Muafaka Na Ccm Ni Ndoto

Kamende

JF-Expert Member
Mar 1, 2008
416
45
Salaam wakubwa

Kwa takribani miezi 14 na ushee tumekuwa tukifuatilia kwa makini tamthiliya ya muafaka baina ya CCM na CUF. Tamthiliya hii imekuwa ikitufikisha mahali pa kuamini kuwa bado kidogo sana muafka ufikiwe na ghafla inatokea tena tunaona jinsi ilivyo vigumu kufukiwa kwa muafaka.

Waheshimiwa muafaka si rahisi kufikiwa kutoka na sababu zifuatazo.
1. Katiba ya nchi ina madhaifu mengi ambayo yanaifanya CCM ichezee
mustakabali wa nchi inavyotaka yenyewe. Hakuna mahali kwenye katiba
panakoainisha wazi wazi adhabu zitakozomkuta kiongozi akichezea amani
yetu.
2. Matendo ya kale ya viongozi wa CCM yanawanyima kufungua milango ya
kushirikiana na CUF kwani kwa kufanya hivyo uovu wao utawekwa wazi na
yamkini umaarufu wao utafutika na pengine wataswekwa lupango.
3. Tatizo la mpasupo wa Zanzibar unafanana kabisa na huu ulioko bara.
Tofauti yetu ni namna tunavyorespond kwenye matukio. Kama wakisikizana
kule visiwani basi wamefungua mlango wa masikizano nchi nzima
4. Asili ya muafaka imepotoshwa kwa kufanywa ya vyama 2 tu vya CCM na
CUF. Nia ya CCM katika muafaka ilikuwa kuwapoza CUF tu. Wavute muda
hadi ufikike wakati mwingine wa uchaguzi.
kwa hiyo kwa maovu ambayo yameshafanywa na serikali ya CCM si rahisi wakashirikiana na CUF ama chama kingine chochote kwani kwa kufanya hivyo itakuwa inajiweka wazi mbele ya umma. Ule usiri wa sirikali utakufa. Hii ni kusema tutapata muafaka baada ya kizazi hiki chote kuondoka madarakana na kufa. Kumbuka kuwa kila kiongozi anayestaafu anaweka mazingira ya kuwa salama dhidi ya kushitakiwa kwa maovu yake aliyotenda. Usalama huu anahakikishiwa na viongozi aliowaweka madarakani yeye mwenyewe wakamrithi. Huu mrithishano ndo gonjwa linalosababisha mpasuko kwa sasa.

CCM wangekubali muafaka vizuri sana, tena wangeusaini kirahisi kwa sherehe kubwa kama usingekuwa na kipengele cha kushirikiana madaraka. CUF wamekubali mengi tu. CCM wamekiri makosa yao kadhaa. Likiwepo la kupoka ushindi. Sasa mmeshafikia kukaa meza moja na kufanikiwa kujadili mabaya yaliyowakosanisha iweje mshindwe kuweka dawa ya pamoja ya kuponya madonda yenu??

NImeona hapa jukwaani tuliangalie hili jambo kwa umakini. Ili tuone kwa nini JK anashughulikia hili jambo kimachale. na kwa nini kamati inakwenda mbele na kurudhi nyuma. Na kutokana na hali hiyo ya kuogopa kuanikwa kwa maovu yake iliyofanya kwa miaka mingi CCM kamwe haitasaini muafaka wenye lengo la kuwa na serikali ya Mseto Zanzibar.
 
Kamende,

Twajua kweli swala za zenj ni tatizo na lenye kuleta sura mbaya ktk taifa letu, sote tungetamani kuona mambo yanakuwa shwari, ila sasa usisahau kuwa zenj ina baraza la mawaziri na pia ina rais, nadhani Jk anashindwa alimalize vipi kama wale walioko madarakani kule zenj wanaendelea kung'ang'ania nafasi walizonazo kwa sasa, wanadhani wakikubali kusaini tu basi watazipoteza nafasi zao, ila hili linawezekana kutekelezwa 2010, tusimlaumu sana jamaa kwani ni yeye huyu huyu aliyelianzisha jambo hili. Jk ana nia njema ktk hili ila ni vile vikwazo anavyokabiliana navyo kwa sasa sote twajua,
 
Back
Top Bottom