EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Tendwa amewaandikia barua viongozi wa vyama hivyo kuwaagiza kuwa wateue wajumbe watakaounda kamati maalumu itakayoshughulikia suala hilo. Vyama hivyo vimejulishwa juu ya utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wa kuwepo timu ya pamoja kujadili na kuutafutia ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo.
Barua ya msajili iliyoandikwa kwa Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na Dk Slaa wa Chadema zilipokelewa katika ofisi za vyama hivyo Agosti 17, mwaka huu.
Kutokana na taarifa hiyo ya Tendwa, Chadema tayari imeteua wajumbe wanane watakaongozwa na Dk Slaa katika vikao vya majadiliano na wenzao kutoka CCM, wengine katika timu hiyo ni wajumbe wa kamati kuu, Mabere Marando, Tundu Lissu na Lazaro Massay ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu na mwenyekiti wa mameya na wenyeviti wa halmashauri zinazoongozwa na Chadema.
Wajumbe wengine ni Mbunge wa Arusha, Godbless Lema, Mkurugenzi wa Halmashauri na Bunge, John Mrema, katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa na Diwani wa Kata ya Levolosi ambaye pekee ndiye hakusaini muafaka uliosababisha wenzake kutimuliwa, Ephata Nanyaro.
Dk Slaa alikiri kupokea barua ya msajili iliyowajulisha uwepo wa kamati vya vyama hivyo kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa umeya Arusha na kuteua wajumbe watakaoshiriki kutoka chama chake.
Kwa upande wa CCM, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nnape Nnauye, alikataa kuzungumzia suala hilo akisema kuwa hayo ni majungu. "Hayo ni majungu," alisema Nnauye alipotaka kujua kama Tendwa amethibitisha kwa kinywa chake kuhusu muafaka huo.
Nnauye ambaye amekuwa mmoja wa viongozi wa CCM walio mstari wa mbele kukisafisha chama chake dhidi ya viongozi wenye kashfa za kifisadi, alisema atakuwa tayari kujibu hoja iliyotoka moja kwa moja kinywani mwa Tendwa na siyo maandishi.
Akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni hivi karibuni, Waziri Mkuu aliwaruka viongozi wa Chadema waliokuwa wameeleza kuwa kamati ya usuluhishi katika mgogoro wa Arusha itaundwa na kwamba, viongozi wa chama hicho na Pinda walishakubaliana.
Source: Mwananchi