Muafaka Arusha-CHADEMA na CCM ndio suluhisho la demokrasia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muafaka Arusha-CHADEMA na CCM ndio suluhisho la demokrasia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Jun 28, 2011.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wito ulitolewa na viongozi waandamizi wa CDM, uchaguzi wa Meya wa Arusha umekuwa na hitilafu wa kisheria na uchaguzi umeendeshwa isivyo halali, kanuni kutofuatwa na kuwa na wapiga kura wasio halali. Kauli mbiu zikaanza kwamba Meya ni batili amepatiana isivyo halali. Cdm ikiwa ni chama kinapigania haki za sheria katika chaguzi na maisha ya kufuata sheria, kauli mbiu ikaingia mioyoni, masikioni na katika aliki za wananchi , wafuasi na mashabiki wa demokrasia hasa CDM.

  Viongozi wa kitaifa wa CDM waliingilia kati wakiomba mamlaka zinazohusika kuitisha uchaguzi huru na wa haki unafuata sheria na taratibu zilizowekwa. Ikumbukwe wizi katikati chaguzi, kuvunja sheria au kubeba wagombea wa chama tawala (CCM) imekuwa ndio desturi ya CCM kushinda chaguzi. Hila za kutumia kutoa hongo za madaraka au hata fedha hutumika kwenye chaguzi nyingi sana, Tanzania na nchi zinakosa demokrasia ya kweli. Hivyo ni matumaini ya wengi kuona vyama mbadala vikipiga vita mbinu zote na hila ya kuingia madarakani kwa mkato.

  Tabia inayostawi sasa kwenye nchi za kiafrika, ni vyama tawala kuiba kura, kuvunja kanuni na sheria za uchaguzi ili wabaki madarakani. Na pale wanapoona kuwa kelele zinakuwa kubwa hulainisha wapinzani wao kwa kuwapa pipi za madaraka ili kuweza kuiua demokrasia na kuua moyo wale wote wenye nia ya kweli kutaka kuona demokrasia ya kweli ikistawi bila upendeleo, wizi, hila, na aina yeyote ya dhuluma kwenye kuchagua viongozi wanaopendwa na wengi. Matokeoa kama haya tumeyaona Zanzibar, Kenya, Zimbwabwe na nchi kadhaa za Afrika.

  Arusha ilikuwa ni litmus test ya CDM kuwa na kauli moja na kutetea demokrasia ya kweli kwa gharama yeyote, hata kupoteza umeya na unaibu meya. Hili linaweza kuonekana sio sawa, ila unapokuwa una nia ya kweli kupambana na utawala dhalimu kama wa CCM, ambao umejipanga kuwa madarakani kwa gharama yeyote ni lazima wajue na kuwaonyesha huwezi kubali kitu chochote zaidi ya haki. Unapokubali sheria ulizosema zimevunjwa, na ukawa tayari kutoa maisha yako kutetea ukweli, halafu ghafla ukaja na kauli inayokubali uliyokuwa unayapinga hata kuweka maisha yako na watu rehani, unapoteza hadhi ya kuaminiwa mbele ya jamii.

  Muafaka wa Arusha ulikuwa ni tunu kwa ajili ya demokrasia ya nchi na Arusha. Ulikuwa ni tunu kwa utulivu wa wakazi, watalii, wageni wawekezaji wa ndani na nje kwa watu Arusha. Ulikuwa ni fahari kwa watetea demokrasia hasa wale walioacha shughuli zao na kuweka maisha yao rehani kwenye mtutu wa bunduki kutetea uhuru na haki ya demokrasia. Makundi yote haya yalitegemea muafaka wenye ukweli, demokrasia, haki na unafuata sheria na kulinda haki ya msingi ya mpiga kura. Muafaka ambao ungejalii zaidi matokeo ya haki yenye kutukuza demokrasia na mfumo wa kuheshimu sheria husika.
  1. Mosi kurudiwa kwa uchaguzi mzima wa meya
  2. kutoa maelezo jinsi sheria zilivyovunjwa
  3. Polisi wote waliohusika kufanya vurugu na kuuwa watu kufikishwa mahamani
  4. Wakurugenzi waloanzisha vurugu zile kwa kukiuka sheria zao za uchaguzi kuwajibika
  5. Fidia kwa wafiwa na wote walioumizwa na jeshi la polisi
  6. Ufafanuzi wa sheria za uchaguzi wa ma-Meya na ufafanuzi wa mipaka ya wabunge wa viti maalumu.
  7. Kufutwa kwa kesi zote zilifunguliwa kwa ajili ya maandamano ya kumpinga Meya
  8. Serikali kulaani uvunjifu wa sheria za uchaguzi za umeya na chaguzi zote zinazozumia kodi za wananchi na kuweka wazi makosa yale hayata rudiwa tena.
  9. Serikali kutamka wazi Kazi ya Jeshi la polisi ni kulinda raia na mali zao sio kuwauwa.
  Viongozi wa CDM walitakiwa wawe wa kwanza kutoa maelezo ya muafaka. Kama ni kweli madiwani walijiamuliwa wenyewe swala ambalo lilikuwa la kitaifa kuna ufa mkubwa sana wa mawasiliano kati ya watendaji wa chini na wa juu ndani ya CDM.

  Madhara ya huu muafaka ukisimama kama ulivyo, inaonyesha wazi kuwa hata chaguzi zingine CCM watakuwa na mwanya wa kuvunja sheria wakijua muafaka utasawazisha. Hii tabia ndio inajenga madikteta duniani. Nelsoni mandela alipopewa deal na makaburu ili atoke nje na wenzeka wabaki ndani, huku akitakiwa aondoke South Afrika alisema hawezi kutoka akiwaacha wenziye nadani na hawezi kutoka na kuondoka SA, kwa kukataa deal ambayo haikuwasaidia wananchi wake kujikomboa alijiongezea miaka mingi zaidi ya kukaa jela. Dk King alipoambiwa na Wazungu wa Marekani aachane na siasa zake za kuwatetea weusi au atakufa alisema yupo tayari kufa kwa ajili ya usawa mbele ya sheria kwa watu wake.

  Watanzania wenzengu, vita tuliyonayo tanzania si tu kuingiza chama kingine madarakani, bali ni kuingia madarakani nchi ikiwa inafuata taratibu, kanuni, haki, usawa mbele ya sheria. Hata tukiwa na katiba mpya kama tutakubali kuvunjwa kwa sheria, na kama hatuwezi kuanza kufundisha jamii nini maana ya utawala wa sheria tutarudi pale pale kwenye kupiga kelele bila matokeo. Nchi nyingi duniani haziendelei kwa sababu tu watu au watawala wanataka, la hasha kila kosa lina sheria na kila anatenda kosa anajua atafikishwa mbele ya sheria bila kujali cheo, na uwezo wa kifedha, au hadhi yake katika jamii. Ndio maana tunaona USA na UK, France wanafikisha mahakamani viongozi wao pale wanapovunja sheria za nchi.

  Tunaweza kujitetea demokrasia yetu changa, hata mtoto anakuwa, na usipomjenga kiakili kwa kumfundisha usitegemee akajua. Huu ni wakati serikali ya CCM inatakiwa ijui wananchi hawatakai kuzulumiwa na kuwaletea muafaka wa upande mmoja.

  Uchaguzi wa Arushwa wa Meya urudiwa ili kdhihirisha haki na utawala wa sheria.
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tafadhali tafuta post aliyotuma mheshimiwa GODBLESS LEMA uisome utapata majibu yoote
   
Loading...