BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,110
Posted Date::4/1/2008
Muafaka: Uamuzi wa CCM Butiama wafananishwa na ufisadi wa kisiasa
*Wasomi wasema utachochea uhasama
*Warioba asema ana mashaka na kura za maoni
*Awataka viongozi kuacha kukwepa wajibu wao
*CUF wataka mataifa ya nje yaiokoe Z'bar
Waandishi Wetu
Mwananchi
TAMKO la Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), kuhusu hatima ya Mwafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar, limezua mapya, baada ya wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chama cha Wananchi (CUF), kuliita kuwa ni ufisadi na usanii wa kisiasa.
Kauli hiyo ilitolewa kwa nyakati tofauti na baadhi ya wahadhiri wa UDSM waliozungumza na Mwananchi na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alipozungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu chama hicho, jijini Dar es Salaam jana.
Wakati wasomi na CUF wakitoa maoni yao, Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Joseph Sinde Warioba aliiambia Mwananchi jana kuwa uamuzi wa CCM kuamua kuendesha kura za maoni utazidi kuwagawa Wazanzibari badala ya kuwaunganisha.
Wahadhiri hao, Maalim Seif na Jaji Warioba walitoa kauli hiyo kufuatia tamko la NEC juu ya suala la Mwafaka lililotolewa juzi baada ya kuhitimisha kikao chake katika Kijiji cha Butiama, mkoani Mara, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo ilitaka ifanyike kura ya maoni visiwani Zanzibar ili kupata ridhaa ya wananchi kuhusu kuundwa kwa serikali ya mseto visiwani humo.
Warioba alisema kwamba suala la maamuzi wa serikali ya mseto liko ndani ya viongozi na kwamba wasikwepe majukumu yao." Suala la kutekeleza Mwafaka liko ndani ya uongozi, hivyo wasikwepe wajibu wao," alisema.
Alisema kimsingi hana matatizo kama viongozi wana nia ya kuboresha mchakato wa Mwafaka, lakini ana wasiwasi kwamba mchakato huo ukifika hadi wakati wa uchaguzi unaweza usiwe na maana inayokusudiwa.
"Matatizo ya Zanzibar yanatokana na uchaguzi, hivyo hayawezi kutatuliwa kwa uchaguzi," alisisitiza Jaji Warioba.
Warioba alitoa mfano wa Chama cha ANC cha Afrika Kusini ambacho kilishinda kwa wingi wa kura, lakini kikashirikisha vyama vingine kwa lengo la kuunganisha wananchi. "Vyama vikiungana kwa mtindo wa serikali ya mseto, hata wananchi pia wataungana," alisema.
Alisema mfano mzuri ni visiwani Zanzibar ambapo kabla ya viongozi wa CUF na CCM kuanza mazungumzo ya kuleta Mwafaka visiwani humo, wananchi walikuwa hawazikani kwa sababu za kiitikadi, lakini viongozi wao walipoanza kuzungumza na wananchi nao walipunguza chuki baina yao.
Profesa Mwesiga Baregu wa Sayansi ya Jamii, Idara ya Siasa ya UDSM, alisema kitendo cha CCM kutaka suala la Mwafaka kupigiwa kura ya maoni na wananchi baada ya kukaa nalo kwa miaka miwili sasa, ni uhuni unaoweza kulipeleka taifa katika migogoro.
CCM wanafanya uhuni na huu ni mchezo mbaya sana kwa sababu yaliyoharibika Kenya yalitokana na wananchi kukosa imani na serikali kutokana na uhuni wa aina hiyo,? alisema Profesa Baregu.
Alisema tabia ya Serikali ya CCM kuanzisha michakato mizito ya kitaifa na kufanya ghiliba za makusudi kisha kuiacha kwenye utata, ni ufisadi wa kisiasa na hatari kwa uhai wake na maendeleo ya taifa.
Tofauti na ufisadi wa uchumi ambao bado unazungumzwa, kitendo hicho ni ufisadi wa kisiasa na kama serikali haisimamii haki, haistahili kuaminiwa wala kuheshimika na matokeo hayo yote ni watu kuchukua sheria mkononi,? alisema.
Alisema uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM kurudisha mjadala wa mwafaka kwa Wananchi wa Zanzibar wakati wajumbe wake ni viongozi wa CUF na CCM Taifa ni ujanja wa kuukataa mwafaka.
Uamuzi huo unaondoa imani na dhamira njema ya CCM kuhusu mwafaka. Kwa nini hatima ya mazungumzo hayo yakafanywe na Wazanzibari tu wakati walioshiriki ni makatibu Wakuu wa vyama vyenye wanachama Bara na Zanzibar?? alihoji Baregu.
Profesa Baregu alisema kama kuna umuhimu kura za maoni ziendeshwe kuhusiana na kutungwa kwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar badala ya kupoteza fedha nyingi kuendesha kura za maoni kuhusu mwafaka tena katika mazingira ambayo jamii inafahamu kuwa CCM inaukataa.
Profesa mwingine wa kitivo hicho, Ernest Mallya alisema uamuzi wa CCM kutaka hatma ya mwafaka kuamriwa na wananchi wa Zanzibar kwa kura za maoni, ni ishara kuwa hawakuwa na nia thabiti kuutafuta.
Alisema kura za maoni haziwezi kutoa mwelekeo unaotarajiwa kuhusu mwafaka badala yake zitaongeza uhasama baina ya pande mbili zinazovutana kuhusu suala hilo.
Kura ya maoni ni uchaguzi ambao ni wazi CCM itashinda kwa mbinu zilezile wanazotumia kushinda chaguzi zingine. Hiki ni kigezo ambacho chama hicho kinataka kukitumia kuukataa na CUF wasikubali, wakatae,? alisema Profesa Mallya.
Profesa Mallya alitaka CCM kuanzisha mchakato wa kura za maoni katika kero zote za muungano kama ina nia njema na taifa badala ya kukazania kura za maoni kuhusu mwafaka ambazo tayari imejiandalia ushindi wa kuukataa.
Kauli ya Profesa Mallya iliungwa mkono na Mhadhiri Msaidizi wa idara hiyo Bashiru Ally aliyesema kuwa kura za maoni haziwezi kuleta mwafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar.
Alisema kama suala hilo limeshindwa kufikia tamati katika mikutano ya viongozi wa vyama viwili vinavyopingana, halitaweza pia kukamilika kwa kura za maoni kwani kura ndizo zilizokuwa chanzo cha mgogoro huo.
Alieleza kuwa utaratibu wa kura za maoni hauna tofauti na kampeni za Uchaguzi Mkuu unaowagawa watu katika makundi mawili yanavutana na kuongeza mgogoro badala ya suhulisho.
Ally alisema hakuna maana nyingine zaidi ya ?danganya toto? kuanzisha mchakato wa kura za maoni kuhusu mwafaka wakati kuna matatizo mengi ya kitaifa yanayotakiwa kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Kwa nini tutumie fedha kuwauliza wananchi kuhusu mwafaka na kuacha mambo ya msingi kama matatizo ya ardhi, madini, uraia na maeneo mengine yenye utata kama siyo kuvuta subiri na kuwadanganya wenzao wa CUF alihoji.
Kuwauliza wananchi kuhusu mwafaka ni kuongeza chumvi kwenye kidonda, kwani hadi sasa Watanzania bado hawajajua hatima ya wizi wa EPA na kamati za madini, alisema.
Mhadhiri wa sheria chuoni hapo, Dk Sengondo Mvungi alisema matumizi ya rasilimali za umma katika mpango wa kupata kura za maoni ni aina nyingine ya ufisadi katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete.
Alisema hakuna sababu za msingi kuitisha kura za maoni kuhusu serikali ya mseto visiwani Zanzibar wakati Katiba haikatazi.
Tunawauliza wananchi ili watupe majibu gani kuhusu serikali ya mseto wakati tayari Katiba haipingani nayo?? Kama watafanya na wakatumia fedha za umma tutawapigie kelele kwani huo ni ufisadi, alisema
Dk Mvungi alisema kuitisha kura za maoni sio kosa na inaruhusiwa kikatiba, alibainisha kuwa matumizi ya rasilimali za umma katika mambo binafsi ya wanasiasa ni kosa kisheria.
Mhadhiri Msaidizi wa kitivo hicho cha sheria, Makarios Tairo alisema kura za maoni VIsiwani Zanzibar zisiendeshwe kwa ajili ya mwafaka bali ziendeshwe kwa upana zaidi kulinda maslahi ya Wazanzibari na Watanzania wote.
Alisema historia inaonyesha kuwa tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi visiwani Zanzibar vyama vya CUF na CCM vimekuwa vikishindana kwa tofauti ndogo ya kura jambo ambalo linaleta umuhimu wa kuwa na serikali ya mseto baina ya vyama hivyo viwili.
Wakati wahadhiri hao wakisema hayo, CUF, imepinga hoja ya CCM ya kutaka ifanyike kura ya maoni Zanzibar ili kupata ridhaa ya wananchi ya ama iundwe au isiundwe serikali ya mseto visiwani humo.
Badala yake, CUF imeitaka CCM kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya Vyama hivyo, ikiwa ni pamoja na kutia saini makubaliano hayo na kuyatekeleza mara moja.
Katika mazungumzo yao yaliyochukua takriban miezi 14 na vikao 21, pamoja na mambo mengine, CUF ilidai kuwa walikubaliana na CCM kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, maarufu kama "serikali ya mseto" itakayoshirikisha pande mbili za vyama hivyo.
Mbali na hilo, CUF pia imepinga hoja ya kufanywa kwa marekebisho katika baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Mazungumzo ya Vyama hivyo, ambayo CCM imeiagiza kamati yake kukutana na wajumbe wa CUF ili kujadili mapendekezo hayo.
Katika tamko lake lilisomwa na Maalim Seif jana, CUF imesema hoja hizo ni usanii wa kisiasa, ubabaishaji na upotoshaji uliofanywa na CCM kwa lengo la ama kuendelea kurefusha muda hadi mwaka 2010 au kuyakataa makubaliano ambayo wajumbe wake wameshiriki kuyaandaa katika miezi 14 ya mazungumzo kati ya vyama hivyo.
"Kwa msingi huo CUF haikubaliani na hoja hizo zote mbili," alisema Maalim Seif.
Maalim Seif alisema kinachosikitisha zaidi ni kuwa tofauti na ilivyoelekezwa, pendekezo la kutaka kura ya maoni, halikuwa limeibuliwa na wajumbe wa NEC, bali lilikuwamo katika taarifa ya Kamati ya CCM inayoshiriki mazungumzo, likiwa ni pendekezo walilotaka liridhiwe na Kamati Kuu (CC) ya NEC.
"Hivyo, ni wazi liliandaliwa mapema kutokana na kile kamati hiyo ya CCM ilichokiita 'kuipiku CUF katika ubunifu wa kujenga'," alisema Maalim Seif.
Alisema kitendo cha Kamati ya CCM kuwasilisha kitu kipya nje ya makubaliano yaliyofikiwa, ni upotoshaji mkubwa wenye lengo la kulifanyia usanii wa kisiasa suala kubwa linalogusa maslahi ya taifa na watu wake moja kwa moja.
Alihoji kama pendekezo la kura ya maoni lina nia njema ya kuwashirikisha wananchi, kwa nini wajumbe wa Kamati ya CCM wasiliwasilishe katika vikao vya mazungumzo na badala yake wakaamua kuliingiza kama mtego wa kisiasa wenye lengo la kuipiku CUF
Maalim Seif pia alihoji iwapo kura ya maoni itaendeshwa na chombo kipi na kwa utaratibu upi, hasa ikitiliwa maanani tayari CCM na CUF wamekubaliana kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Daftari la Kudumu la Wapigakura, vina matatizo ya msingi ambayo yanahitaji kurekebishwa
"Ni vipi basi tume hiyo chini ya daftari bovu lililopo itaweza kuendesha kura ya maoni ambayo itakuwa huru na ya haki?," alisema Maalim Seif na kuongeza:
"Sisi tunaona suala hilo ni mbinu chafu yenye lengo la kuendelea kupoteza muda ili makubaliano yaliyofikiwa yasiweze kutiwa saini na utekelezaji kuanza. Kwa lugha yao CCM waliyoandika katika waraka wao ni njia ya kuipiku CUF na kamwe haikusudiwi kupata maoni ya wananchi".
Kuhusu marekebisho katika baadhi ya mapendekezo ya Kamati ya Mazungumzo ya Vyama hivyo ambayo CCM imeiagiza kamati yake kukutana na wajumbe wa CUF kujadili mapendekezo hayo, Maalim Seif alisema hawaungi mkono suala hilo kwa kuwa CCM haijataja ni maeneo gani inataka yafanyiwe marekebisho.
Alisema hoja hiyo inashangaza kwa sababu wajumbe wa Kamati ya Mazungumzo kutoka CCM, walikuwa wakiwaarifu wajumbe kutoka CUF kwamba, walikuwa wakiwasilisha taarifa kwa kila hatua inayofikiwa katika vikao vya CC na NEC na kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na kupata maelekezo na miongozo inayohitajika.
"Hata taarifa ya karibuni kabisa ya CCM iliyokuwa ikikanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba mheshimiwa Amani Karume si kikwazo cha kufikiwa makubaliano ya mwafaka iliweka mkazo na msisitizo kwamba katika kila hatua viongozi hao wameshauriwa ipasavyo. Hatua hii ya mwisho ilikusudia kubariki makubaliano hayo yaliyokuwa yakifikiwa hatua kwa hatua na siyo kufungua mjadala mpya kupitia mpya ya mazungumzo," alisema Maalim.
Hata hivyo, alisema pamoja na kushtushwa na usanii wa kisiasa katika suala hilo, wamepata faraja kwa kuwa suala hilo limewawezesha Watanzania kujua ni nani kati ya CCM na CUF asiyeitakia nchi mema, amani, utulivu na siasa za maelewano na mashirikiano.
Alisema jambo hilo limeonyesha kuwa CCM iliingia katika mazungumzo hayo ikiwa haina dhamira ya kweli na ya dhati ya kuupatia ufumbuzi wa kweli mpasuko wa kisiasa Zanzibar.
Badala yake, alisema imeonekana kuwa lengo pekee la CCM katika mazungumzo hayo, lilikuwa ni kuwahadaa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kwa kujidanganya kwamba wangeweza kuidhibiti kisiasa CUF kupitia utaratibu wa kuwapa matumaini ya uongo na kurefusha mazungumzo kadri inavyowezekana hadi kipindi kinachokaribia Uchaguzi Mkuu ujao pasi na kuchukua hatua zozote za maana kwa lengo la kutoa ufumbuzi wa kweli wa mpasuko huo.
Kutokana na hali hiyo, alisema CUF ambayo imefanya kila lililomo katika uwezo wake kuinusuru hali tete ya kisiasa Zanzibar isichafuke, imevunjwa moyo na Rais Kikwete akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM.
"Imani tuliyokuwa nayo kwake kama kiongozi wa nchi na ambayo tulibaki nayo hadi CCM inaelekea katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa imetetereka sana," alisema Maalim Seif na kuongeza:
Kutokana na hali hiyo, alisema CUF haiko tayari kushirikiana na CCM kuwafanyia Watanzania usanii wa kisiasa akisema kwamba huo sio utaratibu wa CUF katika uendeshaji wa siasa na akaitaka CCM kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya vyama.
Alisema kinyume na hayo, CUF inatoa wito kwa marafiki wa Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua madhubuti za uhakika na za haraka kuingilia kati suala hilo ili kuhakikisa makubaliano yaliyofikiwa yanatiwa saini.
Aliwashukuru viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, taasisi na jumuiya za kijamii, mabalozi na vyombo vya habari, hususan magazeti huru kwa mchango wao mkubwa walioutoa na ambao ulisaidia kufanikisha mazungumzo hadi hatua za kukamilishwa na kuwataka wanachama na wapenzi wa CUF kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki wakijua chama hicho kiko upande wa amani, ukweli na haki.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema kwamba uamuzi wa CCM kuhusu mwafaka ni hatari kwa taifa na kuishiwa kisiasa. " Maamuzi ya CCM yanaonyesha kwamba viongozi wengi wa chama hicho wamefilisika kisiasa na uwezo wao una mashaka makubwa," alisema Zitto
Suala la mwafaka lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kuamuliwa na NEC baada ya kudumu kwa takribani miaka miwili chini ya makatibu wakuu wa vyama hivyo, Yusuf Makamba na Maalim Seif Sharrif Hamad.
Imeandaliwa na Muhibu Said, Kizito Noya na Rehema Rajabu