Muache na pesa za kuwasafirishia huko makwenu

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
7,554
9,531
:DHii tabia wanayo watu wengi sana hasa kwa walio mikoa mingine au nchi nyingine kikazi ki utafutaji unakuta mtu amezaliwa mwanza akazamia moro kajenga huko na watoto ila utamsikia mimi nikifa mkanizike kwa mababu zangu mwanza mnipeleke kabisa sasa tuwaambie wenye tabia kama hizo muandae kabisa na pesa za kuwapeleka makwenu mkiwa marehemu mpige hesabu kabisa kutoka huko mliko mpaka walikozikwa mababu zenu ni kiasi gani muweke benki ili mkikabidhi jezi msihangaishe watu mpaka wanakopa pesa wanauza vitu ili mpelekwe kwenu msiba unaisha watu wana madeni ya kutosha ili hali hata moro kuna Ardhi ya kukuhifadhi
 
Uzeni nyumba yake mkipata pesa mumsafirishe
 
Uzeni nyumba yake mkipata pesa mumsafirishe
Nimeleta huu uzi baada kukutana mvutano wa familia na ukoo kuhusu marehemu azikwe wapi wanataka kusafirisha ili hali hakuna wanataka kuuza kiwanja sasa najiuliza watoto watarithi nini iwapo wanauza assets muhimu kama hiyo ili hali wanaweza mzika huko tu
 
Watoto watapambania hali zao mkuu
 
Watu hatuna budi kupambana na umaskini kiujumla ili gharama za kusafirisha maiti zisiwe issue kihivyo!
 
Na hata mtu akiacha fedha za kusafirishiwa afapo bado wengine watadai ni bora angewaachia watoto hizo fedha. Nionavyo mimi shida ya kupambana nayo ni umaskini.
 
Uamuzi huo sio mbaya ila kama ulivyosema wafanye maandalizi mazuri. Sina uhakika kama hizi kampuni za bima zinaweza kuwa zinatoa life insurance, hii ingeweza ku cover hizo gharama.
Lakini hili la kuzikwa sehemu fulani maalum halina tija kabisa. Ukifa umekufa, kunafaida gani ukizikwa jirani na babu sijui au bibi?! Sina uhakika kama maiti zinaongea huko makaburini hadi utake uzikwe sijui jirani na mtu fulani, hili halina tija yoyote. Ila kila watu wanamaamuzi yao. Na labda hizo mila lakini lingekuwa na faida tungeshaziona lakini hakuna.
Wengi hutaka kukumbukwa, lakini hukumbukwi ikiwa hukufanya mazuri kwa watu wako wa karibu. Wakizika ndio basi.
Binadamu kuzikwa au kuchomwa baada ya kufariki mi naona yote sawa, location maalum kwangu binafsi halina tija. Unaweza kuzikwa popote na ikawa na maana ileile.
 
Back
Top Bottom