Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,874
- 7,650
Katika hali isiyoeleweka sawa sawa miongoni mwa wananchi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani na Wilaya zilizoko Mkoa wa Mtwara, shirika la Umeme nchini limeanza Mgao Mkali wa Umeme kila siku.
Maeneo yanayoathirika zaidi ni Mangowela, Magomeni, Sabasaba, Maeneo ya stendi ya Mkoa na Gereza la Mkoa Lilungu pamoja na Mangamba, Masasi Mjini na Newala Mjini.
Hakuna afisa yeyote wa Tanesco aliyekuwa tayari kuzungumzia sababu za Mgao huu ambao huanza kila siku saa Moja usiku.
Mtwara ni mmoja kati ya mikoa ambayo haipo katika gridi ya Taifa na wananchi wamekuwa wakielezwa Chini kwa Chini kuwa Mgao huu ni matokeo ya wana Mtwara kutoichagua CCM katika uchaguzi mkuu wa Maana 2015.
Habari ambazo zimezagaa katika vijiwe kadhaa hapa Mtwara zinasema, maeneo ya Shangani na Indian Quarters ambayo hasa hukaliwa na viongozi wakubwa wa Chama na Serikali, hayakumbwi na mgao huo hivyo kuaminisha hisia za wananchi kuwa WANAKOMOLEWA.
Mgao huu una zaidi ya Mwaka sasa na wananchi wa Mtwara wanateseka huku Tanesco ikinyamaza kimya na kuacha wananchi wakiwa na sintofahamu huku wakihusisha mgao huo na matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2015