Mtwara: Watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa kukutwa na noti bandia

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Jeshi la polisi mkoani Mtwara limewakamata watu 2 kwa tuhuma ya kukutwa na noti bandia,zenye thamani ya jumla ya shilingi 770,000 eneo la Magomeni Migomigo katika manispaa ya Mtwara/Mikindani.

Kamanda wa polisi mkoani Mtwara naibu kamishna wa polisi Lucas Mkondya, bila kutaja majina ya watu hao kwa maelezo kuwa uchunguzi unaendelea, amesema watu hao walikamatwa baada ya kuwekewa mtego wakiwa kwenye shughuli za ulaghai na kuwaibia wananchi kwa kutumia fedha hizo za bandia, na kwamba walipohojiwa, walieleza wamekuja Mtwara wakiwa na shilingi milioni moja, fedha hizo za bandia.

Aidha kamanda Mkondya mbali na kuwataka wananchi kuwa makini noti hizo, kwa kuwa zimechapishwa zikiwa na namba za kufanana, amesema polisi imeanza msako mkali wa kufuatilia mtandao mzima wa watu wanaojihusisha na uchapishaji wa noti hizo za bandia na kujua wapi zinakochapishwa, kwa kuwa watuhumiwa hao walipoojiwa, wamesema wenzao wengine wametumwa kwenye mikoa mingine kwa ajili ya kusambaza noti hizo.

Katika tukio jingine, kamanda Lucas Mkondya amesema idadi ya waliopoteza maisha mkoani Mtwara kufuatia mvua zilizonyesha mkoani humo kwa siku 2 mfululizo imefikia 2, baada ya mtoto mwingine Jalia Mussa mwenye umri wa miaka 4 kufariki dunia kijiji cha Kitere baada ya kutumbukia kwenye shimo lililojaa maji ambalo hutumika kama kisima, mwingine aliyepoteza maisha ni mtoto Samson Sanga.

Chanzo: ITV
 
Noti bandia inajulikana tu

jinsi ya kuitambuaa

a/ ule mkanda kwenye noti ukiuchezesha una kitu kama diamond inacheza cheza

b/ kwenye mwanga kuna picha ya nyerere

c/ kwenye maandishi ukiyapapasa yanakuwa wanakwaruza

d/ kuna taa maalum zinatumia ultra violet light ukizimulika katika giza zinang'aa sana

e/ nyuma ya hela kuna yule twiga ukichezesha noti huwa anang'aa kama rangi ya dhahabu
 
Back
Top Bottom