Mu-arobaini wa kukomesha wizi wa mitihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mu-arobaini wa kukomesha wizi wa mitihani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Aalim, Feb 1, 2011.

 1. A

  Aalim Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimekuwa nikikerwa sana na tatizo la kuvuja kwa mitihani mashuleni, vyuoni n.k. Kwa muda mrefu nimekuwa nikifikiria njia mmbadala kukomesha tatizo hili. Nadhani kutumia mfumo ambao nitauitwa "Open Questions System" tunaweza kumaliza tatizo hili kabisa na kulifanya kuwa historia. Mfumo ninaoupendekeza utafanya kazi kama ifuatavyo;

  1. Maswali yasiyopungua 200 yatatayarishwa kwa kila somo litakalofanyiwa mtihani na huwekwa bayana kwa watahiniwa wote mwanzoni mwa muhula.

  2. Vitabu vya kutosha vyenye maswali ya mtihani vitachapishwa na kugawanywa mashuleni, vyuoni, bookstore, kwenye web n.k

  Kwa mantiki hii maswali ya mitihani hayatakuwa siri tena hivyo nadhani hakutakuwa na haja ya kufanya njama/ hujuma ya kuiba mitihani.

  Siku ya mtihani baraza la mitihani litawajibika kusambaza vitabu vipya vya mitihani kwa watahiniwa wote. Hii itasaidia kudhibiti ujanja wa kuandika majibu katika vitabu husika; Na asubuhi hiyohiyo wakati wanafunzi wamekaa kwenye madawati yao wakisubiri kuanza mitihani, baraza litakaa na kupitisha maswali ya mtihani na kuwasilisha namba ya maswali hayo kwa shule/ vyuo husika kwa njia ya simu, fax, e-mail etc.

  Naomba mchango wenu wana JF kuhusiana na hili.
   
 2. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  ukistaajabu ya musa......................
   
 3. M

  Matarese JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35

  Mwanangu hii unayo suggest wewe sio sulution ni problem nyingine kabisaaa..... Nikipata muda nitakubandikia hapa uone kea nn ni problem. It can never work in a country kama bongo!
   
 4. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Matarese,
  Mbona idea hii ni nzuri tu, ndio implementation labda itakuwa na ugumu kiasi lakini haya ndiyo mawazo tunayopenda kuona hapa JF. Kama idea ina mapungufu, watu tunajadiliana on uses of pro's and con's na pengine wahusika kama wanapitia-pitia humu wanaweza kuchukua hatua.
  Kumbuka infrastructure hata kama bado ni changa inakua na inawezesha ishu nyingi tu. Juzi juzi tu kaingia M-PESA, na money movement imerahisishwa. Simu za mkononi ndio kila mtu anatumia (500BILLIONS spend in 3 Months) fibre network (Mkongo wa Internet) nasikia ushazamishwa tayari kwa kazi, "1-computer for every child" ndio inawezekana, na hapo itakuwa a whole new world for education. Sasa ideas kama hizi zitawezeshwa na mijadala na mapendekezo kwa wahusika.

  Comment 1 yangu kwenye hii labda ni the costs involved kuchapisha hivi vitabu. Cost ikiwa ni the production na environmental kwani inamaanisha kama kila kitabu kitakuwa na karibia maswali 200, only 50 may be used for the assessment, hence hapo kuna waste kubwa.

  Comment 2 nyingine ni kuwa, wanafunzi pia wanaweza kukariri maswali yote hayo hence hapa benefit ikapotea. Cha msingi ni kuwa, kuna jinsi ya kutengeneza nitihani kwa kutumia Weighted system. Hii inafanya kazi hivi. Katika chapter au kipengele fulani, maswali ambayo yanabeba same percentage mark yanatayarishwa, na kwenye mtihani, haitakuwa lazima wanafunzi wote kufanya mtihani sawa (question to question) ila maswali yanachanganyika na kutofautiana kati ya mwanafunzi na mwanafunzi. Hapo basi, inabidi mwanafunzi aijue hiyo topic, na sio kujua jibu ya swali specifically. System kama hiyo basi itazidisha uelewa na mwanafunzi itabidi atie bidii kuelewa somo na sio maswali/majibu.
  Sasa ukija kwenye delivery ya maswali kwenye chumba cha mtihani, basi hapo labda tuisubiri technologia iwasili au tuseme, mitihani itachapishwa kama kawaida ikitumia mwelekeo huu na kusambazwa mashuleni kama kawaida.

  Nawakilisha....
   
 5. A

  Aalim Member

  #5
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kimsingi ninachopendekeza ni kuanzishwa kwa vitabu vya maswali ambavyo vitatumika kutahini wanafunzi kila mwaka bila kubadirika. Kitakachokuwa kinabadirika ni namba ya maswali yaliyochaguliwa kwa mwaka husika hivyo basi hakutakuwa na upotevu wowote wa karatasi. Kwa mfano ikiwa sylabus yote ya PHYSICS unaiweza kuisoma katika kitabu cha ABORT basi maswali ninayo pendekeza yatatungwa kwa kutumia kitabu hichohicho na kama mwanafunzi atakuwa amekariri maswali yote hii itakuwa sawa na kukariri kitabu kizima cha ABORT. Nadhani hakuna mwanafunzi yeyote mwenye uwezo wa kufanya hivyo kwa HESABU, PHYSICS, CHEMISRTY, BIOLOGY etc.
   
 6. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimekuelewa, lakini je ishu kama
  1). Mwanafunzi kuandika notes in the book, how would that be policed?
  2). Uchakavu. Reprenishing these books still require some good planning
  3). Syllabus elasticity. Najua syllabus inapaswa kuwa stable kiasi ili mfumo wote ueleweke. Sasa kwa bongo hata nikiuliza syllabus ni ipi nadhani bado maswali yatakuwa mengi.
  4). Learning for learning sake: Je hauoni kama system kama hii itawafanya walimu ku'target masomo kwa malengo ya ku'pass mtihani? Creative teachers could use these question lists to target the learning to likely questions. Unless hicho kitabu kitakuwa na maswali 10,000, in no time you will have exhausted hiyo count ya 200 questions na hapo mwanafunzi atakuwa tu' anasoma yale bado hayajatumiwa.

  Wazo ni zuri na mapungufu yake ndio yanaweza kuwa ironed out lakini ni vyema mwanafunzi aelewe nini anachofuata shuleni, mwalimu aelewe ni nini anachofanya shuleni na mzazi aelewe amemtuma mwanafunzi huyo kufuata nini shuleni (Sio DAY CARE...), na kwa ujumla serikali kupitia wizara husika ielewe, nini maana ya shule.
   
 7. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mawazo ya mtoa mada yana uzuri wake. Lakini pia kuna mapungufu ikiwa ni pamoja na ugumu wa kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa kuelimika na si kwa kufaulu tu. Tukifuata utaratibu huo, mwalimu na mwanafunzi watakuwa wanajitahidi kumaliza ku-cover designated questions badala ya kulenga kuelewa pamoja na kupanua mawazo nje ya vitabu vilivyoruhusiwa. Hii itafanya hata walimu wasisome vitabu vingine.

  Matatizo ya mitihani hayapo kwenye kuvuja tu bali kuna namna nyingine nyingi tu ambazo watahiniwa hutumia pia "kucheat" ili kufaulu. Mapendekezo ya mtoa hoja labda yatapunguza kuvuja kwa mitihani, lakini kuibia kwa namna nyingine kutakuwa palepale.

  Mimi ninaamini kuwa kukiwa na udhibiti mzuri, na usimamiaji mzuri wa mitihani pamoja na uwepo wa adhabu KALI SANA kwa watendaji wazembe, wanaovujisha na wanafunzi wanaobia mitihani, bado utaratibu uliopo ni mzuri. Mfano, ikiwa wanovujisha mitihani watafungwa na kuzuiwa kufanya kazi yoyote ya serikali, wanaobia, wakaanikwa hadharani na kuwa blacklisted wasiajiriwe au kujiunga na taasisi yoyote ndani ya nchi kwa kusoma au kuajiriwa, hakika watu wataogopa kutenda haya makosa. Lakini hii ya sasa mtu anacheat halafu anapewa ulaji serikalini, ina-encourage cheating. Bottom line ni kwamba sheria na kanuni za mitihani zinatakiwa kurekebishwa na matatizo ya uvujaji pamoja na kuibia yakawa minimized.
   
Loading...