmin lakini mnataka kupindisha ooh mrudishe kwa wananchi wenyewe. Jamani pesa zinazidi tu kutumiwa ovyo wakati wenye nchi walishaonyesha hiyo dhamira ya serikali ya umoja.
Mkuki kwa nguruwe bwana kwa binadamu mmmh sijui ni mtamu. Ilipoibuka gasia huko Kenya, watu wakapanda ndege kwenda kusuluhisha huo mgogoro na matokeo yake Katiba ya Kenya ikafanyiwa marekebisho na amani ikarejea nchini Kenya, That was really good kwa sababu sisi hatupendi machafuko nchini au kwa majirani na duniani. Ndiyo maana JK ulidiriki kupeleka majeshi yetu Comoro bila taarifa kwa Watanzania. Sasa leo hapa Zanzibar yanakuwaje magumu??????????????????????? Watu kama akina MKAPA walishindwa kwenda Butiama kujadili suala kama hilo lakini walikuwa wa kwanza kwenda Kenya kuwapatanisha Kibaki na Odinga. Nini tofauti ya Kenya na Zanzibar?? Kenya wananchi waliamua kupitia masanduku ya kura kuwa wanahitaji mabadiliko. Waliamua kwa njia halali tena na ya kiungwana, lakini Kibaki na genge lake walibatilisha maamuzi ya wananchi matokeo yake mnayajua. Sasa Zanzibar nako walishatamka kwa njia halali na ya kiungwana lakini sisi hatutaki kuona hili suala linapewa utatuzi baada ya watu kupoteza maisha yao ingawa tulishuhudia (Mimi kwa macho yangu maana nilikuwa mtumishi wa serikali) watu wakipoteza maisha kwa kudai haki zao.

Mnatakiwa kusoma alama za nyakati na kutumia Busara. Tulisikia mambo mengi eti ooh isingekuwa busara za Kingunge na Makamba hayo majadiliano yasingefika huko. Sasa hizo busara zimeishia wapi??? Au wenyewe hawakuwa katika hivyo vikao vya Butiama. Mie nafikiri umefika wakati sasa mnatakiwa mkae pembeni maana kazi imewashinda.
ACHENI USANII KWA HAYA MAMBO MAZITO. MMLETA USANII NA PESA ZA EPA SASA MNALETA USANII KWENYE AMANI AMBAYO TUMEBARIKIWA UKILINGANISHA NA NCHI ZINGINE. PLS BE SERIOUS FOR A MINUTE FOR THE SAKE OF OUR UNITY.

Wakifanya kura znz wawe tayari kupokea na wageni watakao enda kuwasaidia kupiga kura. Ama kweli CCM ni number one hivi kuna mtu alijua kama CCM wangekuja na hii idea? hawa ni watu waliotunikiwa nishani za juu za roho mbaya iliyochanganyika na uchu wa kutawala hii nchi kana kwamba wao ndio wenye hati miliki. Ndio maana kuna watu humu ndani wanathubutu kusema Chadema whawata kaa watawale! kwa mitindo hii naamini espicial kwa Kikwete kushinda kwa asilimia 80% na 2010 atashindwa kwa 90% mtakuja kusema Sokomoko alisema!

Sokomoko Bin Mloboko
 
" Maamuzi ya CCM yanaonyesha kwamba viongozi wengi wa chama hicho wamefilisika kisiasa na uwezo wao una mashaka makubwa," alisema Zitto

Very strong analysis, haina matusi lakini inaeleweka na kukubalika, na yeyote anayetaka maendeleo ya taifa letu, CCM tunahitaji kufanya more than tuliyoyafanya Butiama, maana sasa hata Mugabe anayejaribu ku-negotiate his future anaonekana kuwa na busara zaidi ya mkutano wa huko Butiama,

I mean sijui the rest of the story, lakini so far ina-sound like it was another waste of time and money, na I hope hela zilizotumika huko sio za walipa kodi!
 
Warioba anachemka sasa, anaogopa kura ya maoni kwa sababu itawagawanya Wazanzibari, kama wenyewe wanataka mgawanyiko je? Kama Pemba inaamua kuwa nchi kivyake na Unguja kubaki katika muungano je, utataka kuwalazimisha?
 
Very strong analysis, haina matusi lakini inaeleweka na kukubalika, na yeyote anayetaka maendeleo ya taifa letu, CCM tunahitaji kufanya more than tuliyoyafanya Butiama, maana sasa hata Mugabe anayejaribu ku-negotiate his future anaonekana kuwa na busara zaidi ya mkutano wa huko Butiama,

I mean sijui the rest of the story, lakini so far ina-sound like it was another waste of time and money, na I hope hela zilizotumika huko sio za walipa kodi!

Hivi ni kweli kwamba hawa jamaa walipata 80% if yes uoga wote huu na kuhatarisha usalama wa Nchi kwa maslahi binafsi ni wa nini ?
 
Very strong analysis, haina matusi lakini inaeleweka na kukubalika, na yeyote anayetaka maendeleo ya taifa letu, CCM tunahitaji kufanya more than tuliyoyafanya Butiama, maana sasa hata Mugabe anayejaribu ku-negotiate his future anaonekana kuwa na busara zaidi ya mkutano wa huko Butiama,

I mean sijui the rest of the story, lakini so far ina-sound like it was another waste of time and money, na I hope hela zilizotumika huko sio za walipa kodi!

Mkuu inapochukua miaka miwili kujadili muafaka halafu jamaa wanakuja na kauli kwamba kufanyike kura ya maoni huo ni UHUNI TU na pia NI UFISADI WA HALI YA JUU. Kikwete nchi inamshinda hakuna lolote alilolifanya tangu aingie madarakani pamoja na ahadi chungu nzima zilizomfanya achaguliwe kwa asilimia kubwa sana. Aliahidi kufikia muafaka na CUF ndio huo baada ya majadiliano ya miaka miwili haukuleta maelewano yoyote. Aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania, tunajua hali ya maisha ilivyokuwa ngumu kwa Watanzania walio wengi. Aliahidi ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya, tunaona alivyokuwa hana uwezo waufanya maamuzi yanayoungwa mkono na Watanzania wengi kuhusiana na matukio mbali mbali mazito ndani ya nchi yetu ya ufisadi uliotokea BoT, Richmonduli, ununuzi wa rada, magari ya jeshi na helicopters, ndege ya Rais n.k.

Aliahidi kupitia mikataba ya madini, kama siyo Slaa na Zitto kuanika hadharani mkataba wa Buzwagi uliovuja hadi hii leo angekuwa hajafanya chochote! Mafisadi wa mabilioni ya BoT bado wanapeta mitaani na mapesa yao ya wizi. Waliosaini mkataba na Richmonduli ambao tumelipa $172 million bila wahusika kufanya kazi yoyote bado wanapeta mtaani. Watanzania wana uvumilivu wa hali ya juu. Wengi walikuwa na matumaini makubwa na kikao cha NEC na CC kilichoisha juzi, lakini kama tunavyofahamu wametumia mabilioni ya walipa kodi na kufanya usanii na uhuni mwingine.

Kwa hiyo Watanzania watakapoanza kuwazomea, kuwarushia matusi basi hakuna wa kulaumiwa bali ni wahuni na mafisadi wa CCM wenyewe ndio wa kulaumiwa kwa kusababisha hali hiyo. Tuuvumilie ufisadi na uhuni wao mpaka lini? :(
 
Warioba anachemka sasa, anaogopa kura ya maoni kwa sababu itawagawanya Wazanzibari, kama wenyewe wanataka mgawanyiko je? Kama Pemba inaamua kuwa nchi kivyake na Unguja kubaki katika muungano je, utataka kuwalazimisha?

Usimkurupikie mzee wetu huyu!!

Sio kwamba warioba anaogopa kura, lakini anajua the end result ya kupiga kura zanzibar.

Ebu wewe mwana democrasia tukuulize:: Kwani kura za 1995, 2000, 2005 ziliheshimiwa au CCM ilifanya ambacho itafanya hata kwenye kura za maoni???

JK amechemsha kupita kiasi.

Mimi nadhani hata tax ya petrol, sigara, bia zinawagusa wananchi sana sasa kwa nini tusiwe na kura za maoni kuona watanzania wanataka tax iondolewe au la??

Also tuwe na kura za maoni kama tunaridhika na utendaji wa viongozi wetu sababu hili nalo linagusa wananchi.

Yaani uongozi mmepewa halafu kwenye hili mnajifanya tuwaulize wananchi ahahahaha
 
I mean sijui the rest of the story, lakini so far ina-sound like it was another waste of time and money, na I hope hela zilizotumika huko sio za walipa kodi!

Mzee baadhi ya gap ya story ni kuwa mafisadi wa bara waliungana na wazanzibar kuleta mtarafuku kwenye hili wakijua wazi kuwa kutakuwa hakuna nafasi ya kudeal nao baada ya hii fiasco. Also wazanzibar wa kwenye NEC walihitaji msaada wao kuzima hili na mafisadi wameahidiwa kulipwa fadhila JK atakapoleta za kuleta.

CCM and JK are in big trouble.

Mkuu najua unapata za ndani kabisa ya chama, lakini mkuu wa Kaya kachemsha kupita kiasi. Sasa hivi hana support ya mafisadi kwa kumbwaga Lowassa na mambo ya EPA, also kwa kushindwa kuwadhibiti kikamilifu kwenye chama anakosa full support ya wazee wa chama wenye maadili kwa hiyo ana kosa kote kote.

Yaani anaonekana amateur kupita kiasi because he doesn't stand firm on anything. Yaani aibu tupu
 
CUF plans mass action

CCM Chairman President Jakaya Kikwete during the last session of the part's National Executive Committee meeting in Butiama on Sunday evening
By The Citizen Team

The Civic United Front (CUF) is gearing towards mass action to demand the implementation of the power-sharing deal agreed with CCM.

Mediation committees of both sides agreed on a grand coalition government as the way forward to govern Zanzibar, but the ruling party has dramatically turned down the agreement, throwing the ball into a referendum.

The deadlock between the two parties could trigger another conflict in the Isles, which has experienced a political impasse since the first multiparty elections held in 1995. CUF is expected to issue a statement in what it described as a strong stand about the decision by the ruling party to turn down the proposed peace accord that would enable the two parties to share power virtually on equal terms.

In Zanzibar, CUF members of the House of Representatives yesterday cut short their participation in the House session, after they were summoned by the top party officials to discuss the CCM stance. Speaking to The Citizen in Dar es Salaam yesterday, CUF deputy secretary general Juma Duni Haji said his party was shocked by the decision of the ruling party's National Executive Committee meeting in Butiama.

We didnt expect this situation but we have initiated consultations before issuing our stand tomorrow, he said. CUF took up mass action was on January 27, 2001 and 39 people were killed, according to a presidential commission of inquiry later. But diplomats had put the figure at more than 60 dead. Several thousands crossed by boat to Mombasa, northward from Pemba.

Following the shootings, the Government allowed demonstrations. Discussions started later. The September 11 strikes dramatically changed the scene, and the negotiations saw a surprising breakthrough on October 10, 2001. It was half implemented, and the same climate of polling was repeated in 2005.

With similar complaints governing the post-election mood, and new Union President Jakaya Kikwete declaring his intention to find a solution to the Isles impasse, new talks were engaged, ending virtually as the second mandate of President Amani Karume reached halfway point. With the accord torpedoed, and the issue directed towards a vexing referendum, chances of power sharing before the end of the current Isles presidency ends have now evaporated.

The Citizen was told that NEC members from Zanzibar were the main stumbling block for the power sharing deal that was supposed to be endorsed by the party during the meeting.

After stiff opposition from the Isles' members of the ruling party, CCM decided that a referendum be held in Zanzibar to determine whether power sharing be introduced.

Signs towards the ruling party's failure to approve the agreement last weekend were evident on Friday after news broke out that central committee members were divided on the agenda right before the NEC meeting.

The decision to take back the matter to Zanzibaris for final approval was reached by the NEC meeting held from Saturday to Sunday in Butiama, Mara region under its chairman, President Jakaya Kikwete.

Reading the resolutions after the NEC meeting at 2300 hours, CCM vice chairman Pius Msekwa said basically the ruling party agreed to the recommendations in the Mwafaka talks report. However, he said after scrutinising the report on Mwafaka NEC members made some amendments to the original Mwafaka report compiled between CUF and CCM negotiation teams.

NEC ordered the CCM negotiation team to go back to the negotiation table to deliberate on the amendments made by NEC members in their meeting. He said since the recommendations made to Mwafaka report by NEC will change the system of administration in the Zanzibar government if endorsed, then Zanzibaris must participate in reaching the decision through a referendum.

He said NEC members were disappointed by the CUF decision to make the agreement public, contrary to the terms of the agreement at that point. In what political analysts view as delaying tactics by the party's hardliners from Zanzibar, after the CCM side failed to endorse the agreement over the weekend, peace prospects have receded.

The burning issue according to CCM insiders was the inclusion of the CUF in the government, to occupy the post of chief minister.

Chief Minister Shamsi Vuai Nahodha was to be replaced for a CUF member as head of the government, a move that wasn�t endorsed by NEC members from Zanzibar. Reacting to the CCM move, Prof Mwesiga Baregu of the University of Dar es Salaam warned that the stand stokes political tensions in an already volatile climate in the Isles.

What CCM has decided is a big shame�after all the efforts by interparty committee the matter is again being taken back to negotiation and a further vote,� the don said in a telephone interview. Recently CUF secretary general Seif Sharif Hamad told supporters in Zanzibar that CUF had reached a power sharing deal with CCM in which CUF would take the post of Chief Minister.

Addressing a rally, he said that the agreement provides that a party garnering more votes would take the presidency while the other would take the slot of chief minister. The CCM decision to take back the pact to a referendum was a disavowal of the pact, as it appears that the negotiations have been taken back to the drawing board.

Reports by Rodgers Luhwago, Butiama; Mkinga Mkinga, Dar es Salaam; and Salma Said, Zanzibar
 
Back
Top Bottom