Mtwara: Watoto 11 wa kiume hawajulikani walipo kwa zaidi ya siku 10. RPC asema huwenda Watoto hao wameenda Msumbiji kwani walishawahi kukamatwa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Hofu na vilio vimetanda miongoni mwa baadhi ya wazazi, ndugu na jamaa katika Kijiji cha Mtimbwilimbwi Halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara baada ya watoto 11 wa kiume wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kutoweka kwa zaidi ya siku 10 na bado haijulikani walipo.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda amesema Serikali ina taarifa hiyo ya watoto kutoweka na wameshawahoji wazazi kujua kama wanafahamu walipo watoto wao huku akisema kwa sasa ni msimu wa korosho na inawezekana wapo kwenye mashamba ya wakulima wakubwa wakiokota korosho.

Amesema jitihada za kuwatafuta watoto hao zinaendelea, pia ametoa wito kwa wazazi kuwa karibu na watoto, hasa kipindi hiki cha msimu wa korosho kwani baadhi ya wakulima wakubwa huwachukua wototo kama vibarua jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

UPDATE
Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP Blasius Chatanda amesema jumla ya watoto 11 waliotoweka katika kijiji cha Mtimbwilimbwi, Halmashauri ya Nanyamba huenda wakawa wameenda nchini Msumbiji

Amesema kulingana na historia iliyopo juu ya watoto hao kuwa waliwahi kukamatwa na Maafisa wa Usalama wa nchini Msumbiji kwa makosa ya uhalifu na kurejeshwa Nchini, huenda hata sasa wakawa wameenda nchini humo

Amesema, "Hawa watoto waliwahi kuingia kwenye makundi ya uanaharakati nchini Msumbiji, wakakamatwa na kurejeshwa. Wapo wengine watu wazima hapo Kijijini wameondoka na wameacha familia zao, tunaamini huenda hawa nao wameendoka nao, sio kwamba wametekwa ama kuuawa”

Watoto hao 11 wanadaiwa kutoweka wote kwa pamoja, kati ya Oktoba 10 na 15, 2019, na kwamba Jeshi la polisi mkoani humo, linafanya mawasiliano na vyombo vya ulinzi na usalama nchini Msumbiji ili kuangalia namna ya kuwapata
 
Yawezekana msimu wa korosho umewabeba watoto pamoja na watu wazima pia maana fikiria iwapo mtu analipwa sh 10000 kwa siku hadi msimu uishe atakuwa na kiasi gani cha pesa?
 
Ukiunganisha haya matukio pamoja na lile la utekaji wa kijiji hicho utagundua kuna wakubwa wanataka kutuchonganisha!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom