Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,733
- 40,846
Najaribu kujiuliza kama kweli muafaka, mapatano na umoja wa Zanzibar na hatima ya Taifa letu vinaweza kufikiwa bila kuzungumzia kwa uwazi na ukweli matukio yaliyosababisha mapinduzi ya 1964, matukio yenyewe ya mapinduzi na kilichotokea usiku ule wa damu, machozi, na machungu; usiku uliozaa Zanzibar ya leo na matukio yaliyotokea baada ya mapinduzi. Ule usiku wa kukumbukwa.
Haya madai ya Uhizbu n.k yanatulazimisha kuangalia kama kweli muafaka unaweza kuwa wa kina, wa kweli, na wenye kuleta hatima ya umoja na mshikamano kwa watu wa Unguja na Pemba pasipo kugusia tukio ambalo naamini ni kiini na mzizi wa mgogoro wa leo?
Je mtu aweza kuukausha mti kwa kukata majani na matawi tu bila kung'oa mizizi?
Mjadala is open.